Maswali ya kijinga na majibu ya hasira. Ongeza na ya kwako

Maswali ya kijinga na majibu ya hasira. Ongeza na ya kwako

Mmepewa assignment ya group,siku ya Presentation umesogea mbele ili uliwakilishe group Lecturer anauliza Umekuja kupresent?....Hapana nimekuja kucheza mziki wa Awilo


Hapo hapo nakuahidi kukushika...
 
Mtu hajakuona cku nyingi anajikuta anakuuliza ni wewe kweli au nakufananisha unamjibu kistaarabu tu hapana ni Izraeli mtoa roho
 
Umebeba ndoo ya maj unaelekea bafuni alf unataulo m2 anakuulza, unaenda kuag?......hapana naenda kuosha vyombo
 
Hahahaaaaaa! Dahhh nimecheka hadi machozi.
 
-unampigia Mtu Simu Hajapokea, Anakuta Missed Call, Anaamua Kukupigia Anakuuliza Ulikuwa Unanipigia, Unamjibu 'hapana Nilikuwa Nakagua Simu Zilizoko Silent'

-unamkuta Mke Wako Yuko Na Mshikaji, Wako Ziro Distance Unamuuliza Mke Wangu Unanisaliti, Anakujibu 'hapana Nimekuja Kudai Madeni

-mnakutana Na Mchungaji Kwa Mganga Na Unaona Anapewa Hirizi Unamuuliza Mchungaji Na We Unakujaga Huku, Anakujibu 'hapana Nilikuwa Nimekuja Kuombea Wagonjwa'

-unamwona Binti Mlokole Kapewa Mimba Unamuliza Na Wewe Una Mimba Anakujibu 'hapana Mi Bado Bikra'.

-kuna Msiba Umetokea Watu Wako Hapo Msibani, Anafka Jamaa Anauliza Hivi Hapa Kuna Msiba, Jamaa Anajibiwa 'hapana Tuko Kwenye Send off'.
 
Saa nane ucku mtu anakupigia cm unapokea anakuuliza umelala?.......hapana naongea na cm
 
Jamaa aliniagiza leo nipeleke pesa mahali. Nimerudi ananiuliza vipi usharudi ??? Nikakumbuka huu uzi nikamjibu hapana bado sijarudi. Niliwaza nitafute jibu lingine zuri zaidi ya hili nikakosa
 
Back
Top Bottom