Mi mi
JF-Expert Member
- Jul 14, 2024
- 2,748
- 5,112
Watu humu wanachukulia ubishani wa humu na uelewa wetu finyu kuwa hivyo ndivyo nchi zinapaswa kuongozwa hili ni tatizo.Yani wametoa sababu nyepesi sana aisee.
Mbaka nawashangaa.
Tanzania tuna mgogoro na Malawi ila hatupo tayari kuivamia Malawi si kwamba huo uwezo hatuna hapana tunao ila zile tu athari za kagera war sidhani kama kuna kiongozi atakuwa na ubavu wa kuipeleka nchi vitani kipuuzi.
Nchi zinaongozwa na washauri na wataalam wa masuala kadhaa hivyo hupima faida na hasara za maamuzi yao tena haya mataifa makubwa ambayo yapo katika vita za kushushana huwezi ipeleka nchi vitani kwa sababu za kipuuzi.
China wana mpango wa mwaka 2049 sio wa leo huu mpango, sasa fikiri taifa linawaza 2049 lifanikishe nini ndio uliingize vitani kwa sababu ya hisia na mihemko yako.
Xi yupo kwenye nafasi mbali mbali za uongozi wa China kwa zaidi ya miaka 40 sasa maana yake anaifahamu China, Taiwan na marekani kuliko sisi humu tunaotumia hisia zetu kutoa maamuzi