Mataifa ya Magharibi tayari yameiona nguvu ya China

Mataifa ya Magharibi tayari yameiona nguvu ya China

Shing Yui

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2015
Posts
15,168
Reaction score
38,049
Mataifa ya Magharibi yamo kwenye mfumo wa ushindani na China.

Changamoto za ulimwengu zinawalazimisha kuwa washirika zaidi kama Kongamano la Usalama la Munich inavyojaribu kutafuta uwiano wenye manufaa kwa pande zote.

Wakati umechaguliwa vyema:
Rais Joe Biden wa Marekani anaanza ziara yake barani Ulaya - kwanza kwenye mkutano wa kilele wa mataifa ya G7 nchini Uingereza, kisha mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO mjini Brussels. Viongozi wa mataifa ya muungano huo wenye nguvu kubwa kijeshi wanakutana kabla ya Biden kukutana na Rais Vladimir Putin wa Urusi mjini Geneva.

Katika mazingira kama hayo, ndipo Kongamano la Usalama la Munich linapochapisha ripoti yake mpya ya Usalama iliyopewa jina "Baina ya Hali za Uhasama – Ushindani na Ushirikiano".

Jina lenyewe tayari linaelezea kizungumkuti kikubwa kilichopo: serikali za Kimagharibi zinajihisi kuwa zinakabiliwa na changamoto kubwa, hasa kutoka China, lakini wakati huo huo zinahitajiana sio tu kama washirika wa kibiashara, bali pia kukabiliana na changamoto kubwa zaidi za kilimwengu.

Mfano wa wazi kabisa ni janga la virusi vya corona, mabadiliko ya tabia nchi na ushindani wa silaha za nyuklia.

Kwa hivyo, licha ya yote mengine, China inaonekana kuwa ni mshirika rasmi wa kimkakati na mshindani wa Umoja wa Ulaya kwa wakati mmoja.

Uimara wa China
China ambayo inaongozwa na wakomunisti wanaoendesha nchi kwa ubepari wa dola imefanikiwa katika kile ambacho Umoja wa Kisovieti ulishindwa: mchanganyiko wa utawala wa kiimla na mafanikio ya kiuchumi na ukuwaji wa ustawi wa wananchi wao.

Brasilien Brasilia BRICS Treffen 16.07.2014 Xi Jinping

Rais Xi Jinping wa China

Hii ndiyo sababu kwa nini kauli za kujilinda zinazosikika mara kwa mara kwenye hutuba za Joe Biden, kama mathalani pale anaposema: "Tunapaswa kuonesha kwamba serikali za kidemokrasia bado zinaweza kuwahudumia watu wetu vyema katika dunia inayobadilika."

Inaonekana kwamba ikiwa taifa/China lenye watu bilioni 1.4 linakuwa kiuchumi kwa kiwango cha tarakimu mbili kwa miaka miongo minne mfululizo, inamaanisha kuwa taifa hilo kuna wakati fulani linaweza kuitafsiri nguvu yake ya kiuchumi kuwa nguvu ya kisiasa – na bila ya shaka pia kuwa nguvu ya kijeshi.

Na Beijing imejiwekea malengo makubwa: kufikia maadhimisho ya miaka 100 tangu kuundwa kwa Jamhuri ya Watu hapo mwaka 2049, China inataka kuwa taifa lenye nguvu na la kisasa la kisoshalisti, inataka iwe na uwezo wa kuweka na kuunda kanuni na kuwa na kiwango cha juu cha teknolojia, uchumi na utamaduni. Maana yake kuwa taifa linaloongoza Dunia.

Ripoti hiyo ya Usalama ya Munich inaeleza kwamba wawakilishi wa demokrasia za kiliberali sasa wanataka kujilinda dhidi ya ushindani usio wa kiliberali.

Kama anavyosema Tobias Bunde, mmoja wa waandishi wa ripoti hiyo na ambaye pia Mkurugenzi wa Utafiti wa Kongamano la Usalama la Munich akimnukuu Joe Biden kwenye utangulizi wa ripoti yenyewe: "Tupo kwenye njia panda na serikali za kidemokrasia ulimwenguni lazima ziungane pamoja.

Kiuhalisia mabeberu/umoja wa kujihami wa nchi za magharibi wameshazidiwa sema tu wamebaki na maneno matupu ya mwishomwisho kitu ambacho wanakielewa ila hawataki kukiri kwa uwazi ila kwa kificho.

Jambo lingine inaonekana China ipo bega kwa bega na mahasimu wa NATO kama Urusi iliyokuwa Muungano wa kisovieti, Iran inayozidi kupata nguvu Mashariki ya Kati, Korea Kaskazini inayowatishia NATO kwa silaha za nyuklia, Belarus, Venezuela na mataifa yote yanayoonekana kushikamana na sera za kikomunisti.

Kibaya zaidi kwa Ulaya Magharibi ni kwamba, mataifa kama Ujerumani, Uingereza, Ufaransa na wanachama wengi wa umoja wa kujihami wa nchi za magharibi wanaona kufanya kazi na China, Urusi, Iran kuna faida kuliko kuendelea kupangiwa na Marekani kila kitu.

Inaonekana miaka michache ijayo Marekani itajikuta imebaki yenyewe ikiendeleza uhasama ambao uhasama huo utakuwa ukiigharimu yenyewe.

Juzi kati rais Putin wa Urusi alisema, namnukuu.

(Marekani inakumbwa na matatizo ambayo madola makubwa hukumbana nayo. Amebaini kuwa matatizo ambayo Marekani inakabiliana nayo yanatokana na nguvu ilizonazo na sasa imeshindwa kutatua matatizo hayo na hali hiyo ndiyo ile ile liliyokumbana nayo Shirikisho la Sovieti)

Putin ameongeza kuwa, watawala wa Marekani wanadhani kuwa kutokana na kuwa nchi yao ina uwezo mkubwa wa kisiasa, kiuchumi na kijeshi basi inaweza kukabiliana na matatizo ya aina zote. Rais wa Russia amesema tatizo la jamii kama hiyo ni kuwa hudhani ina nguvu za kutosha na iwapo itakosea haitapata madhara.

Rais Putin ameendelea kusema matatizo makubwa ambayo Marekani inakumbana nayo na sera zake zilizofeli za kutumia mabavu na kusema, hivi sasa matatizo ya nchi hiyo yanazidi kuongezeka na itafika wakati ambao haitaweza kuyatatua.

Kwa maana hiyo Marekani imeingia ule ule mkondo ambao ulichukuliwa na Shirikisho la Sovieti, kwa kuzingatia hali ya hivi sasa ya Marekani, Rais wa Russia amesema nchi hiyo iko katika ule mkondo ambao ulikuwa umechukuliwa na Shirikisho la Sovieti baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia na ni mkondo ambao hatimaye ulipelekea shirikisho hilo kusambaratika.

Putina halikadhalika amekosoa sera za maamuzi ya upande mmoa na utumiaji mabavu ambazo zinashuhudiwa Marekani hata baada ya kuondoka madarakani Donald Trump.

Putin amesema Marekani inakosea inapodhani kuwa ina nguvu za kukabiliana na tishio kutoka nchi zingine.

Wakuu mnaonaje hizi siasa za kimataifa? Ni kweli usipojipanga vyema utapangwa?

Karibuni kwa maoni yenu.
 
R.I.P Magufuli

Ulikataa lock down kwa watanzania licha ya chadema kukimbia bunge na kwenda kukaa lockdown.
Sasa uchumi umekua.
 
Ni dhahiri anguko la marekani lipo mbioni Sana na ukisikiliza kauli za viongozi wakuu utaliona mfano: "make America great Again" kwani ni lini waliacha kuwa great?

Lakini pia ukiangalia vikwazo mbalimbali marekani wamekuwa wakijaribu kuweka dhidi ya China, Ulaya na Canada vyote vinaanshiria kushindwa kwenye ulingo wa biashara huria hivyo kutumia vikwazo Kama sehemu ya kuirekebisha mahusiano yake kibiashara. Matokeo yake yamekuwa tofauti na matarajio maana na wenyewe wamewekewa vikwazo.

Ukisoma machapisho mengi yanasema between 2024 - 2032 China itakuwa imeipita marekani kwa kila nyanja Kama uchumi wake utaendelea kukua kwa rate inayoendelea kukua kwa sasa
 
Dah! Hamjasoma bandiko au mimi ndio sieleweki 😲
sio wewe pekee mkuu, hata mm nimebaki nashangaa... umechambua vizuri zana sasa sielewi ni wapi hapaeleweki,

ila nimehisi tu huu uchambuzi ujo juu ya level yao,
labda wamezoa kubishana kuhusu ccm na chadema, kwa hyo andiko kama hili ni gumu sana kwao. nadhani labda ndio sababu
 
Ni dhahiri anguko la marekani lipo mbioni Sana na ukisikiliza kauli za viongozi wakuu utaliona mfano: "make America great Again" kwani ni lini wakiacha kuwa great?

Lakini pia ukiangalia vikwazo mbalimbali marekani wamekuwa waharibu kuweka dhidi ya China Ulaya na Canada vyote vinaanshiria kushindwa kwenye ulingo wa biashara huria hivyo kutumia vikwazo Kama sehemu ya kuirekebisha mahusiano yake kibiashara. Matokeo yake yamekuwa tofauti na matarajio maana na wenyewe wamewekewa vikwazo.

Ukisoma machapisho mengi yanasema between 2024 - 2032 China itakuwa imeipita marekani kwa kila nyanja Kama uchumi wake utaendelea kukua kwa rate inayoendelea kukua kwa sasa
Unaona kama mimi. Amerika ya leo sio ile Amerika tuijuayo!
 
sio wewe pekee mkuu, hata mm nimebaki nashangaa... umechambua vizuri zana sasa sielewi ni wapi hapaeleweki,

ila nimehisi tu huu uchambuzi ujo juu ya level yao,
labda wamezoa kubishana kuhusu ccm na chadema, kwa hyo andiko kama hili ni gumu sana kwao. nadhani labda ndio sababu
Wanamuwaza JPM tu
 
Ukubwa wa dola ni kuwa mzalishaji bidhaa ambazo dunia inazihitaji-nadhani marekani huchukua bure bidhaa zinazozalishwa nje ya mipaka yake-kwa kigezo cha mafuta kuuzwa kwa dola-nishati mbadala ni hatari sana kwa taifa la marekan-mtego wa free market umemnasa muasisi. Ni dhahiri Us inakwenda kuanguka-asante mleta hoja.
 
Dah! Hamjasoma bandiko au mimi ndio sieleweki 😲
China kwasasa ni unstopable. Yani inapiga one man show na imashinda kuanzia kwenye masuala ya anga za juu, jeshi, teknolojia ya gadgets kote huko inaendelea kujiimarisha.
Ndiyo nchi pekee yenye space station yake peke yake.
China kwasasa sijui wafanye nini kuizuia .
 
China kwasasa ni unstopable. Yani inapiga one man show na imashinda kuanzia kwenye masuala ya anga za juu, jeshi, teknolojia ya gadgets kote huko inaendelea kujiimarisha.
Ndiyo nchi pekee yenye space station yake peke yake.
China kwasasa sijui wafanye nini kuizuia .
Inabidi wamnyoshee tu kofia kwa jinsi alivyo fanya space program Kama 5 mfululizo kwa mafanikio makubwa kuazia na tianwei -1 hadi zile core module za space station
 
R.I.P Magufuli

Ulikataa lock down kwa watanzania licha ya chadema kukimbia bunge na kwenda kukaa lockdown.
Sasa uchumi umekua.

Taarifa iliyoletwa haihusiani na ulichokiandika, na ukizingatia hii ni international forum
 
China kwasasa ni unstopable. Yani inapiga one man show na imashinda kuanzia kwenye masuala ya anga za juu, jeshi, teknolojia ya gadgets kote huko inaendelea kujiimarisha...
Bila shaka baada ya miaka 10-15 China ndio itakuwa mpangaji wa mambo mengi ya dunia
 
Back
Top Bottom