Habari Zenu,
Mimi ni mkazi wa Dar es Salaam na ni mtumiaji wa barabara ya Bagamoyo Road. Kila siku napita kwenye barabara hii kwenda katika majukumu yangu ya kila siku, lakini aisee, mataa ya barabara hii, kuanzia njia panda ya Goba Masana hadi hapa Tanki Bovu na njia panda ya kwenda Kawe, hayafanyi kazi kwa muda sasa. Hali hii si salama kwa watumiaji wa barabara hii, kwani ajali zimekuwa nyingi kutokana na kila mtu kujaribu kuwahi.
Wahusika, tafadhali tunaomba marekebisho ya mataa sehemu hizi ili kuondoa kero hii na kuhakikisha usalama wa watumiaji wa barabara.