Maswali yangu kuhusu Mkataba DP World

Maswali yangu kuhusu Mkataba DP World

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Mimi binafsi napenda sana uwekezaji na hasa uwekezaji uliofuata utaratibu wa kisheria. Naomba kuuliza maswali yafuatayo kuhusu mkataba wa DP World;

(1) Kama tuna sheria ya manunuzi inayotuongoza nchi nzima ni kwa nini mkataba huu haukutangazwa na kuwepo na ushindani?

(2) Jana Mhe. Waziri aliitangazia umma kuwa kuna mashirika 10 yanayojishughulisha na kusafirisha mizigo baharini ikiwemo DP World kwanini hamkuwashindanisha ili mpate Kampuni yenye uwezo?

(3) Mkataba huu unataka wananchi watoe maoni yao. Je, ni kwa nini maoni yalitolewa kwa masaa machache hata bila kutoa muda wa kutosha?

(4) Kwanini saini upande wa DP World hauna jina na cheo cha mhusika?
 
Asilimia kubwa ya wanaopinga mkataba (IGA) Hawapingi mkataba (IGA) wa bandari, kwakua ili kupinga mkataba, ni lazima uanze na sheria zitakazo ongoza mkataba kwanza, kabla ya yaliyomo, kwakua yaliyomo ni lazima yafuate sheria. Hii ni kama tu unataka kupinga kwa nia njema ya taifa. Usipofanya hivyo nisawa na kuchukua maneno, na mistari miwili kwenye vitabu vitakatifu ili iendane na haja zako. Waingereza wanaita hali kama hiyo “ulterior motives”

Kuna msukumo mkubwa kwa wanaopinga lengo Lao kuu ni wanapinga Jamhuri ya Muungano ya Tanzania 🇹🇿 kuwa HURU kimapato kwa mara ya kwanza. Usione ajabu, Kaskazini wanakua na mtazamo tofauti wa mambo na sio dhambi. Hata Mangi Mkuu Mangi Marialle alipingana na Mwl kuhusu Tz kupata uhuru 09 Dec 1961, aliona muda haijafika kwanza, hatuna uwezo wa kujiongoza Bado.

Lakini Uhuru uliletwa na TANU, ambayo leo inaitwa CCM, baada ya kuugana na Afro Shirazi (ambacho likua na wapini Znz) 1977, na Kila mtu amefaidika kutokana na hilo.

unaweza kuiangalia South Africa 🇿🇦 Kijuju ukadhania bora tungechelewa kidogo kupata uhuru kama ulivyokua mtazamo wa Mangi Mkuu Mangi Marialle, japo alikua hapatani na mmoja wa mangi wadogo, mangi Shangali.
Laking Uhuru ni sasa, alisisitiza Mwl, na njia aliyofanikisha kutupitisha ndio tunaendelea nayo Leo.

Hili Jambo ni kubwa kiasi kwamba haliwezi kuwa na mkataba (IGA) mmoja wenye kurasa 38 tu, lazima iwepo mengine, pia ya kupenda na na makubaliano kati ya Tanzania 🇹🇿 na Dubai. Kuku, mbuzi, nguruwe, ngombe, ni nyama, kama vile IGA, HGA, na PA(s) yote ni mikataba, lakini nyama zote ziko Sawa? Mikataba yote iko Sawa?
Watu wanajua tofauti Za nyama, ila kutokana na shughuli zao Za Kila siku sio wote wanajua tofauti ya tofauti ya IGA, HGA, na PA(s).
Kutokua kwao usikutumie kwa faida yako kama wewe ni kiongozi wa kweli.

ukiiangalia kipengele cha 21, kipengele pekee pekee kinachoelezea sheria zitakazo ongoza mkataba, kwakua yaliyomo yote lazima yaendane na sheria.

Kimsingi tafsiri ya mkataba ni makubaliano yanayoweza kulazimishwa na sheria.

Sheria gani sasa zinaweza kulazimisha hayo makubaliano?

Jibu liko kipengele cha 21, kwamba IGA itafuata sheria Za uingereza ambazo tunazifuata tayari, zinafanana na Sheria zetu, kwakua tumezirithi kutoka serikali iliyokuwepo kabla ya 09 Dec 1961. Kipengele cha 21 pia kinasema HGA na makubaliano ya mradi yatafuata sheria Za Jamhuri ya muungano ya Tanzania. Na sheria Za Tanzania tunaweza kuzibadilisha tunavyotaka bila na mkataba (IGA) inatambua hilo, na kukiri hilo. Hii inakua muhimu kwenye mapato. Ndio maana mapato hayamo kwenye IGA, yatakuwepo kwenye HGA ili yafuate sheria Za Tanzania, na hapo ndipo Prof Mbarawa, wanalinda maslahi, ya wa Tanzania, kwamba mapato yangekuwepo kwenye IGA, tusingekua na control nayo. Badala ya kufurahia hilo wanaliruka, hakuna anayepinga anaweza kukataa ukweli huu.
 
Majibu yako ni mepesi.
1. Sehemu kubwa ya Mkataba huu si ushindani ,bali ni kama Msaada wa kirafiki wa kiuchumi kwa Taifa letu toka kwa Rafiki yetu Mfalme wa Dubai.

2. Uwezo wake DP World ulifanyiwa utafiti na tukaona ni wenye tija kwa Tanzania zaidi,na kwa hiyo hatukuhitaji mchakato na mlolongo mrefu.

3. Tunatakiwa tutowe maoni kwa sababu mkataba huu ni wa kiudugu kabisa. Kama vile Mchina alipotujengea Reli ya Tazara , Mkataba wake haukujadiliwa kwa vile ulikuwa ni Msaada wa kidugu.(Wachina walichukua kila kitu walichokiona porini ikiwemo mchanga wa Almasi na Rubi, na Magogo .

4. Kuna mambo mengine hata ukiyajua hayana msaada wowote . Ukwel ni kuwa kuna baadhi ya mambo wamekubaliana yawe siri za kibiashara. lakini Watanzania wanalazimisha ziwekwe Hadharani.
Mbona Barick hawakuonesha Mikataba yao kwa Magufuli? wala Kwa Kikwete, Mbona, Wachiba Madini Kule Bulya mkulu mikataba yao Imekuwa Siri hadi leo?
Huu ni Utamaduni ya Mikataba ya Kibiashara kuwepo na Secret .

Kama Kuna swali jngine kubwa ni kuwa Tanzania Itaongeza Pato lake la Bandarai kwa 3 times
kutoka Tril. 7 hadi Tril. 24.
Hili ndilo linatuhusu zaidi kama taifa.
Ajira kwa watu wetu zitaongezeka . na ufanisi wa Bandari yetu utakuwa.
 
Sheria ya manunuzi ya Tanzania ni Puplic Procurement Act ndani ya sheria hiyo soma section 4 itakuelewesha vizuri sana kuna mazingira maalumu yanaweza kuipelekea serikali kufanya manunuzi bila kutangaza tenda wala ushindani wowote maswali mengine ni political siwez kuyajibu kwani kuna mikataba mingi sana imesainiwa bila discussions na wananchi na wala wananchi hatujui hiyo mikataba huu umevuja on purpose.
 
Asilimia kubwa ya wanaopinga mkataba (IGA) Hawapingi mkataba (IGA) wa bandari, kwakua ili kupinga mkataba, ni lazima uanze na sheria zitakazo ongoza mkataba kwanza, kabla ya yaliyomo, kwakua yaliyomo ni lazima yafuate sheria. Hii ni kama tu unataka kupinga kwa nia njema ya taifa. Usipofanya hivyo nisawa na kuchukua maneno, na mistari miwili kwenye vitabu vitakatifu ili iendane na haja zako. Waingereza wanaita hali kama hiyo “ulterior motives”

Kuna msukumo mkubwa kwa wanaopinga lengo Lao kuu ni wanapinga Jamhuri ya Muungano ya Tanzania 🇹🇿 kuwa HURU kimapato kwa mara ya kwanza. Usione ajabu, Kaskazini wanakua na mtazamo tofauti wa mambo na sio dhambi. Hata Mangi Mkuu Mangi Marialle alipingana na Mwl kuhusu Tz kupata uhuru 09 Dec 1961, aliona muda haijafika kwanza, hatuna uwezo wa kujiongoza Bado.

Lakini Uhuru uliletwa na TANU, ambayo leo inaitwa CCM, baada ya kuugana na Afro Shirazi (ambacho likua na wapini Znz) 1977, na Kila mtu amefaidika kutokana na hilo.

unaweza kuiangalia South Africa 🇿🇦 Kijuju ukadhania bora tungechelewa kidogo kupata uhuru kama ulivyokua mtazamo wa Mangi Mkuu Mangi Marialle, japo alikua hapatani na mmoja wa mangi wadogo, mangi Shangali.
Laking Uhuru ni sasa, alisisitiza Mwl, na njia aliyofanikisha kutupitisha ndio tunaendelea nayo Leo.

Hili Jambo ni kubwa kiasi kwamba haliwezi kuwa na mkataba (IGA) mmoja wenye kurasa 38 tu, lazima iwepo mengine, pia ya kupenda na na makubaliano kati ya Tanzania 🇹🇿 na Dubai. Kuku, mbuzi, nguruwe, ngombe, ni nyama, kama vile IGA, HGA, na PA(s) yote ni mikataba, lakini nyama zote ziko Sawa? Mikataba yote iko Sawa?
Watu wanajua tofauti Za nyama, ila kutokana na shughuli zao Za Kila siku sio wote wanajua tofauti ya tofauti ya IGA, HGA, na PA(s).
Kutokua kwao usikutumie kwa faida yako kama wewe ni kiongozi wa kweli.

ukiiangalia kipengele cha 21, kipengele pekee pekee kinachoelezea sheria zitakazo ongoza mkataba, kwakua yaliyomo yote lazima yaendane na sheria.

Kimsingi tafsiri ya mkataba ni makubaliano yanayoweza kulazimishwa na sheria.

Sheria gani sasa zinaweza kulazimisha hayo makubaliano?

Jibu liko kipengele cha 21, kwamba IGA itafuata sheria Za uingereza ambazo tunazifuata tayari, zinafanana na Sheria zetu, kwakua tumezirithi kutoka serikali iliyokuwepo kabla ya 09 Dec 1961. Kipengele cha 21 pia kinasema HGA na makubaliano ya mradi yatafuata sheria Za Jamhuri ya muungano ya Tanzania. Na sheria Za Tanzania tunaweza kuzibadilisha tunavyotaka bila na mkataba (IGA) inatambua hilo, na kukiri hilo. Hii inakua muhimu kwenye mapato. Ndio maana mapato hayamo kwenye IGA, yatakuwepo kwenye HGA ili yafuate sheria Za Tanzania, na hapo ndipo Prof Mbarawa, wanalinda maslahi, ya wa Tanzania, kwamba mapato yangekuwepo kwenye IGA, tusingekua na control nayo. Badala ya kufurahia hilo wanaliruka, hakuna anayepinga anaweza kukataa ukweli huu.
Mbona huzungumzii kifungu kinachokataa mkataba kuvunjika kwa namna yoyote ile hata kama kutakuwepo na ukiukwaji fulani! Ni punguani awezaye kujifunga na mkataba kama huo!
 
Mimi binafsi napenda sana uwekezaji na hasa uwekezaji uliofuata utaratibu wa kisheria. Naomba kuuliza maswali yafuatayo kuhusu mkataba wa DP World;

(1) Kama tuna sheria ya manunuzi inayotuongoza nchi nzima ni kwa nini mkataba huu haukutangazwa na kuwepo na ushindani?

(2) Jana Mhe. Waziri aliitangazia umma kuwa kuna mashirika 10 yanayojishughulisha na kusafirisha mizigo baharini ikiwemo DP World kwanini hamkuwashindanisha ili mpate Kampuni yenye uwezo?

(3) Mkataba huu unataka wananchi watoe maoni yao. Je, ni kwa nini maoni yalitolewa kwa masaa machache hata bila kutoa muda wa kutosha?

(4) Kwanini saini upande wa DP World hauna jina na cheo cha mhusika?
Mkuu mbona nilimsika Johar akisema hakuna mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya DP, akasema ni mkataba wa makubaliano kati ya Dubai na Tanzania ndiyo iliyopitishwa na Bunge, asema kwa sasa tusiitaje kabisa DP word kwakua haija ingiza mkataba na Tanzania wala TPA, kuitaja DP word kwasasa.
 
Katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaruhusu rais kuongoza mihula miwili (2) mfululizo ya urais kwa maana ya miaka 10.. ila ikiwapendeza wabunge wetu wanaweza wakafanya namna kurekebisha hicho kifungu ili kukidhi mahitaji yetu kwa sasa.. Mama Samia aongoze hadi 2040.
 
Huu mkataba umejaa jinai nyingi sana. Yawezekana walioweka saini wote including but not limited to SSH walijifunga kwenye mtandao wa kijinai dhidi ya sheria za Tanzania.
 
Back
Top Bottom