Maswali na ushauri kwa Malinzi

Maswali na ushauri kwa Malinzi

muheshimiwa malinzi hivi tff unayoiongoza wewe nayo pia inatengenezewa tiketi na kampuni za nje?

tukijaliwa kuanzia ligi msimu huu tiketi zitakuwa ni za electronic kupitia benki ya crdb
 
Hana na hawezi kukupa...
Kifupi musonye alijua yanga ikienda kigali kamili ataweza.kupata watazamaji..wengi kule kigali yanga inapendwa rejea walivyochukua ubingwa walimpelekea kombe kagame...

Sasa cecafa wakajua kuwa kagame ya mwaka huu watapiga hela kupitia yanga...rayon..apr....rayon na apr zinapendwaa rwanda.. ukiongeza na yanga..viwanja vinge jaa...kutokuwepo kwa yanga ndio kapanic mkenya wa watu...bora aondoke..tu...

Kipaji Halisi hili la Yanga na cecafa siai kama federation we tried our best kuokoa situation na hili Yanga wanajua,walichoamua cecafa ndo hicho.
 
Last edited by a moderator:
Yombayomba inahitaji muda na utulivu kuingia kwenye ukurasa huu na kujibu hoja za wadau,wiki nne hizi TFF imekuwa na mechi nne za kimataifa senior na U17 home and away,na wiki nzima hii tuna ujumbe mzito wa FIFA,isitoshe nina shughuli zangu binafsi za kuniingizia kipato,muda nikiupata kama leo naingia na kujibu hoja,tuwe na subira na hakuna hoja naogopa kuijibu.Kusifiwa hakuniongezi tija,ni bora kukabiliana na changamoto.
Haya tunasubiri majibu au tamko lako rasmi
 
Mr prezidaa tunahitaji majibu ya vigezo vilivyotumika kuitoa Yanga ktk mashindano ya kagame

cecafa walidai Yanga wapeleka a youth squad,bila shaka kuna majina waliyatarajia,ni jambo gumu kwa TFF kulielezea maana hatukutaka Yanga iondolewe.
 
wakuu unajua musonye ana shida na yanga muda mrefu tu toka yanga walipokataa kuingiza timu kucheza na simba mwaka ule na kuanzia hapo amekua akiwaundia zengwe sana. pia tff bila kujua wameingizwa mkenge na wao wakaingia kama yanga ilikosea waliotakiwa kuwajibishwa ni tff kwa kuyapitisha majina hayo

Shark TFF tungekataa kuyapitisha kwa kanuni ipi?
 
Last edited by a moderator:
Asante Mkuu kwa kunisoma, ningependa kuona jambo hili halipiti hivi hivi, viongozi wa TFF waliohusika katika hili wachukuliwe hatua. Siyo lazima wafutwe kazi wanaweza kuandikiwa barua za onyo kuonesha kuwa walichokifanya ni upumbavu mtupu.

makoe matale viongozi wa TFF wawajinishwe kwa lipi? Kwa kupeleka jina la Yanga cecafa na players list? Its all we did.
 
Last edited by a moderator:
Hili ni swali kutoka kwa mdau #mansoorsaid ameliuliza katika thread nyingine, nimelileta huku kwako mkuu. Lipo hivi
"J .Malinzi huwa unapita jf naomba jibu tff ni mwanachama wa fifa.je iweje tff iwe mwanachama wa chama ambacho sio mwanachama wa fifa? chama chenyewe ni cecafa
la pili yanga ilipeleka majina kwenda kagame cup na hayo majina tff mliyathibisha je hayo majina yalikuwa sahihi

tunaomba majibu ya kina"

SaaMbovu FIFA na CAF wanazitambua associations hizi kama cecafa,cosafa nl na ndio maana kwenye congress za FIFA na CAF wanakaribishwa kama wagwni maalum na hata kuhutubia congress,they are regional groupings.
Ni kweli Yanga walituletea orodha na sisi tukaipelwka cecafa kwa jinai ilivyokuwa.
 
Last edited by a moderator:
Malinzi,

Swali ni kuwa ni kipengele gani, ambacho hata kinalazimisha timu ipeleke kocha gani? Hivi mpira wa Tanzania utakuzwa na CECAFA?

TFF, ilitakiwa ionyeshe ukomavu, heshima ya nchi ilitakiwa kuwekwa mbele. Leo ni Yanga kesho tutaambiwa hata timu ya Taifa ije na nani./ Hata Azam, hawakuonyesha uzalendo, ni kitendo cha kipuuzi kufurahia kwenda wakati Taifa lako lina dhalilishwa.

Kama Musonye alikuwa hataki, tuanze kujenga timu ya mchanganyiko na vijan, kwani ni lazima timu za Tanzania zishiriki? kwa nini hatujifunzi uamuzi wa serikali kukataa kuendesha kwenye EAC?

Malinzi, hili swala ni sensitive, ukweli TFF, au kiongozi aliye handle kaishusha heshima ya Taifa letu, anatakiwa ajiuzulu.
 
hilo ki kweli mheshimiwa mi biinafsi nakuonea huruma sana jinsi unavyoendesha mpira kwny mazingira magumu km hya coz duniani kote vilabu ndyo vinanafanya timu ya taifa kuwa bora kwa mfano huwezi kuzungumzia mafanikio ya timu ya taifa ya ivory coast bila kuizunngumzia asec memosa vile vile huwez kuzungumzia mafanikio ya spain bila kuzungumzia Barcelona vile vile ujerumani na bayern Munich pamoja ghana na libety professional so utaona kwa staili hii ni ngumu kufikia mafanikio ya kweli ya kimpira ukichanganya na kukosa exposure na kutojjitambua kwa wachezajii wetu(rejea ishu ya kapombe na boban) ukichanganya na udhaifu Wa ligi yetu ( mechi chache sana 26?????) bado na rushwa na upangaji matokeo ndyooo kabsa soka letu liinazidi kuzama

komeka we acha tu,ahsante kwa kulitambua hilo.Ifikie wakati vilabu (hasa hivyo vinavyoitwa vikubwa) vitambue kuwa in thw long term kutafuta ubingwa wa papo kwa papo kwa kutumia wachezaji wa nje hakuwasaidia,kuwekeza kwa vijana ndio nguzo ya mpira wa nchi yoyote duniani.
 
Last edited by a moderator:
Imezoeleka Tz kuwa ni kichwa cha wenda wazimu ktk soka na cha ajab zaidi Ukweli wa maneno haya bado timu za mpira zinauthibitisha.Licha ya jitihada kadhaa za TFF ,serikali,Vilabu na taasisi mbalimbali ktk kuibua vipaji vya vijana tatzo bado vipaji vinavopatikana haviendelezwe,nafkir tutaungana kuwa tatizo ni umaskini.Sasa bas mh. kunahaja ya kuwa na mifumo tofauti inayoendana na uhalisia ulivo sasa bas pendekezo langu ni hili,TFF UNDENI TIMU ZA VIJANA ZA KUDUM ANGALAU MBILI AU PENGINE HATA MOJA NA IINGIZENI KTK MIKIKI MIKIKI YA LIGI KUU pana faida nyingi za kufanya hivo.Au vp mzee wangu.

JITU PEVU uko sahihi kabisa na mimi nakuhakikishia tutafanya hivyo,stay tuned
 
Last edited by a moderator:
Malinzi,

Rejea habari za Yanga kukataliwa kupeleka timu ya vijana, nauomba uongozi wa TFF utoe ufafanuzi, ni wapi ilipoandikwa kuwa timu iwakilishwe na nani? Kama nia ni kukuza soka la ukanda huu, basi hii ni kitu cha ajabu saana, nia na dhamira ya Yanga ilitakiwa kuungwa mkono, kwani ilikuwa inatoa nafasi kuwajenga vijana kwa ajili ya baadae, ambayo ni faida kwa Yanga na Taifa stars. Pili imeandikwa kuwa MUSOKE ana uliza kwa nini Maximo haendi? Hivi ni busara kweli yeye apangie timu nanani awe mwalimu? Mbona hakuwapangia Harambee Stars mwalimu wa kuipeleka Lesotho? Kuna ubaya gani kwa Yanga kuanza kumjenga Nsajigwa kuwa kocha?

Kama sera yako ni kuinua vijana, imekuwaje TFF mkubaliane na kusalimu amri kwa kitu ambacho hakipo kwenye sheria? Huu ni udhaifu mkubwa mno, na wala hausaidii kujenga soka la CECAFA.

mluga yako mambo si ya kueleza hapa,suffice to say TFF tulifanya jitihada Yanga icheze ikashindikana,too sad.
 
Last edited by a moderator:
Jamali Malinzi
natamani kujua aina ya wadau..wafadhili na washirika wa karinu wa tff na mipango yao
mikataba ambayo iliingia tff..mikataba ambayo imeingia tff ..na mikataba ambayo itaingia tff katika kukuza soka letu

mtu chake hadi sasa mikataba tuliyonayo ni ya TBL /taifa stars,vodacom na azam media/premier league na mingine ya copa coca cola na airtel rising star.
 
Last edited by a moderator:
Jamal Malinzi mkimuachia Musonye wa CECAFA ipo siku atawaambia lzm team ya Tanzania inapocheza michuano fulani mkuu wa msafara awe Waziri Mkuu!
Kupeleka team B lilikuwa ni jambo la kuungwa mkono na kila mpenda michezo maana kwa sasa hawa akina Canavaro wamezeeka wawapishe vijana wapate uzoefu!!
Kama Rais wa soka la Tanzania ndiyo kauli ya Musonye haipingwi?

Malafyale wala haikuwa timu B
 
Last edited by a moderator:
Malinzi,

Swali ni kuwa ni kipengele gani, ambacho hata kinalazimisha timu ipeleke kocha gani? Hivi mpira wa Tanzania utakuzwa na CECAFA?

TFF, ilitakiwa ionyeshe ukomavu, heshima ya nchi ilitakiwa kuwekwa mbele. Leo ni Yanga kesho tutaambiwa hata timu ya Taifa ije na nani./ Hata Azam, hawakuonyesha uzalendo, ni kitendo cha kipuuzi kufurahia kwenda wakati Taifa lako lina dhalilishwa.

Kama Musonye alikuwa hataki, tuanze kujenga timu ya mchanganyiko na vijan, kwani ni lazima timu za Tanzania zishiriki? kwa nini hatujifunzi uamuzi wa serikali kukataa kuendesha kwenye EAC?

Malinzi, hili swala ni sensitive, ukweli TFF, au kiongozi aliye handle kaishusha heshima ya Taifa letu, anatakiwa ajiuzulu.

Mh.Malinzi hili suala la klabu ya Yanga tunaomba Ufafanuzi wa kina tafadhali Ili turidhike....

Je CECAFA Inaweza ikaiadhibu Yanga moja moja bila TFF Kuhusishwa? Je Yanga ilipeleka Majina ya mchangani?

Mwisho,walivunja kanuni ipi ya mashindano/CECAFA? Natumaini milipewa sababu/taarifa kama chama cha soka juu ya adhabu ya Yanga...
 
Mheshimiwa Rais
Nina swali moja kwako

Naipenda sana nchi yangu, naipenda sana Timu ya Taifa langu, Naupenda mpira wa Tanzania

Tokea umeingia madarakan mambo yamekua mabaya zaid kwenye timu ya taifa, Sikumbuki kama Taifa Stars imewahi kushinda tokea uwe madaraka

Je Tatizo n nini?

Danpol on the contrary kocha maart nooij tangia tumeanza mkataba naye kafungwa mechi mbili tu,ya tar 03/aug vs msumbiji maputo na ya botswana,amedraw mara tatu vs malawi,mozambique na zimbabwe na kuifunga zimbabwe,FIFA rankings aliikuta Tanzania ni ya 133 leo ni ya 110.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom