Sababu ya Kwanza ni Dini ya Kiislam, baada ya mtume kufariki walishindwa kukubaliana nani awe mrithi wa mtume, kati ya baba mkwe na mkwe wa mtu, hiyo tofauti imeendelea hadi Leo.
Sababu ya Pili ni mfumo wa utawala wa Ottoman na Mipaka iliyowekwa na Uingereza na Ufaransa baada ya vita ya Kwanza kuisha.
Waingereza walikosea wakaweka Watu ambao ni Ethno-religious tofauti kwenye nchi Moja, so kila wakati jamii Moja ndogo au kubwa huingia madarakani na kuikandamiza nyingine.
Nikupe mifano
1. Iraq-Iran
Mpaka wa Iran na Iraq una jamii kubwa sana ya Washia ambao wako pande zote za hizi nchi, na kawaida ya Washia na Wasunni hawaivi kabisa so siku zote nchi Moja kati ya hizi hutaka kuwa kiranja wa Washia au Wasunni au kuumaliza Watu inaohisi ni tishio
2. Iraq na Kuwait
Wakati wa Ottoman Kuwait ilikuwa sehemu ya Jimbo la Basra-Iraq lakini Waingereza wakaipa Kuwait nchi na kuindolea Bahari Iraq.
3. Bahrain - Saudia - Iran
Hadi Miaka ya 1800 Bahrain ilikuwa inatawaliwa na watawala wa Persia kwa hiyo Bahrain ikawa na Washia wengi na Watawala wa Iran wote huiona Bahrain kama sehemu ya Iran iliyojitenga na ipo siku wataichukua, Bahrain inapakana na Jimbo/Eneo la Saudia ambao Lina idadi ya Washia na Ndio kuna visima muhimu na Makao makuu Aramco yako kwa hiyo Saudia inaona kitisho cha Usalama wake (Nikipata muda siku nitaandika why Falme zote za Mashariki ya kati zina ugomgvi na Iran).
3. Palestinians - Syria - Lebanon - Jordan na Egypt
Baada ya Waarabu wa Wapalestina kukosa nchi na kukimbilia haya Mataifa jirani, wakasababisha na kushiriki migogoro ya ndani.
Lebanon ilikuwa ni Ufaransa ya Mashariki ya kati na ilikuwa na wakristo wengi sana, na ikawa na inawaunga mkono Israel nje na ndani ya nchi, Wapalestina wengi waliokimbilia huko walisababisha change ya demographic kati ya wakristo na Waislam na kupelekea vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyodumu Miaka 15
Same issue ilitokea Jordan wakamuua Mfalme, Syria walitaka kumpindua Assad, akawaua hadi kwenye kambi za wakimbizi
Egypt Muslim brotherhood ambao ndio baba wa Hamas walitaka kuharibu Usalama wa Misri
4. Yemen - Saudia
Yemen ni Moja ya nchi Complex lakini kwa sababu ni maskini Hakuna anayeipa umuhimu, Yemen ilikuwa North na South na muungano wake ni wa Juzi tu Miaka ya 1990, Kati ya Watu 35 40 ni Washia na Saudia na Wayemen wote wana migogoro ya Mipaka na wanaamini kila nchi ni zawadi ya Uingereza