Nyie ndio mnaamini Bakhresa aliuza kahawa pale msikitini akaanzisha kiwanda cha kusaga nafaka taratibu hivyo hadi akawa bilionea. Upewe mashine ya kusaga tuone kama utapata hata utajiri wa milioni 50. SAS anawatazama uko.
Au mnakuja kwa mzee Gulam Dewji na mwanae Mo mnasema walipambana, ni sawa walipambana. Ila hata wewe tukikupa vile viwanda vya nguo bure kwenye ubinafsihaji, na ukavitumia kama dhamana kukopea mabilioni nje, na tukakupa mashamba ya mkonge sawa na bure miaka 20 baadae huwezi shindwa kuwa bilionea mkubwa.
Huwezi nipa klabu kubwa kwa hela za "maandishi" billioni 20, alafu nikiulizwa nimeziweka akaunti gani na zimetumikaje nafoka nakulalamika ninavyopata hasara. Baadae ukarudi ukakuta sipo bilionea.
Sasa hayo yote huwezi yapata bila mkono wa kisiasa au kuwa na wanasiasa nyuma. Katafute mmiliki wa Kagera kiwanda cha sukari nani, mmiliki wa Mtibwa nani alafu ujue kwanini sukari Tanzania haitoshelezi kwa uzalishaji ila serikali haitaki kuagiza nje tena kwa bei nafuu.
Nilishtuka baada ya serikali ya Magufuli kukisumbua kiwanda cha Dangote kuhusu either makaa ya mawe au clinker (sikumbuki ni kipi hapo) ghafla Rais mstaafu wa Nigeria, Olisegun Obasanjo akafanya ziara binafsi kwa private jet kuonana na Magufuli. Baada siku chache mambo ya Dangote cement yakatulia. Nikaenda kufuatilia kwanini suala linamhusu Dangote alafu Olisegun ndio aje binafsi wakati ana tiketi ya kidiplomasia anaweza kuja kitaifa.
Kiufupi iko hivi, Dangote alitokea familia ya uwezo ila akaongezea kuwa na political and military connection, Nigeria ilitawaliwa na military rulers. Akafanya awe na haki ya kuagiza mchele na sukari nje na kuuza kwa faida kubwa (sababu kwa kutumia siasa aliua ushindani). Baadae Nigeria ikafanya uchaguzi kutafuta kiongozi wa kiraia iachane na utawala wa kijeshi, Dangote akafadhili uchaguzi mkuu wa Olisegun Obasanjo na akashinda.
Obasanjo akaleta sera ya viwanda kwa kiqsi fulani, ghafla Dangote akaanza kujenga viwanda na ghafla akawa bilionea maradufu. Ukifuatilia biashara za Dangote huwa zinapewa subsidiaries, exclusive rights, mara ndio zinakuwa kipaumbele na sera kuu ya serikali. Kwa sasa ana refinery, ni usanii mtupu unaendelea. Dangote ni GSM wa Obasanjo. Na Marais wa Nigeria huwa wanaachiana na kulindana, mnyororo unaendelea na ukitaka kuingia hapo kati wanufaika wako tiyari muingie vita ya wenyewe kwa wenyewe.
Biashara za Afrika zina mkono mkubwa wa kisiasa. Hata pale Misri ni hivihivi, Sudan ni hivi, Somalia baada ya kuharibika ile miaka ya 90 waliokuwa wanahamia Nairobi na Dar kujenga mahoteli na kuanzisha biashara kubwa ni wanasiasa wao waliotoroka. South Africa pale hao ndio kabisa wanafanya biashara ikulu.
Biashara ambayo haina innovation nyuma ni vigumu itengeneze utajiri wa haraka. Biashara za kawaida kama unga na simenti inataka uwekezaji mkubwa (sijui hela utapata wapi), sera rafiki kwako mfanyabiashara hiyo (nani ataweka sera za kuku-favour) na ulinzi (dhidi ya sheria, kesi, upinzani, ushindani). Hivyo vyote vinapatikana kwenye siasa za Kiafrika.
Hao wote uwezo mkubwa kibiashara wanao, kisha tag ya kisiasa ndio inakuja.