Maswali na ushauri kwa Malinzi

Maswali na ushauri kwa Malinzi

faiza do you know how much i am worth mpaka ufikirie kukagua mali zangu?
Nikusaidie Faiza,Federation nyingi Africa zinaendeshwa kwa nguvu na uwezo wa viongozi wa hivyo vyama,Look at Zimbabwe FA Mozambique FA etc FA presidents wao ndil wanahangaikia timu hasa za vijana.Kwa nini hujiulilizi majuzi bila udhamini wa uhakika tuliwezaje kuingiza kwenye mashindano ya Africa timu mbili za wanawake under 20 na senior,tukaingiza wavulana under 17 na under 20?Na zote zilikaa kambini zikala zikalala zikapanda ndege kwenda lusaka,lagis,nairobi na jburg.Taifa stars imekaa kambini since march hadi august inakula,inalala,posho,kambi botswana na timu haidai posho,Faiza bado una fikra potovu kuwa Malinzi mwizi? FIFA's motto ni "fair play".

mambo mengine mkuu naomba uwe unapuuzia tu kwani naona kama hayajengi, lugha zinazotumika sio za staha, mi binafsi nathamini uwepo wako hapa kwani kuna vitu vingi unavitolea ufafanuzi na bila wewe ukute tungekuwa tunajiuliza bila kujua wapi tutapata majibu, keep it up ndugu
 
maji yamekwisha mwagika,tugange yajayo

Hon. Eng. President Jamal Malinzi kama unakubaliana na makosa yaliyofanyika pale TFF, nawe ukiwa kiongozi mkuu wa chama hicho, basi tafadhali omba radhi kwa Yanga na Watanzania kwa ujumla. Kama Yanga wali-nominate wachezaji wasiotambuliwa na TFF weka mambo hadharani ili sisi tuwakomalie viongozi waombe radhi.
 
Kipaji Halisi hili la Yanga na cecafa siai kama federation we tried our best kuokoa situation na hili Yanga wanajua,walichoamua cecafa ndo hicho.

Kwann yanga na si cofee ya Ethiopia.?..mbn wameleta adamma city timu ya daraja la pili?..kubali kataaa musonye yuko juu yenu..cofee wamekataa kuja..st George's nao pia mbn hkn kelele wala majibu ya dharau..km aliyoyatoa musonye.. musonye...?......nitarudi
 
Last edited by a moderator:
komeka we acha tu,ahsante kwa kulitambua hilo.Ifikie wakati vilabu (hasa hivyo vinavyoitwa vikubwa) vitambue kuwa in thw long term kutafuta ubingwa wa papo kwa papo kwa kutumia wachezaji wa nje hakuwasaidia,kuwekeza kwa vijana ndio nguzo ya mpira wa nchi yoyote duniani.

Yanga alianza kutoa mfano kwa kupeleka timu ya vijana mbn hakuisapoti?...mkuu musonye mwenyewe anakiri kuchemka ktk hili..APR..ATLETICO..wameleta vijana mbn hamsemi?..hahahaha....
 
Last edited by a moderator:
Mkuu..naomba nikae kimya maana nina mabomu ya cecafa..nikiyatoa hapa..mtanitafuta bure..ukweli cecafa wapigaji tu..mshukuru mungu president kagame...mwisho unaenda lini Kigali..maana kule hayupo tenga wala wewe..naambiwa yuko kayuni tu..hahaha
 
uanachama wetu cecafa ni wa kisiasa na kihistoria kuanzia enzi za Gossage tukipigania uhuru.Mwaka huu tuliwaomba cosafa watualike nafasi ikawa ngumu (wamealika Ghana ).Hata hivyo usidhanie kote ni shwari,changamoto za uongozi ziko kila mahali,ni kukabiliana nazo tu.

Kisiasa, kiuchumi na kihistoria tuko vizuri zaidi na nchi wanachama wa COSAFA kuliko CECAFA. Naamini unazikumbuka nchi 5 zilizokuwa mstari wa mbele katika harakati za ukombozi kusini mwa Africa. Naamini pia unakumbuka uwepo wa miundo mbinu kama TAZARA, TAZAMA, Malawi Cargo, UMOJA bridge etc. Mwisho naamini pia unakumbuka vyama kama TAMOFA. Sasa kwa kuwa CECAFA wanaingiza siasa katika mpira na sisi tunataka kukuza mpira wetu tuwaambie finito! Usishangae huenda kuna mkono wa Kagame kuenguliwa kwa Yanga eti kwa vile JK ni shabiki wa Yanga na kwamba JK na Kagame haziivi! Ha ha haaa!

Twende COSAFA kwa ndugu zetu wa ukweli ambao hawana longolongo kama za Musonye.
 
COSAFA ndio kunakutufaa zaidi,lkn hawa wachumia tumbo hawakutaki sbb ya maslahi yao ndani ya cecafa
 
ahsante nguvu ,it all comes with the territory.Baadhi ya watu hapa jf wanashindwa kukubali kuwa najitahidi kutoa maelezo ndani ya mipaka ya kimaadili ya uongozi,yako ambayo kamwe siwezi kuya disclose hapa.La Yanga goes even beyond uwezo wa cecafa yenyewe,naishia hapo.
cc Malafyale

Kama issue ya Yanga iko beyond ya cecafa na ninyi kwa nini msijitoe? Kwa nini msiwaambie Yanga ndo wajitoe kwa sababu zao watakazosema badala ya kuwatungia sababu za ki.pu.uuzi? NIA YENU NI KUWAFARAKANISHA VIONGOZI WA YANGA NA WANACHAMA WAO SIYO? Kwa nini Musonye atoe lugha chafu kwa Yanga na wana Yanga kama unafikiri si kwa watanzania? Kwa nini Wambura naye aliongelee kwa kusema Yanga wamekiuka kanuni? kwa nini mtumie uongo kuondoa timu???? kwa nini? kwa nini? Unafikiri unajenga kwako au unabomoa? Wewe Malinzi utakuwa kiongozi gani kama utakuwa unatumika kudidimiza kwako kwa ajili ya maslahi ya nchi zingine? why, why,why?????????Hatujengi kwa kuongea sana Malinzi, tunajenga kwa vitendo!
 
Watanzania watu wa ajabu sana, kwa hiyo leo mnataka kusema matatizo ya soka la bongo yanasababishwa na musonye au kuwa cecafa?

wewe unaonaje kwan kama mna programe zenu halafu mtu mwingne anakupangia kuanzia kocha mpk wachezaji kuna nini hapo. Jamal Malinzi wewe kama raisi hili linahitaji ufafanuzi wa kwa wananchi na wadau maana rumours zpo nyingi kuhusu suala hili la yanga kuna hyo ya kupiga hela toka AZAM pia kuna hyo ya beef kati ya musonye na YANGA pia kuna hilo la ushabiki wa JK kwa YANGA ndo umeponza. huwezi ukasema maji yameshamwagika halafu basi je na mie nikichoma moto uwanja wa karume kisha nikasema yaishe maji yameshamwagika nitaeleweka. Jamal Malinzi hebu tunza heshima yako katika hili kwa kulitolea ufafanuzi hata kama sio humu basi katika media nyingne. nakuamini bado unaweza ila hili la yanga cjakuelewa hata kidogo
 
Nawashukuru sana wakuu mnapotoa mawazo kama haya. Majibu ya Jamal Malinzi ni 'questionable' hayaingii akilini mwa mtu yeyote mwenye akili timamu, eti 'maji yamemwagika ..., mara issue ya Yanga iko beyond uwezo wa CECAFA yenyewe...', ipo haja ya kuitaka TFF itoe maelezo ya kutosha. Nahisi Azam wamekata pochi kwa TFF na kama hali hii ikiendelea tunakwenda siko. Endapo Jamal Malinzi ataendelea na majibu ya namna hii, uangaliwe utaratibu wa kumpigia 'Vote of no confidence' aachie ngazi; hili liko mkononi mwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF waliomchagua.
 
Katika hilo la rushwa tuko pamoja ndugu ya blueband,tetesi za azam kwenda kagame hv,plan A kuna bloger mmoja aliripoti kuwa azam amepewa nafasi ya km mualikwa ktk yale mashindano,hiyo ikaonekana ni kuvunja kanuni ya cecafa kwani nchi mwenyeji ndio inaruhusiwa kuwa na timu mbili,plan B barua ya mualiko ilikaliwa pale tff mpaka Yanga waliposema hawajapata barua plan C ikakubali dhamira ya wapigaji,ndio maana hapa tunaambiwa maji yashamwagika,kwa mfumo huu na kwa watu km hawa bado sana kwa sisi kupiga hatua ktk soka

Tatizo ni fedha za Azam. Mimi nashauri hii issue ifanyiwe uchunguzi wa kina, ikithibitika kuna rushwa imetumika basi wahalifu wafikishwe katika vyombo va sheria.
 
Haya mambo ya cecafa tungeachana nayo coz ni upuuzi tu ... Makoyematale naona umekomalia cecafa utadhani ni mashindano ya klabu bingwa africa wakati ni upuuzi Wa musonye na wenzake isiitoshe cecafa haina mchango wowote kwny soka letu
 
Last edited by a moderator:
Mh jamali Malinzi.
Umefanya jambo la maana sana kuanzisha uzi huu maswali
1.Siku zote huwa tunasema ili soka letu liendelee lazima tuwekeze katika soka la vijana,na pia vijana tuwape nafasi ya kucheza,sasa yanga waliwapandisha vijana 6 na kuwajumuisha katika kikosi cha kwenda kagame cup,lakini cecafa wamewatoa,sasa mbona sijasikia tff wakiwatetea yanga ilhali tff ndio walenzi wa yanga na ilikuwa kwa faida ya soka letu?
2.Musonye anaonekana kuifanya cecafa mali yake binafsi kwa kauli za chuki dhidi ya yanga na zaidi kutoa vitisho,yanga awakwenda sudan kwa ushauri wa serikali,vipi tff baba mlezi wa vilabu bubu?je na nyie mnaufyata kwa cecafa inayodidimiza soka la huu ukanda wa africa mashariki?
3.Ipi mipango yako ya kuendeleza soka la vijana? na hasa vijana kupewa nafasi zaidi ya kuonyesha viwango vyao kwenye mashindano yenye ushindani?vilabu kuwatumia kwenye ligi kuu?Inawezekana wc urussi tumechelewa lakini qatar?
 
Haya mambo ya cecafa tungeachana nayo coz ni upuuzi tu ... Makoyematale naona umekomalia cecafa utadhani ni mashindano ya klabu bingwa africa wakati ni upuuzi Wa musonye na wenzake isiitoshe cecafa haina mchango wowote kwny soka letu

Mkuu kama umesoma vizuri posts zangu; nalalamikia hawa TFF kutumiwa na huyu Mkenya asiyetahiriwa aitwaye Musonye, TFF wametudhalilisha sana Watanzania tumeonekana hatuna akili hata kama za ng'ombe. Azam walitakuwa kukataa ofa ya dhuluma waliyopewa kwa mizengwe, nao kwa uroho wao wakakubali huku wakijua kilichofanyika ni fitina tupu. TFF ya mambumbumbu nayo ikaingia kichwa kichwa hadi lisemaji lao likaanza kuishutumu Yanga. Kama Tanzania inaongozwa na watu wa namna hii, mtu hahitaji kufikiria ni kwa nini hii nchi ni maskini huku ikiwa na maliasili lukuki.

Naenda half time, nitarudi.
 
Last edited by a moderator:
Shida ni tff kihamisha ofisi kwenda kupanga kwa mamilioni ya pesa huku wafanyakazi kwakilipwa tarehe 50 yale majengo ya karume yamebaki makumbusho yakisubiri mradi hewa
 
Malinzi

Katika muda mfupi tu wa uongozi wako unakabiriwa na tuhuma nyingi nzito. ili kusafisha jina na heshima yako, unaonaje iundwe tume ambayo ni independent na ina watu wenye heshima kama waakili Said El Maamry, ili kuchunguza na kuweka bayana hizi tuhuma hapa chini

1) Saga la Azam lilivyogubikwa na mwendo wa rushwa, ili ishiriki kombe la kagame kwa mlango wa nyuma. kwani hapa zimeshushwa detail nyingi.
2) Tuhuma za wewe kuweka watu hotelini, na kuwalipia wakati wa uchaguzic.c @FF
3) Kuhamisha offisi kinyemela na kuiweka taasisi ya TFF katika wakati mgumu ki pesa
4) Mradi wa maduka (frame)
5) Kushiriki kumtorosha kinyemela Ngassa kwenda kufanya majaribio Afrika ya Kusini, bila kuwashirikisha Yanga. Habari hizi zilikaliliwa na blog moja , mwenye blog aliandika kuwa mlikutana uwanja wa oliver Tambo, ukawa unalalamika kuwa umefanya kazi kumleta sasa Yanga wanafanya nini? Hili swala halitakiwi kufanywa na mtu kama wewe, inawezekan, huyu mwandishi anataka kukumaliza, au wewe mwenyewe hujajua miiko ya kuongea na wandishi wa habari

Nia si kukutafuta ubaya, bali ili kusafisha jina lako na heshima yako, na taasisi kwa ujumla.
 
Hongera Mkuu, umemshauri kiutu uzima sana. Uamuzi ni wake.
 
Wadau nimeiona hii kwenye Facebook page ya mwanaspoti
FIFA imeitaka TFF kuanza mchakato wa kuhamisha ofisi katikati ya Jiji na kurudi Ilipokuwa awali na ndani ya masaa 24 mchakato huo uwe umeanza
 
Back
Top Bottom