JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 2,118
- 4,863
Katika hali ya kustaajabisha leo wakati wa uapisho wa Raisi Trump matajiri watatu wakubwa zaidi marekani na dunia nzima, Elon Musk, Mark Zuckerberg, na Jeff Bezos na demu wake Sanchez, Boss wa Google, wamekaa siti ya mbele kwenye shughuli ya uapisho wa raisi Trump wakati mawaziri wake wamekaa siti ya nyuma.
Ni dhahiri sasa Trump anaheshimu zaidi matajiri kuliko watendaji wake wa serikali.
Imagine mwanasheria wake mkuu, na waziri wake Robert Kennedy Jr, na mawaziri wake wote kawaweka nyuma ya matajiri hawa.