Maswali na ushauri kwa Malinzi

ikizu waamuzi hawabadilishwi bila sababu ya msingi na si kila maamuzi tutakuja kuyatolea ufafanuzi jf.
TFF ikiamua kuwa inaunda kamati au kutekeleza maamuzi yake kwa kuangalia nani yanga/simba/azam/mtibwa/ndanda/coastal etc basi hatutakaa tufanye maamuzi kwenye mpira wa nchi hii.Midhali wenyeviti wa hizi kamati wamekugusa,niambie ni maamuzi gani wameyatoa ambayo wewe unayaona ni yanaegemea upenzi wao wa klabu.
Kwenye hili la kuunda kamati ya uendeshaji wa ligi,hii ni kamati NDOGO ya bodi ya ligi na tangia BODI ianzishwe siku zote imekuwa ikisikiliza na kutoa maamuzi kwa masuala ambayo ni NON APPEALABLE na hii mandate Bodi imepewa na kanuni za BODI ya ligi ambazo uongozi wangu umezirithi toka awamu iliyopita.Kamati ya utendaji ya awamu iliyopita ndiyo ilitengeneza kanuni hizi,mbona ulikuwa hujawahi kulalamikia hilo.Malinzi kuboresha utaratibu ambao tayari ulikuwepo imekuwa nongwa?Nia yetu ni kuhakikisha maamuzi yanatolewa ndani ya muda mfupi na sio hadi umma upaze sauti.
 
Last edited by a moderator:

Mheshimiwa Jamal Malinzi, hadi leo hii tunangoja kujua jezi mpya ya Taifa Stars.
Kila tumikia simu huko offisini tunaambiwa.. ngoja tutatangaza... Tuambiane sasa tusuburi hadi lini?
Tupatie kauli isiyo tata.!
 
Last edited by a moderator:
Mheshimiwa Jamal Malinzi, hadi leo hii tunangoja kujua jezi mpya ya Taifa Stars.
Kila tumikia simu huko offisini tunaambiwa.. ngoja tutatangaza... Tuambiane sasa tusuburi hadi lini?
Tupatie kauli isiyo tata.!
Washindi watapewa zawadi zao muda si mrefu na jezi kuzinduliwa
 
Tickets za mechi ya leo Yanga vs BDF zinapatikana kwa mfumo upi..?
 
Rais vipi kuhusu adhabu kwa wale watu walijihusisha na matukio ya vurugu katika michezo hasa tukio lile lililofanywa na Katibu wa Simiyu kwa kumpiga mwamuzi makonde mpaka leo sisi wadau hatujui huyu jamaa ameadhiwa au la? maana tunavyojua aliitwa na kamati ya maadili lakini hakuhojiwa kwa sababu ya muda ulikosekana kwa wajumbe baada ya kuanza kikao muda ukiwa umeende.
tafadhali tujuze
 
Mr. President hivi kwanini tunafeli kwa vijana, wapo vijana mbao wanaanza na kuonesha dalili nzuri lakini ghafla upotea eg. ile serengeti boys ya wakina Nurdin Bakari iliyotolewa kwa kukiuka taratibu na hawa watoto walio win kikombe huko SA.
Hivi ni kweli tunashindwa kuwaweka vijana pamoja hata kwa miaka mi5 kisha kufanya yale yaliyofanywa na Senegal WC?
 
ikizu mr wise katibu wa simiyu alishinda kesi baada ya kukosekana ushahidi na TFF hatukukata rufaa.
Hili la soka ya vijana tumechukua hatua tukianzia na dream team ya copa coca col 2014,tunaichukua na kuiweka kambini kuiandaa na Africa qualifiers U17 mwezi juni mwakani.
 
Last edited by a moderator:
hivi raisi,hili swala la kuongeza wachezaji wakigeni wafike hata 10 linafanyiwa kazi kwenye..!?
maana hawa wachezaji wakibongo wanaturudisha nyuma sana hususan kwenye virabu vyetu hivi..
 
Mkuu Jamal Malinzi ni muda kiasi umepita tangia uchukue hatamu za Urais kukiongoza chama chetu cha mpira wa miguu. Je tangia uchukue madaraka hayo hadi sasa ni mafanikio gani ambayo unaweza kuwaambia watanzania wapenda mpira kwamba umeyapata ndani ya muda wa uongozi wako hadi leo hii?

Pili, bila shaka kuna changamoto ambazo umekumbana nazo tangia umeingia madarakani ikiwemo kushutumiwa kuwa wewe ni mkabila na pili una uyanga; je hadi sasa ni changamoto gani ambazo unaona zinakukwamisha kufikia malengo yako na unazikabili vipi hizo changamoto?
 
Last edited by a moderator:
Sijui hawa watu wanaongelea ukabila wanatoka wapi. Kwanza Jamal hausiki na ajira ya wafanyakazi TFF kazi inatangazwa magazetini na kila raia anarihusiwa kuomba kazi na akishinda mahojiano hanaajiriwa. Kumbukua kuna chombo maalumu kinachofanya usaili wala Jamal hausiki kabisa hii imetokeo by incindent wengi waliopata kazi ni watu wa kutoka Bukoba. UkabilaTanzania haupo. Mimi naona watu wanoongelea ukabilau hata kuuliza ukabila nafikiri wao ndo wana ukabila. Nafikiri hapa tuongelee football hakuna haja ya kupoteza muda na mawazoyaliyopitwa na wakati
 
hivi raisi,hili swala la kuongeza wachezaji wakigeni wafike hata 10 linafanyiwa kazi kwenye..!?
maana hawa wachezaji wakibongo wanaturudisha nyuma sana hususan kwenye virabu vyetu hivi..

guti kabla ya kufikia maamuzi juu ya ni idadi gani ya wachezaji wa kigeni tuwaruhusu kusajiliwa na vilabu huwa tunakaa na vilabu vyote na kufanya kikao nao maana wao ndio wadau wakuu.Kikao cha mwisho tulikubaliana wawe watano tu.Jambo hili bado linaweza kujadilika.
 
Last edited by a moderator:
Kimbunga mwisho wa siku Watanzania wanachotaka ni kuona matokeo mazuri uwanjani.Swali ni je sisi kama nchi tunawekeza kiasi gani kuhakikisha timu zetu za vijana ambazo ndilo chimbuko la Taifa na Twiga stars zinafanya vizuri.Mtihani mkubwa uko hapo.
 
Last edited by a moderator:
Kimbunga mwisho wa siku Watanzania wanachotaka ni kuona matokeo mazuri uwanjani.Swali ni je sisi kama nchi tunawekeza kiasi gani kuhakikisha timu zetu za vijana ambazo ndilo chimbuko la Taifa na Twiga stars zinafanya vizuri.Mtihani mkubwa uko hapo.

Ahsante Mr President. Haswaaaa matokeo uwanjani ndicho tunachokitaka. Lakini pia TFF ndio inatakiwa iweke mipango thabiti ili watu na serikali wajitokeze kuwekeza. Nakumbuka JK aliwekeza mwanzoni kwa kumleta Maximo, nchi ikachangamka, timu yetu ikapata support toka kwa wananchi lakini baadaye naona tena mambo hayajaenda vyema na JK naona kama kakata tamaa wananchi nao wamekata tamaa. Timu bado kama vile ni kichwa cha mwendawazimu. Je Uongozi wako una mipango gani na mipango hiyo imefanikiwa kwa kiasi gani?
 
Mtaacha lini kupangua pangua ratiba, nimesikia mgambo wapo mbeya ninyi mmewapa ratiba mpya wacheze tanga, hiyo ni Sawa?
 
j malinzi unamatatizo gani na tff hizi ratiba za ligi hazieleweki kanuni za ligi zinatungwa watu wakiweka mikono mifukoni au mnapanga mkiwa bar
 
Kawaida siku zote kanuni za mashindano yoyote utungwa mwanzo wa mashindano na kuwa ndio mwongozo sasa hii ya kuleta kanuni katikati ya rigi nyie mmeipata wapi? Na mchezaji kucheza na kadi nne za njano
 
Kitulo na wakimataifa mabadiliko ya ratiba mara nyingi yanatokea tokana na matukio mbali mbali mfano matakwa mahsusi ya timu ya Taifa au vilabu vinavyoshiriki michuano ya Afrika.Nikupe mfano,mwaka huu 2015,Tanzania tutashiriki qualifiers za CHAN,AFCON na World cup Russia.CHAN na WC qualifiers tutaanzia mtoano.Ratiba ya ligi kwa vyovyote vile itategemea tuta progress vipi katika knock out hizi.Hali kadhalika kwa Yanga iliyo kwenye mashindano ya Afrika.Wengi wanasema mbona Ulaya hawabadilishi ratiba,hao wanasahau kuwa wenzetu miundo mbinu yao inarahisisha usafiri na size ya nchi zao nyingi ni ndogo kulinganisha na Tanzania hivyo ni rahisi jumatano kucheza Ufaransa na jumamosi ikacheza Manchester.Sisi ukicheza jumamosi Tunis ndo basi tena wiki kwenye ratiba imepotea hiyo.
Mfano mechi ya away confederation cup Yanga watacheza kilomita zaidi ya mia moja nje ya Bulawayo Zimbabwe,watoke hapa waende Harare waruke kwenda Bulawayo,waendeshe gari kwenda uwanjani mgodini watarudi lini nchini kucheza ligi?
 
Last edited by a moderator:

sawa nimekuelewa na hili la kanuni la kadi za njano naona yanga analipigia kelele na vilabu vingi hawaijui kanuni hiyo
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…