Israel imewekwa pale badala ya Uganda sababu waliona pale Middle East ndio kwenye mnofu pesa+mambo ya dini. Na jina hilo waliona kwenye bibilia jina la Yakobo ni Israel wakaona watumie jina la Israel ndio bibilia ilisema atakaye mdhuri Israel na mimi tamdhuri. Waliyapika vizuri wale ma Zionists 😄
Israel ndio ikiwa pale wataingiza mabillions kwa kuza silaha n.k. We huoni ilo taifa linapebda kunywa damu.
Itabidi hii mitaala ya elimu za madrasa ipitiwe upya.
Kwa taarifa yako
1. Israel ni jina la mtu aliejulikana kama Yakobo.
2. Huyu Yakobo au Israel ni pacha wa Esau wakiwa ni watoto wa Isaka na mke wake Rebeka.
3. Isaka ni mtoto wa Ibrahim akiwa mtoto pekee aliyezaliwa na Sara.
4. Kabla ya kumzaa Isaka, Ibrahim alizaa mtoto anaitwa Ishmael au Ismail. Huyu akizaliwa na mtumishi wa Sara kutoka Misri kipindi Ibra alipoenda kule na kudanganya Sara ni dada yake hivo Farao akajitwalia awe mke, baadae akagundua na kumrudisha kwa Ibra pamoja na mjakazi. Ibrahim na mkewe wakaondoka kurudi Kaanani.
5. Ishamael aliondolewa asije kurithi pamoja na Isaka. Ishmael alizaa watoto 12 pia.
6. Wote Isaka na Ishmael walishirikiana kumzika Ibrahim pindi alipofariki.
7. Mrithi wa mali na ahadi za Mungu akabaki kuwa Isaka, kisha Yakobo/Israel kufuatia kumpora Esau uzawa wa kwanza. (Usije kusema kumbe uporaji wa familia ya Israel ulianza na baba yao, mimi sijui).
8. Israel alizaa watoto 12 kisha akahamia Misri kukwepa njaa, lakini pia akimfuata mtoto wake Yusuf aliyeuzwa utumwani na ndugu zake lakini akaibuka kuwa mtawala akishika nafasi ya pili katika utendaji na maamuzi baada ya Farao.
9. Alipofariki, Israel alirudishwa Kaanani kuzikwa mahali alipozikwa baba yake IIbrahim.
10. Baada ya miaka 400 kupita, wana wa Israel waliondoka Misri kwenda Kaanani kuimiliki nchi ambayo Mungu alimpa Ibrahim na uzao wake ambao ni Israel. Wakati wanarejea waliambiwa wasipigane na watoto wa Esau ndugu zao. (Usiniulize kwanini Mungu hakuwakataza kuwapiga wana wa Ishmael, mimi sijui muulize Mungu, si yupo!!!). Musa aliongoza msafara akisaidiwa na Harun, na kisha baadae Joshua aliwaongoza.
11. Ibrahim aliwasiri Kaanani akitokea ilipo Iraki ya sasa. Hapo sasa ndipo wanasema ngumu kuwatofautisha waIsrael na waarabu wengine ndio maana akina Harnie wanadunguliwa hata bila kujua nani kadungua.
12. Mipaka ya Israel ya sasa na ile ya zamani haipo sawa. Ya kwanza inaikusanya Jordan yote kuelekea Lebanon nk.
Sasa iko hivi, wakati taifa la Israel limesambaratishwa na kufutwa wayahudi wakitawanyika, miaka ya 1940 na kitu huko Umoja wa Mataifa wakawaza kuwapatia taifa lao ili kuepuka madhira yawapatayo mfano mauaji ya waNazi chini ya Hitler kiongozi shupavu wa Ujerumani. Ilifikiriwa Uganda na Ethiopia lakini ikaamuliwa wamegewe ardhi kwenye eneo lao la ahadi.
Hii ya kumegewa ardhi eneo lao la asili haikuwa bahati mbaya. Tambua hii ni ahadi ya Mungu, agano la Mungu na Ibrahim. Na halitakaa libadilike, ni sheria/law. Fanya ufanyalo lazima Israel atabaki hapo alipo ukijaribu kumfuta utafutika mwenyewe.
Lakini pia ijulikane kwamba, miaka ya 1940 haikuwa mara ya kwanza Israel kurudishwa eneo hilo baada ya kuondolewa. Kwanini? Ni agano, makubaliano ya Mungu na Ibrahim. Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo.
Zingatia, atafurushwa kila anaejaribu kuiondoa Israel. Ndio maana labda Iran kaona asimlipie kisasi Harnie wa Hamas, sina uhakika lakini yaweza kuwa kuna sababu tofauti.
Ni hayo kati ya mengi yanayojulikana.