Parabora
JF-Expert Member
- Jul 6, 2019
- 1,504
- 2,203
Lockdown bado inaendelea hapa Uswisi japo serikali imedhibiti sana maambukizi mapya mpaka leo asubuhi kwa mujibu wa takwimu za serikali kuna jumla ya wagonjwa 43,000+ na waliokufa zaidi ya 19,000+ ni idadi ndogo sana kulinganisha na nchi zilizotuzunguka
Matajiri wa hapa jijini GENEVA kushirikiana na Serikali imesema hakuna hata mhamiaji mmoja atakaekufa njaa kwa kipindi hiki cha zuio la kutoka nje, haijalishi umeingiaje utapata huduma zote muhimu bure KILA SIKU katika kipindi hiki na taratibu zingine zitafanyika baada ya hali ya kawaida kurejea na pia serikali imetangaza itaanza kulipa pesa kwa wahamiaji wote maskini na vibarua waliokuwa wanalipwa kwa saa ambao wamepoteza ajira zao kwa ajili ya kulipia gharama za makazi na kujikimu na ambao hawana makazi maalum serikali imewapa apartment za kukaa kwa kipindi hiki chote na mpango huu unatarajiwa kusambaa nchini kote kuanzia wiki ijayo
Kwa foleni iliyokuwepo juzi na jana inakadiriwa ni zaidi ya wahamiaji 1300+ walienda kuchukua chakula hiki, hivyo matajiri hawa na serikali wameamua kuweka utaratibu huu katika kila mtaa jijini hapa kwa kununua supermarket kubwa kwa mda huu wote wa hili janga ili zisitishe huduma zao za kuuza na ziweze kuwa zinagawa vyakula bure kwa wahamiaji kila siku. Wazawa hawana shida kabisa na masuala kama haya wao wamejitosheleza kwa kila kitu.
Uswiz ilichukua hatua muhimu kabisa za kupunguza makali ya maisha kwa raia waishio nchini humu tangu mwanzo, walipunguza kwa kiasi kikubwa bei ya bidhaa muhimu kama maji,gesi na umeme na hii hatua yao ya kugawa chakula bure imekuwa nafuu kwa wahamiaji hasa wale waliokuwa na mikataba ya mda mfupi na malipo ya saa kama vibarua, Radio na TV za hapa nchini kila mda zinatangaza na kuhamasisha watu wasio na uwezo wa kumudu kupata chakula wakachukue chakula, wakuu hapa hata mimi leo nitaenda,najiandaa baadae nitatia timu kupanga foleni haiwezekani ninunue kwa pesa wakati kipo cha bure tena ni bora kabisa kuzidi ninachonunua
Pia serikali imetangaza kuongeza maslahi manono kwa wale watakaojitolea kufanya kazi katika nyumba za wazee, walemavu na watoto yatima katika kipindi hiki cha janga la corona. Hapa ndio unaona umuhimu wa nchi kuwa na uchumi mkubwa pamoja na sera nzuri kwa raia
parabora
Geneva-Switzerland
Chukua hatua stahiki, Corona ipo na ni hatari