MKALIKENYA
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 1,196
- 486
Twende kitakwimu labda, kati ya mechi zilizochezwa Dar na mikoani ni zipi ambazo timu ya Taifa ilifanya vizuri. Hapa nimeshashuhudia tukufungwa na Msumbiji na kushindwa kufuzu AFCON 2008, tukaja kupigwa tena na Kodivaa na ndoto za WC2014 zikakomea hapo.
Nasapoti timu kucheza mikoani kwa kuwa washabiki wa mikoani ni wazalendo kuliko wa Dar, washabiki wa timu fulani huzomea timu ya Taifa kama wachezaji wao hawajaitwa kwenye kikosi, kuna kipindi John Boko alistaafu timu ya Taifa kutokana na upuuzi wa mashabiki wa Darisalama, mambo haya hayapo mikoani poti.
Azawaizi naungana na Jamal Malinzi kuwa tuusambaze mchezo mikoani na sio kila siku kukomaa na jiji moja tu.
Nadhani utakuwa hujanielewa mimi sipingani na wazo la kusambaza mpira mikoani lakini lazima tuwe na mpango mkakati na si kukurupuka sababu viwanja vingi vya mikoani ni vibovu havifai kabisa sasa kama tumedhamilia kusambaza soka mikoani hasa kwa mechi za kimataifa lazima tuvifanye viwanja hivyo kuwa na hadhi hasa pitch mbona tumeshuhudia mechi kubwa zikichezwa kirumba mwanza yote ni sababu uwanja wa kirumba una hadhi hiyo na si mikoa yote.
Mmmh hizo takwimu zako mbona zinaegemea upande mmoja ok pia uwanja huo huo wa taifa stars iliifunga Morocco goli 3, ikaifunga cape velde goli 3, ikaifunga cameroon goli 1, ikaifunga sudan goli 3 ikaifunga algeria goli 2 sasa sijui kama unatambua maana ya neno takwimu.