Maswali na ushauri kwa Malinzi

Nadhani utakuwa hujanielewa mimi sipingani na wazo la kusambaza mpira mikoani lakini lazima tuwe na mpango mkakati na si kukurupuka sababu viwanja vingi vya mikoani ni vibovu havifai kabisa sasa kama tumedhamilia kusambaza soka mikoani hasa kwa mechi za kimataifa lazima tuvifanye viwanja hivyo kuwa na hadhi hasa pitch mbona tumeshuhudia mechi kubwa zikichezwa kirumba mwanza yote ni sababu uwanja wa kirumba una hadhi hiyo na si mikoa yote.

Mmmh hizo takwimu zako mbona zinaegemea upande mmoja ok pia uwanja huo huo wa taifa stars iliifunga Morocco goli 3, ikaifunga cape velde goli 3, ikaifunga cameroon goli 1, ikaifunga sudan goli 3 ikaifunga algeria goli 2 sasa sijui kama unatambua maana ya neno takwimu.
 
Nimetaja mechi hizo kwa kuwa tulifungwa katika mechi ambayo ushindi ungetusogeza hatua fulani. Kuhusu pitch ni majuzi tu ile ya Sokoine ilirekebishwa kwa maagizo ya TFF kwa hiyo nadhani iko vizuri.

Wakati mwingine uwanja mbovu unaweza kuwa na faida hasa unapocheza na timu ambazo zimezoea viwanja vizuri, kwa hiyo kuna faida na hasara.
 
Hivi ni vigezo gani vilivyo tumika kubadili rangi ya jezi Taifa stars.?
Mbona rangi yenyewe haina mvuto,halafu tofauti kabisa na bendera ya Taifa
 
Hivi ni vigezo gani vilivyo tumika kubadili rangi ya jezi Taifa stars.?
Mbona rangi yenyewe haina mvuto,halafu tofauti kabisa na bendera ya Taifa

idawa ni kweli watu wengi wamelalamikia hizi jezi.Jezi hizi tulizipokea kutokana na TFF kusaini mkataba na adidas kupitia msaada wa CAF,mwisho wa kuxitumia itakuwa ni desemba,tutazibadilisha
 
Last edited by a moderator:
kwahiyo ile draw na senegal pale mwanza ni sababu ya mechi kuchezwa mkoa ule? { taifa starz na Senegal 1-1 ]
 
kwahiyo ile draw na senegal pale mwanza ni sababu ya mechi kuchezwa mkoa ule? { taifa starz na Senegal 1-1 ]

Inaweza isiwe sababu pekee, lakini hamasa ya raia wa kule ilichangia kujiamini kwa wachezaji wetu. Dar kidogo tu zomea zomea...
 
Inaweza isiwe sababu pekee, lakini hamasa ya raia wa kule ilichangia kujiamini kwa wachezaji wetu. Dar kidogo tu zomea zomea...

Ni kweli lakini hiyo zomea zomea uwa ina sababu na baadhi ya mechi na hasa mechi ambazo watu wanaamini timu inafanya vibaya believe me hata uko mikoani mathalani mechi ziwe zichezwa mfululizo uwanja wa sokoine mbeya halafu timu isifanye vizuri na wao watazomea tu washabiki wa Tanzania ni wale wale hatuna uvumilivu hasa timu inapofanya vibaya.
 
idawa ni kweli watu wengi wamelalamikia hizi jezi.Jezi hizi tulizipokea kutokana na TFF kusaini mkataba na adidas kupitia msaada wa CAF,mwisho wa kuxitumia itakuwa ni desemba,tutazibadilisha

Hamkuwapa mapendekezo ya rangi mnataka ziweje? Au sbb ni msaada basi wameingia stoo na kutoa kilochopo safisha ghala
 
Last edited by a moderator:
Hamkuwapa mapendekezo ya rangi mnataka ziweje? Au sbb ni msaada basi wameingia stoo na kutoa kilochopo safisha ghala

Walichouliza ni :tuambie rangi za bendera yenu ya Taifa" thats it kilichofuata ni kutuletea kontena
 
in rain or sunshine you will never walk alone,Liverpool motto,ya kwetu?
 
idawa ni kweli watu wengi wamelalamikia hizi jezi.Jezi hizi tulizipokea kutokana na TFF kusaini mkataba na adidas kupitia msaada wa CAF,mwisho wa kuxitumia itakuwa ni desemba,tutazibadilisha

Hivi mheshimiwa rais kwa hatua tuliyofikia ya kuwa na udhamini mkubwa wa maana wa wa TBL kupitia bia yake KILIMANJARO kulikuwa na haja ya kuingia mkataba wa kupewa msaada wa jezi wakati hilo halikuwa tatizo hata kidogo kwenye timu yetu ya Taifa. Ndugu Malinzi huoni haya ni maamuzi mabovu kabisa kuwahi kufanywa?naomba majibu tafadhari. Halafu napenda kujua hizo jezi ziliendana na kupatiwa kiasi chochote cha hela na hao Adidas au tumepewa jezi tu tuvae utadhani tulikuwa tunacheza bila jezi.
 
Hili suala la jezi nafkiri Rais amelisemea,kwamba mkataba ulisainiwa kabla hajaingia madarakani..
Labda atuambie kwenye huo mkataba wa Msaada hakuna kipengele tunachoweza kutumia ili tuache kuvaa hizi Jezi...
Siamini kama TFF Na Timu yetu ya Taifa ina Sababu ya kutafuta msaada hadi wa Jezi..Hii ni aibu sana..Ona sasa tulicholetewa??
Hivi kabla ya Jezi kutumika si huwa zinaonyeshwa kwanza design,rangi n.k?? MH;Rais hii ni timu ya Taifa hebu kuweni serious kidogo..
 
Mchakato wa ku design jezi mpya za National teams zetu unaendelea,tukijaliwa utakamilika mwaka huu,itakuwa ni kwa jezi za home na away.
 
Mchakato wa ku design jezi mpya za National teams zetu unaendelea,tukijaliwa utakamilika mwaka huu,itakuwa ni kwa jezi za home na away.
mlitangaza tenda magazetini ili wengine wenye uwezo tu design kisha tupambanishwe..?au mie sikuona tangazo hilo..?
..ok..naweza kudesign na kisha kuleta kwenu? na ikiwa katika animation pia..
 
mlitangaza tenda magazetini ili wengine wenye uwezo tu design kisha tupambanishwe..?au mie sikuona tangazo hilo..?
..ok..naweza kudesign na kisha kuleta kwenu? na ikiwa katika animation pia..

Mkuu, umeniwahi nami nilikuwa na swali hilo hilo, maana inasikitisha katika ukanda wa kusini, nchi yenye jezi dhaifu ni ya kwetu, yaani hata ku design tu hatuna kweli uwezo?
 
Mr President Malinzi,
Nadhani utakumbuka, wasiwasi wangu wakati umeunda kamati kuteua wachezaji wa timu ya Taifa, nikakwambia tangu lini timu ichaguliwe na mtu ambaye hataifundisha? sasa tumeona, anyway tusitake kurudi nyuma kuuliza gharama zilizotumika maana tutaleta ya kuleta.

leo nakuomba, ili uache legacy, kazania kuimarisha ligi yetu iwe nzuri na yenye hadhi, kutoka pale tutapata timu imara ya Taifa, hili la academy waachie private sector. TFF inaweza kuwa mshauri tu, hasa katika kuisaidia serikali kuimarisha mashindano ya mashule.

Umechaguliwa kujenga soka ya bongo na wala si kuuza wachezaji nje, please nina wasiwasi na huyu mshauri wako wa mambo ya soka.
 
hiyo pool ya wachezaji qa kucheza ligi kuu unawapata wapi kama huna mfumo imara wa grassroot na youth development? Lazima turudi kwenye drawing board tujenge mfumo wa mpira wa vijana na tutafute pesa za kuu fund,maendeleo ni gharama
 
Mh Rais mfano wa Youth Development programs kuendeshwa na Football Association unatumika nchi gani??
Labda inawezekana hatuna habari kiundani zaidi..
 
Mh Rais mfano wa Youth Development programs kuendeshwa na Football Association unatumika nchi gani??
Labda inawezekana hatuna habari kiundani zaidi..

correct wording: Youth Football development programme,huu utaratibiwa na TFF,wadau wote watahusishwa ie serikali,NGO's,kampuni binafsi na za umma,wewe na yule etc
 
correct wording: Youth Football development programme,huu utaratibiwa na TFF,wadau wote watahusishwa ie serikali,NGO's,kampuni binafsi na za umma,wewe na yule etc
Mh, hujajibu swali, tunaomba utupe mifano, in nchi zipi? Unajua unaua Mpira kabisaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…