Mkuu, chanjo ilishafanyiwa majaribio kwa raia wao, ndio maana wanawapa chanjo raia wao. Na bado chanjo hazitoshi kuwapa raia wao wanajaribu kutengeneza zaidi.
Sie tusubiri makombo/msaada kama kweli tunazitaka lakini kujifanya guinea pigs ni uongo.
Sisi tutaendelea kuletewa kila kitu, na kujifanya wazuri wa kuchagua na kukataa ni kujipa moyo, umaskini wetu mpaka wa fikra ndio umetufanya kila siku tue watu wa kusubiri tu. Ubongo tunao lakini hatutumii, tumelala sana.
Wana sayansi wapo lakini wanaamini uchawi kuliko sayansi.
Tuache unafiki, chanjo kuletewa ni chaguo lao sisi chaguo letu ni kuchomwa. Na kuchomwa hamna mtu anaelazimishwa. Na kwa nini tuchomwe chanjo wakati ugonjwa wenyewe
"haupo"?.