Ndipo uache mahaba, nataka nijue China ilifanya nini baada ya kuzuiliwa installation za 5G tech.
Hao EU usifikiri ni wajinga , kuna bidhaa wata support kuna bidhaa watakataa, uchumi wa China hautegemei EVs, China kwa sehemu kubwa ameminywa kende yupo anajitutumua tu.
Hao EU ndio hao hao US , masuala ya kiuchumi ni complex, mtaendelea kila siku kusema uchumi wa China unapanda kasi mwakani anamzidi US.
Hivi unafikiri hao EU kuna nchi inataka ione China anakua kiuchumi kuliko US?
China ina safari ndefu, production kubwa ya EVs sio kukamata uchumi wa dunia.
Utaendelea kuruka ruka kama maharage ya Mbeya bro.
Hizo EV nimekutolea mfano kama wewe ulivyotolea mfano wa Huawei 5G,kwani China anategema uchumi wake kwenye 5G!!??
Suala la kuzuia 5g lilikuja sawa na suala la kui ban Huawei kutumia google pamoja na suala la USA kuongeza ushuru kwenye bidhaa za China.
Mwishowe China alizuia madini mkakati ya kuundia simu kwa USA hususan Iphone,akaongeza ushuru mkubwa na kodi kubwa katika uzalishaji wa hizo simu ndani ya China,aliongeza ushuru mara tatu ya alivyoongezewa yeye katika bidhaa za USA,alizuia vipuli vya utengenezaji boti kuelekea USA,alizuia malighafi chuma kuelekea USA.
Na katika miaka USA wali slow down kukua kiuchumi basi ni kipindi hiko.
Hadi wanauchumi wa USA walimsisitiza Trump amalize trade war na China.
Hao Ulaya kama wao unadhani wamembana kende China wasingekua wanapishana kwenda Beijing kuzungumza na Jinping.
Tulitarajia China ndio awe anazunguka mataifa ya Ulaya kuomba unafuu,badala yake mataifa ya Ulaya ndio yanaenda China kufanya nae negotiations.
Na wakati huo huo suala la BRI kuna mataifa ya Ulaya yalijitoa ikiwemo Italy,mwaka huu kiongozi wa Italy ameenda China kuomba kurudi kwenye BRI initiative.
China kwa uchumi tayari kiuhalisia amesham overtake USA kilichobaki kwa USA ni siasa tu ama propaganda za kumuonesha bado yupo juu.
*
China inaongoza kwa contribution ya manufactured goods duniani zaidi ya 45% asilimia zilizobakia wanagawana mataifa mengine.
*China is the most industrialized nation.
*China ndio taifa ambalo benki kuu yake imekopesha usawia wa WB na IMF.Kitu ambacho akijaribu kufanya USA kwa benki yake anafirisika.
Ila benki kuu ya China ilitolewa ripoti kuwa imekopesha mataifa 138 na mataifa 38 yamesamehewa madeni.
Huko unakosema China amebanwa kende kabanwa kende wapi!??
Basi kama hao watu wa Ulaya na USA wamembana China kende tusiwaone wakipanga ziara za kwenda Beijing wakae watulie kwao.