Mkuu
Proved , asante sana kuni tag, nimetia timu.
Mkuu
ASIWAJU , maswali yako ni ya msingi sana, Watanzania bado wanahitaji sana kufundishwa somo la uraia, nadhani ni JF pekee ndio inatoa elimu hii, karibu
Hatua ya kwanza ni kuelimisha kuhusu Pre colonial Tanganyika na na Pre colonial Zanzibar. Tanganyika na Zanzibar, ziligawanywa kwa wakoloni wakati wa ule mkutano wa mabeberu wa 1884-5 kwenye the scramble for Africa ulioitishwa na Mtawala wa Ujerumani Von Bismarck, kwenye jiji la Berlin, ambapo Tanganyika ilitwaliwa na Ujerumani na kuwa a German East Africa. Zanzibar haukutawaliwa bali eneo lote na visiwa vyote vya Indian Ocean plus a 10 miles of coastal tripe kutoka Sofala hadi Lamu ilikuwa chini ya Sultan of Zanzibar ila Uingereza itawalinda.
Kenya iligaiwa kwa Waingereza na Uganda iliachwa chini ya Baganda Kingdom chini ya Kabaka.
Hivyo Tanganyika na Kenya zote zilikuwa ni land locked countries kwasababu pwani yote ilikuwa chini Sultan of Zanzibar.
Hivyo ili Tanganyika na Kenya wapate access to sea, Waingereza na Wajerumani wakaingia mkataba wa Hellingoland au The Zanzibar Treaty 1890 ambapo Wajerumani waliwapa Waingereza mji wa Hellingoland na kisiwa cha Witu ambazo zilikuwa chini ya Ujerumani, and in return, Sultan of Zanzibar aliachia ile 10 mile Coastal strip hivyo Tanganyika na Kenya ndipo zikapata access to Indian Ocean, na ni mkataba huu ndio ulioifanya Zanzibar kuwa a protectorate of the British Empire na ndio uliathiri mipaka ya Ziwa Nyasa na Ziwa Tanganyika, badala ya mpaka kupita katikati, Ziwa Nyasa lote liliwekwa chini ya Malawi lakini Tanganyika wanaruhusiwa kuvua tuu samaki na Ziwa Tanganyika lote ni la Tanganyika, Congo wanaruhusiwa kuvua samaki. Hiki ndicho chanzo cha mgogoro wa Ziwa Nyasa ambao bado haujawa resolved hadi leo!.
https://www.jamiiforums.com/threads...tukufu-alikuwa-ni-puppet-wa-wakoloni.1181508/
Baada ya Mjerumani kushindwa Vita Kuu ya Kwanza, ya Dunia, WWI (1914-1918), Wajerumani walinyang'anywa makoloni yake yote na sisi Tanganyika tukakabidhiwa kwa Muingereza as a Trusted Colony, wakati jirani zetu Kenya wao ndio waliendelea kuwa a British Colony, Uganda ilikuwa ni British Protectorate.
Hivyo Tanganyika ilikuwa chini ya Uingereza na League of Nations ilipoanzishwa ile 1945, Tanganyika ilikabidhiwa kwa Uingereza as a mandated territory kuiandaa kujitawala, hivyo it was right for Tanganyika to seek freedom from the British.
Sababu ni moja tuu ya msingi ni kujitawala na kuwa nchi huru.
Zanzibar licha ya kupata uhuru wake December 10, 1963, ilikuwa ni monarch chini Sultan of Zanzibar kama ilivyo Uingereza. Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya January 12, 1964 yaliyomtimua Sultan of Zanzibar, yalipelekea Uingereza kutuma manowari ya kivita na majeshi ya Uingereza kuja kuikomboa Zanzibar chini ya waasi na kumrejesha Sultan of Zanzibar madarakani.
Karume akaja Tanganyika kuomba ulinzi wa Tanganyika kuyalinda Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Nyerere akapima tukipeleka majeshi Zanzibar kuilinda Zanzibar, Waingereza wakileta majeshi kuikomboa Zanzibar jee tutaweza?. Taarifa za majeshi kuandaliwa kwenda kuilinda Zanzibar tayari kwa Mapambano kupigana na jeshi la Uingereza ziliwashitua sana Wanajeshi hivyo siku 6 baada ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, tarehe 18 January 1964 wanajeshi wa kambi ya Calitto (Lugalo) wakaasi na kufanya Mapinduzi kumpindua Nyerere, kesho yake 19 January 1964 jeshi la Kenya nao wakaasi kumpindua Kenyatta, tarehe 20 January 1964 jeshi la Uganda nalo likaasi kumpindua Militon Obote. Ni Oscar Kambona aliyemtorosha Nyerere kwa mtumbwi kumficha Kigamboni akawatuliza waasi na kumrejesha Nyerere.
Wakati yote haya yakiendelea ndipo Nyerere akamshauri Karume, ili kuilinda Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar dhidi ya ukombozi wa Waingereza, kwanini tusiungane na kuwa nchi moja, hivyo Uingereza hautaweza tena kuivamia Zanzibar. Karume alikubali pale pale!, "we rais, mimi makamu". Hivyo sababu kuu ya muungano wetu kwa uharaka ule ni tuliungana fasta for security reasons kuyalinda Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar!.
Realty ya visiwa vya Zanzibar, ni sehemu ya Tanganyika ikamegeka miaka milioni nyingi kabla, Waarabu wa Zanzibar na Sultan wao ni wavamizi tuu, wenyeji halisi wa Zanzibar ni Wahadimu chini ya utawala wa Mwinyimkuu ambao asili yao ni huku bara, ila wahamia wengi wakaingia wakiwemo Wangazija, Wahindi na Waarabu na ndipo mwaka 1732 Sultan Seyyid Said akaivamia Zanzibar na kuhamishia the sultanate yake kutoka Oman na kuja Zanzibar na kujitwalia tuu kama ameiokota, as if ilikuwa haina wenyewe!, kumbe no!, wenyewe walikuwepo wamejinyamazia tuu kimya!, hadi ile January 12, 1964 walipoamua liwalo na liwe, wakaikomboa Zanzibar yao.
Nimeisha kutajia ni ulinzi. Muungano ni kama ndoa, kuna mmoja alikwenda kujibebisha kwa mwingine ili apate ulinzi, wakaoana na kuwa kitu kimoja.
Baada ya muungano mipaka yote ilibadilika, muungano wetu ni wa union, nchi mbili kuungana kuunda nchi moja ya JMT. Mipaka ya JMT ni eneo lote la iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Hakuna tena mpaka wa Jamhuri ya Tanganyika kwasababu Jamhuri ya Tanganyika ilikufa na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar pia ikafa, mipaka ni ya JMT.
Ni eneo lote la iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar
Baada ya muungano Jamhuri ya Tanganyika ilikufa, hivyo hakuna tena katiba ya Jamhuri ya Tanganyika. Ila baada ya muungano, tulikuwa na katiba ya mpito toka ile 1965 hadi 1977 tulipopata katiba ya JMT ya 1977 ndio katiba ya nchi.
Katiba ya Zanzibar ni katiba ya mwaka 1984.
SMZ inapata mgao wa asilimia 4.5% ya mapato yote ya mikopo na fedha za grants JMT inazopata kutoka nje.
Hakuna serikali ya Jamhuri ya Tanganyika, kuna serikali ya JMT na SMZ, serikali ya JMT hahitaji chochote kutoka SMZ kwasababu SMZ iko chini ya JMT.
Muungano wetu ni muungano wa kikemikali kuunda a compound mpya ya JMT ambayo haiwezi kuvunjwa milele!. Hakuna taratibu zozote za kuuvunja muungano wetu adhimu. Muungano tutaulinda kwa gharama yoyote!.
Ila kwa vile Zanzibar haikuridhia muungano
https://www.jamiiforums.com/threads...r-haikuridhia-muungano-ina-maana-gani.276286/ lakini imetekeleza muungano, kama binti akibakwa, na asilalamike, baada ya kujikuta amebeba ujauzito wa yule mbakaja akaamua kwenda kuishi naye, atahesabika ameridhia!. Hivyo japo Zanzibar haikuridhia muungano kwa ratification lakini imetekeleza muungano kwa matendo, huko kunahesabika ni kuridhia!.
Hivyo kama ni kweli Wazanzibar hawautaki muungano nimewashauri kitu cha kufanya
https://www.jamiiforums.com/threads...ama-pigeni-kura-ya-maoni-muamue-moja.1071288/
Asante tumekaribia, we Asiwaji, una kipaji cha uandishi wa habari, wa habari za uchunguzi, una kipaji cha kuhoji, una kipaji cha uchunguzi, upepelezi, uhojaji na ufuatiliaji. Waalimu wako wa darasa walipaswa wakuripoti kwa Mwalimu Mkuu ili uwe spotted tangu shuleni, ili uwe groomed na kuingizwa kwa wale 'jamaa zetu' wa kule ulifaa sana!.
P