Malinzi, jana nimekushuhudia ukisema kwa kinywa kipana kabisa kwamba Kamati ya Utendaji ya TFF ilishampa majukumu kocha wa Timu ya Taifa na hivyo hawezi kutoka. Ukasema Kamati ya Utendaji ya TFF imempa kazi ya kuipekeka CHAN timu ya Taifa na hivyo hata ikifungwa kocha hawezi kutolewa. Atatoka tu ikiwa atashindwa kuipeleka timu CHAN! Watu wanataka kocha aende zake tupate kocha atakaye tuletea ushindi lakini wewe unasema Kamati ya Utendaji ilishaamua, hivi Kamati ya Utendaji ni kwa ajili ya nini? Tunataka mpira, tunataka ushindi, hatutaki maamuzi ya Kamati ya Utendaji ambayo hayatusaidii.
Unataka hadi tufungwe na nchi gani ndio Kocha aondoke? Tumefungwa na Swaziland ambayo ni nchi unayoweza kuizunguka kwa siku moja, bado tunataka tufungwe na nani ili kocha aonekane hafai?
Hivi Ndugu Malinzi kwa maana hiyo Kuipeleka timu AFCON siyo jukumu la Kocha? Kwa nini tunatumia pesa zetu kuipeleka timu nje ya nchi kwenye mashindano ya AfCON? Naona kwa hakika kuna shida kubwa huko TFF.
Malinzi tunataka mpira, tunataka kocha wa kuleta ushindi, hatutaki utetezi wa maamuzi ya kamati ya utendaji ambayo yahatusaidii.