Mataifa 20 sasa yatia saini kuilinda bahari Nyekundu dhidi ya magaidi, Iran inazidi kutengwa

Mataifa 20 sasa yatia saini kuilinda bahari Nyekundu dhidi ya magaidi, Iran inazidi kutengwa

Kwanini wao wasimvamie ili kukomesha jeuri ya Urusi, kama walivyofanya Libya na Iraq? Kumbuka alichokifanya Urusi kuivamia Ukraine kinafanana na Kile Alichokifanya Saddam kuivamia Kuwait nwaka 1990.
Tambua tu kuwa Urusi na Marekani Ni mataifa makubwa na yenye nguvu kubwa za kijeshi duniani, hivyo yanaogopana na ndiyo maana hayataki kuji-involve in direct war, zaidi watabaki kupigana indirectly kupitia proxy wars.
Wamvamie kwa sababu gani, kumbuka hajagusa maslahi yao, ila anajaribu karudisha kanchi kaliko jitenga na pande zote yaani NATO na huyo mrusi......na kumbuka Ukraine ilikuwa Russia enzi za U.S.S.R.....
 
Kama hujui sababu ya US kuvamia Syria na vibaraka wake kaa pembeni nenda kajifunze geopolitics then rudi hapa.
Kumbe huu uzi unazungumzia sababu za U.S.A kuivamia Syria..?..... "mental disorder is real".....
 
Wamemshindwa Taleban watamuweza Houthi?
Kidume kakukalia kooni miaka 20 kuhakikisha kabisa hakuna hata sisimizi anayehema ardhini pako kilipoona maslahi hayalipi kikasepa afu wewe Mmang'ati uliyekaa hapo vijiweni Vingunguti Dar useme "USA aliishindwa Afghanistan" kumbe ni kweli kabisa akili ni nywele?
Screenshot_2023-12-21-02-28-55-19_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg
 
hawezi hana ubavu miaka yote anategemea muungano kama yeye kidume aende mwenyewe apeleke pmb eti pentagon anahaha hajui afanye nini akijichanganya tu akiingilia imekula kwao amekuwa mbayuwayu hatulii mavi debe
Hujiulizi bajeti za majeshi ya ulinzi wa USA kwanini ziwe kubwa sana kuliko nchi zote duniani?

Unadhani USA military bases zaidi ya 750 katika nchi 80 duniani zinajiendesha zenyewe tu kifedha?

Hujui moja ya faida za USA military bases ni nyakati kama hizi kuzitumia kwa nchi kama Yemeni?
 
Hapo HOUTHI anadeal na BAB EL MANDEB tu, nasio RED SEA yote. Sasa wao wapitishe waone, mbona walimzuia RUSIA kupitisha meli zake Kwa baadhi ya maeneo akatii, hicho nikikwazo ambacho YEMEN kawawekea Israel Kwa sharti kwamba Israel aruhusu misaada ya kibinadamu iingie Gaza, vinginevyo nae hakuna meli itakayoelekea Israeli itakayopita hapo. CHINA&RUSSIA mbona meli zao zimepita juzi na Jana. Israel aruhusu misaada yakibinadamu Gaza nae aruhusiwe meli zake zipite hapo, mbona MALYESIA kazuia meli zinazoelekea Israel kupita katika maji yake mbona hatusikii makelele?.
Yeye si hataki?

Zitapita kwa lazima sasa
 
Dawa ya Iran inachemka, akijichanganya tu ataingia ndani ya 18 za wenyewe - tutamsahau kama vile kina Sadam na Gadafi.
Toka mwaka 1979 mnaimba hizi ngonjera tushazichoka
Hakuna taifa lakuivamia iran maana hio israhell mlokua mnaitegemea imewaangusha sana
Mlijua itaibeba ghaza jumla jumla ndani ya dakika sita
Leo mwezi wa nne uleeeee[emoji1787][emoji3][emoji1787]
 
Siyo kwamba anashindwa kuilinda sema bahari ni mali ya binadamu yeyote na haimilikiwi na mtu taifa au kikundi cha watu, ndiyo maana anahitaji ushawishi..
Sasa mbona hawajaenda kule black sea kuilinda ili ukraine asafirishe ngano zake kwenda nje
Mpaka maskini ikabidi atumie mto Danube tena kusafirisha tani af mbili badala ya zile tani af thelathini
Hakuna hoja hapo
 
Kumbuka mrusi hajapigana na mataifa hayo uso kwa uso, sema wanampatia Ukraine silaha kama rafiki tu maana hakujiunga na umoja wao wa NATO hapo awali so, hawana sababu yeyote ya kumsaidia zaidi ya urafiki na ujirani.

Kama ukweli mrusi anajiona jeuri aachane na kupepesa avamie moja ya mwanachama wa NATO ndipo nitaona kweli jeuri...
Kwani kuwait ilikua mwanachama wa NATO kijana[emoji3][emoji1787][emoji3]
Mbona wakat anapelekewa moto na Iraq kina us na shost zake walipelekana kumsaidia
Huna hoja hapo
 
Sheria za kimataifa kuhusu ulinzi (self defense) ni kali sana, na ndiyo maana mataifa yanashindwa kuingia vita moja kwa moja. Jiulize kwa nini mataifa ya kiislam hadi sasa yanasita kuingia vitani kuishambulia Israel moja kwa moja - kwa nini Iran yupo kimya badala yake anatumia hao magaidi kufanya proxy war na si kwenda live.

Kwa mfano Ukraine ana haki na kulipigania taifa lake, unachoweza kufanya ni kumsaidia tu na si kuingia live vitani - utakwisha - Kama Marekani ataingia live basi Korea na Uchina nao wanaweza kufanya hivyo hence vita kuu ya 3 ya Dunia.

Mfano mwingine kwa nini IRAN asiingie live kusaidia HAMAS kuishambulia Israel? hawezi kabisa maana akifanya hivyo basi itakuwa balaa kwa ulimwengu wetu. Vivyo hivyo US hawezi kwenda peke yake kulinda Red Sea ingawa anaweza sababu ya hizo hizo sheria, sasa badala yake ana mobilize mataifa mengine ili wafanye ulinzi kwa pamoja.
Huna hoja
Kwanini israhell asiipige iran moja kwa moja kwamadai anayosema iran inapeleka wanamgambo Syria
Badala yake kila siku anaipiga tu Damascus wakati anajua kama wanamgambo wanaletwa kutokea iran na silaha zao
Pia mwaka 2006 kwanini alipigana na Hizbullah wakati anajua wanapewa silaha na iran kwanini asiwapige iran moja kwa moja
Kwanini us asinge mobilize mataifa mengine wakalinda black sea kule ili ukraine akapitisha ngano na bidhaa zake nyengine tena ikumbukwe ukraine aliomba kabisa wamagharibi wamsaidie ila wakapita kushoto
Jamaa huna hoja hata kuwait iliposhambuliwa na iraq marekani na shoga zake walienda kuisaidia moja kwamoja kuwait mbona hapo ukraine wanagoma huna hoja
Mwaka 1980s wakat wa vita ya iran na iraq marekani hao hao walikua wanampa silaha iraq ambae aliivamia iran tena walimpa mpaka silaha za sumu na bado iraq ndio alikua kavamia sio kama ukraine ambae kavamiwa na anaomba sana msaada huna hoja
Huna hoja hapo
 
Hawa magaidi wa kidini pamoja na mfadhili wao Iran wanazidi kuwekwa kwenye msalaba, mataifa 20 yote kulinda hilo bahari.

===================

More than 20 countries have joined the US-led coalition to protect Red Sea shipping from attacks by Yemen’s Houthi rebels, the Pentagon says.

The Iran-backed Houthis have repeatedly targeted vessels in the vital shipping lane with strikes they say are in support of Palestinians in Gaza, where Israel is battling terror group Hamas following its unprecedented attack on Israel on October 7.

“We’ve had over 20 nations now sign on to participate” in the coalition, Pentagon spokesman Major General Pat Ryder tells journalists.

Je wewe unalijua ? ....tupatie taarifa msemaji wa Syria kutoka namtumbo huko ndani ndani...

View: https://x.com/WarMonitors/status/1738146208940482939?s=20
 
Hivi waarabu wanawashwaga na nini, kwanini hawapendi amani?
Sababu ya Kwanza ni Dini ya Kiislam, baada ya mtume kufariki walishindwa kukubaliana nani awe mrithi wa mtume, kati ya baba mkwe na mkwe wa mtu, hiyo tofauti imeendelea hadi Leo.

Sababu ya Pili ni mfumo wa utawala wa Ottoman na Mipaka iliyowekwa na Uingereza na Ufaransa baada ya vita ya Kwanza kuisha.

Waingereza walikosea wakaweka Watu ambao ni Ethno-religious tofauti kwenye nchi Moja, so kila wakati jamii Moja ndogo au kubwa huingia madarakani na kuikandamiza nyingine.

Nikupe mifano
1. Iraq-Iran

Mpaka wa Iran na Iraq una jamii kubwa sana ya Washia ambao wako pande zote za hizi nchi, na kawaida ya Washia na Wasunni hawaivi kabisa so siku zote nchi Moja kati ya hizi hutaka kuwa kiranja wa Washia au Wasunni au kuumaliza Watu inaohisi ni tishio

2. Iraq na Kuwait

Wakati wa Ottoman Kuwait ilikuwa sehemu ya Jimbo la Basra-Iraq lakini Waingereza wakaipa Kuwait nchi na kuindolea Bahari Iraq.

3. Bahrain - Saudia - Iran
Hadi Miaka ya 1800 Bahrain ilikuwa inatawaliwa na watawala wa Persia kwa hiyo Bahrain ikawa na Washia wengi na Watawala wa Iran wote huiona Bahrain kama sehemu ya Iran iliyojitenga na ipo siku wataichukua, Bahrain inapakana na Jimbo/Eneo la Saudia ambao Lina idadi ya Washia na Ndio kuna visima muhimu na Makao makuu Aramco yako kwa hiyo Saudia inaona kitisho cha Usalama wake (Nikipata muda siku nitaandika why Falme zote za Mashariki ya kati zina ugomgvi na Iran).

3. Palestinians - Syria - Lebanon - Jordan na Egypt
Baada ya Waarabu wa Wapalestina kukosa nchi na kukimbilia haya Mataifa jirani, wakasababisha na kushiriki migogoro ya ndani.

Lebanon ilikuwa ni Ufaransa ya Mashariki ya kati na ilikuwa na wakristo wengi sana, na ikawa na inawaunga mkono Israel nje na ndani ya nchi, Wapalestina wengi waliokimbilia huko walisababisha change ya demographic kati ya wakristo na Waislam na kupelekea vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyodumu Miaka 15

Same issue ilitokea Jordan wakamuua Mfalme, Syria walitaka kumpindua Assad, akawaua hadi kwenye kambi za wakimbizi

Egypt Muslim brotherhood ambao ndio baba wa Hamas walitaka kuharibu Usalama wa Misri

4. Yemen - Saudia

Yemen ni Moja ya nchi Complex lakini kwa sababu ni maskini Hakuna anayeipa umuhimu, Yemen ilikuwa North na South na muungano wake ni wa Juzi tu Miaka ya 1990, Kati ya Watu 35 40 ni Washia na Saudia na Wayemen wote wana migogoro ya Mipaka na wanaamini kila nchi ni zawadi ya Uingereza
 
Back
Top Bottom