Mataifa ambayo ni vigumu kuyavamia kijeshi duniani

Hii list inavichekecho kwa hiyo ni rahisi zaidi kuivamia Russia kuliko Canada,Japan,North Korea,Switzerland na Israel.

Hapa Duniani nchi pekee ambayo ni ngumu kuivamoa kijeshi na Russia.just imagine nchi tajiri zaidi ya 32 Ulaya na America zimeungana kuikabili yenyewe toka miaka ya 1940.
 
Wanam control wapi!?
Je China kutoa sapoti ya kiuchumi kwa Russia hiyo sio sapoti!?
Kipindi West na USA wanatoa economic sanctions kwa China waliweka wazi kabisa hakuna taifa linalotakiwa lifanye biashara na Russia.
Ila China ilisimama ilimpa fedha Russia na ikawa inanunua mafuta na gesi Russia ambayo yalisusiwa na West.
US na EU walikuja juu na walimjia juu Jinping,ila Jinping alitamka wazi hatoingilia vita yeyote hapa duniani ikiwemo ya Russia,ila kiuchumi atasaidia.
Huyo Russia kasimama pale narudia tena uelewe hiyo Russia kasimama pale sio ujanja wake,Russia HANA UCHUMI HUO WA KUHIMILI vikwazo vya West peke yake,but Giant China ndio kamuokoa kwa fedha zake.
 
Kwani wewe upo Dunia ya ngapi,Russia ndio nchi pekee duniani inayoongoza kwa rasilimali nyingi,mtu mwwnye rasilimali hizo zote unaweza semaje eti hana cha kufanya bila China.Ni sawa na Bakhresa sasa hivi ailishe Tanzania nzima kwa ngano halafu useme tukiacha kununua Bakhresa hata survive sasa unajiuliza wewe usiponunua hiyo products utaishije?? so kwa vyovyote vile ni lazima utanunua.
Hoja ni kuwa Ulaya hana malighafi so pamoja na kuban imports za Russia bado wananunua kwa back door hivyo hivyo kwa China na India wanaihitaji Russia kuliko Russia anavyozihitaji.Its all about economics.
 
Mzee hio point umekomaa nayo, unazungumza vipi kuhusu India ambae alikataa matakwa ya west na akaendelea ushirikiano na Russia kiuchumi.

India bado inanunua mafuta kutoka Russia na wanashirikiana kwenye nuclear hadi tech, Modi juzi hapa alikuwa Moscow wakiendelea ushirikiano kiuchumi.

Je umeona US akimsusa India?

Hayo anayofanya China haimaanishi China kwamba ni mbabe kiuchumi kuliko hao wazungu.
Pia India imekuwa msaada mkubwa sana kwa Russia.

Geopolitics haziendi hivyo.
 
Mkuu nimependa ulivyo eleza, kuna kampuni ya Russia inaitwa Rosatom ambapo Putin ndiye founder.

Rosatom walishawauzia US uranium na waka enrich hio Uranium hapo Russia.

Ukweli ni kwamba hio China sio mwamba inampa msaada Russia bali na wao wanafaidika tena pakubwa.

Russia imebarikiwa sana mali asili, aio gas wala mafuta, madini n.k

Ndio maana hadi leo India anaendelea kushirikiana na Russia hasa kwenye biashara za mafuta, nuclear na masuala mengine ya tech.

Kwa maana hao Rosatom duniani kwenye tech za nuclear hakuna shirika linawafikia.
Nuclear medicine, ct scan, pet scan.

Wana deal na nuclear kuanzia kutumia kama energy, silaha hadi kutumika kama matibabu.

Sasa kama wanafanya biashara hadi na US ambae ni adui yao, hawa wengine ni kina nani wasiifanye nao kazi.

Russia ni kama maji, usipo oga utakunywa.
 
Mtu anakwambia China haijawahi kupigwa sanctions na USA.
Kumbe hadi sasa USA imeipiga China sanctions na ina mpango wa kumuongezea sanctions.


 
Nimekuwekea sanctions kule USA alizomuwekea China kwasababu ya kumsaidia Russia kiuchumi.
Contribution ya China kwa Russia kiuchumi usifananishe na ya India.
India anatoa MCHANGO MDOGO SANA KIUCHUMI kwa Russia.
India inafanya biashara na Russia basi.
Ila China inatoa hadi FINANCIAL AID kwa Russia.
Je hivyo vinafanana!??
Nenda katizame msaada wa kiuchumi China anaotoa kwa Russia kama unafanana na wa India.
 
Financial aid kiasi gani?
Na hio financial aid ya kufanyia nini?
Hio financial aid ina mchango wa asilimia ngapi kwa Russia katika bajeti yao? na kiuchumi?
 
Leo hii huyo Bakhresa tukimgomea ngano yake sijui atauzia wapi??
Au atatuuzia kilazima!??
Hiyo Russia ilipowekewa vikwazo taifa ambalo lilibaki kununua gesi na mafuta ni Germany peke yake kwa miezi ya kwanza.
Mapato yalishuka,China ndiye aliyenunua mafuta kwa wingi na gesi kwa wingi kutoka Russia.
Sio hivyo tu China pia alitoa msaada wa kifedha.
China ina uwezo wa kununua mafuta kwingine pasi na kuitegemea Russia,China ina deal na VENEZUELA ya kununua mafuta mengi tu pamoja na gesi.
Hiyo Yemeni ina rasilimali nyingi ya mafuta,dhahabu na gesi kuliko hata Russia na ni nchi masikini kwa kukosa wawekezaji kuja kuwekeza ndani ya Yemeni.

Kuwa na rasilimali ni kitu kingine na kuiuza hiyo rasilimali ni kitu kingine.
 
Bwana mdogo punguza hisia.

Yaani mimi nishikilie uhai wa uchumi wako halafu ulete mashindano ya kunishusha nikuchekee tu ?
 
Punguza hisia katika masuala mazito yanayo hitaji data na facts za kulinda maoni yako.
 
Swali jepesi hili kwa yoyote atakaye taka kujibu.

Mfano wewe ndie kiongozi wa Urusi[ Putin ] ni msaada gani utautaka toka kwa mshirika wako mkubwa China kwa kutazama nafasi aliyonayo duniani, je ni msaada wa makombora kupambana na adui yako uwanja wa vita ambae naye atazidishiwa msaada wa silaha na washirika wake ama msaada wa uchumi utakao kabiliana na utitiri wa vikwazo ulivyo wekewa ?

Zingatia fedha/uchumi ndio unao endesha vita.
 
Ni ngumu kujitenga na dunia kwa sasa japo inawezekana ila ni kwa maumivu makali sasa hapa itategemeana na akili na uvumilivu wa unao waongoza.
 
Jibu jepesi ni msaada wa kiuchumi tu.
Kwasababu licha ya Russia kuwa na teknolojia ya silaha ila bado atahitaji fedha za kuweka bajeti ya utengenezaji hizo silaha kwa viwanda vyake vya ndani.
Una vikwazo vya kiuchumi vilivyodumaza mapato utawezaje kuendesha uzalishaji silaha!??
Vita yenyewe inahitaji fedha pia kuiendesha tofauti na silaha peke yake.
Magari yale hayatembei bure,askari hawapigani bure,vyakula vya askari haviokotwi vinahitaji pesa pia.
 
Always research si about Europe America and Asia not Africa.
 
Sijui kwa Nini 10 countries inapendwa sana katika listings nyingi,kama hii list ingekuwa na ranking basi Bhutan isingekuwemo,maana sababu zinazidiwa na na zingine kama Seychelles, Malta na wengine
 
Jamaa katumia kimombo kuandika hekaya zake za uongo lakini Bahamian nzuri aliowataja baadhi yao washabondwa hasa huyo Israel tena na migambo inamchachafya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…