Nionavyo No reform no election ni uamuzi sahihi kabisa.
Huwezi shiriki uchaguzi ambao siyo wa haki. Ni uenda wazimu kushiriki jambo unalojua halikupi haki yako.
Hata wana CCM wanao jitambua wakienda kupiga kura huku wanajua mazingira sio sawa wanafanya hivyo kiuwenda wazimu. Wale wasioelewa au kuona dosari na ambao ni wengi, wana samehewa. Ipo siku wataelewa hata miaka 100 ijayo.
Binafsi sipendelei maandamano, naamini zipo njia nyingi za kuwasilisha ujumbe na ukawa na madhara.
Kujitolea kuumia au kufungwa kwa kuamini unawatendea vema mamilioni wasio jitambua nao unaweza kuwa uenda wazimu.
Napendekeza na kuunga mkono yafuatayo yafanyike.
1. Kufikia na kuongea na makundi mbalimbali katika jamii.
2. Kutumia vyombo vya habari kama ilivyo fanyika hivi kribuni.
3. Kuendesha midahalo swali la msingi ni ikiwa kuna uhalali wa mtu unayejitambua kushiriki uchaguzi kwa taratibu za sasa.
4. Kufungua pingamizi mahakamani bila kujali uimara au udhaifu wa mhimili huo.
Binafsi nina tabiri watu wengi hawata itikia wito wa No reform no election sababu wengi wana maono dhaifu, madogo sana kutokana na malezi kitaifa.
Itatuchukua miaka 50 au zaidi kuelewa haki zipi tunanyimwa.
Ingawa CCM wanajua hata mabadiliko yakikubaliwa bado watashinda lakini wanajua pia kuwa muda wa kuondolewa madarakani utazidi kuwa mfupi, wataendelea kufanya danadana yasifanyike mabadiliko yoyote ya maana.
No reform no elección ni sahihi lakini ifanyike kwa namna ambayo haitaumiza watanzania wenzetu.