Matajiri wakubwa Tanzania si wafanyabiashara bali ni wanasiasa, viongozi wa serikali na ndugu zao, kuonyesha kwamba kuna kitu hakipo sawa

Sasa mkuu mtu kudhamin kampen za uraisi unadhani alikuwa hana hela?
Halafu hio ya kudhamin vyama au kampen ipo dunia nzima, kuanzia USA hadi andora, ni kawaida, usishangae kaka, dunia sio fair play ground, lazima kuna kuviziana kwa hapa na pale,
Sijasema dunia ni fair play wala sijasema kudhamini kampeni alikuwa hana hela. Mbona hujajibu kwanini Rais mstaafu Obasanjo alikuja kutatua mgogoro wa kiwanda cha Dangote?

Kwanza unalinganishaje Marekani wakati wadhamini wa Marekani ni kisheria inatambulika na mgombea anataja amepokea kiasi gani kutoka kwa nani. Wakati kwa Dangote na Obasanjo ni makubaliano binafsi sio kisheria.

Nilichosema ni kwamba biashara za Kiafrika zina mkono wa kisiasa, hapa unapinga kisha unasema Bakhresa alipewa ekari alime sukari kisa "ana uwezo". Tena mtu huyohuyo alipewa NMC miaka ya nyuma. Kampuni ya Mayanga Construction kipindi cha Magufuli ilikuwa inapewa tenda za ujenzi za fedha nyingi hadi inazidiwa, napo utasema "ina uwezo". Magufuli kafa na kampuni hatuisikii.

Kikwete alipoondoka kampuni ya Home Shopping Centre ikafunga biashara, wakati enzi za Kikwete ilikuwa inapiga hela sana. Hutaki kuelewa unakomaa wote hao wana uwezo.
 
Fuatilia hio India unayosema haina picking up ya wanasiasa, Fuatilia ufalme wa Jio unavyowekwa na wanasiasa,

Huawei haikuwa kulinda data wala blabla, ingekuwa kulinda data wangeifungia kutumika USA, Kwanini waliiwekea vikwazo vya kuiua kabisa?

Same kwenye nchi zetu, kingine, hakuna utajiri wa huruma, et tumtoe mtu nanjilinji aje tumpe kiwanda mjini aendeleze, hapana, utajiri ni connection, utajiri ni kuchangamkia fursa, utajiri sio siasa kwamba uanze kulalamika sijui kwenda kwenye mikutano sijui nn, utajiri ni lobbying zinazofanywa kwenye vyumba vya siri,

Mengine yote ni kutafuta justification, india nenda tofauti na serikali kama una hela umeisha,
USA biden anamnyima tender za EV Elon Musk kisa wanatofautiana, inabidi ujue utajiri ni mgumu, ni kumtumia yeyote aliye mbele yako, awe mwanasiasa au lah,

Utajiri sio wa kugawana kama chai, ni ujanja ujanja, na kupiga kazi sana kwa maarifa

Hakuna mbinu nyingine, tukiendekeza siasa za cdm kwamba ccm ndo wametuzuia tusiwe matajiri, nakuahidi, hata tuwaweke cdm nao wataendelea hivi hiv tu
 
Usiseme biashara za Africa, hio ipo dunia nzima,
Siasa zinaplay part, kuanzia USA mpaka China mpaka Andora,

Usiwalaumu wafanya biashara,
France wamemuahidi Elon $1B kama ataenda jenga kiwanda ufaransa, umeona sasa, that is how world work, just live with it or be killed with it
 
Fuatilia hio India unayosema haina picking up ya wanasiasa, Fuatilia ufalme wa Jio unavyowekwa na wanasiasa,
cdm kwamba ccm ndo wametuzuia tusiwe matajiri, nakuahidi, hata tuwaweke cdm nao wataendelea hivi hiv tu
Kwahiyo mkuu unanipinga kwamba utajiri hauna mkono wa kisiasa au unaniunga mkono. Maana nilichosema unakataa, ila maelezo yako yanakikubali.
 
Hakuna sehemu nimelaumu wafanyabiashara mzee. Nimeelezea kinachotokea, wewe unakomaa ku-sugarcoat uhalisia kwa kuuita "uwezo".

France kumpa Musk $1 billion sijasikia, ila hata wakimpa wana faida kama nchi. Kiwanda cha Tesla kikichopo Ujerumani kitagharimu $4 za ujenzi tu. Bado faida ya kodi na ajira. Hapo France ikitoa $1 inakuwa ni investment, uchumi huo.

Na bado huo sio mfano sahihi na Obasanjo & Dangote. Kama Ufaransa ingemwambia Musk njoo ujenge kiwanda alafu tutapiga marufuku mshindani wako kuuza bidhaa kama zako, au tutakutoza kodi kiduchu kuliko wapinzani wako hapo ndio ingekuwa mfano sawa na Dangote & Obasanjo.
 
Nakuunga mkono,
Ila nataka ufute kauli ya Africa, useme utajiri duniani una mkono wa wanasiasa
Nikisema duniani nitataja hata nchi zisizousika. Duniani nchi nyingine zina mahakama independent za usuluhishi wa kibiashara huwezi waletea huo ujinga wa kumchagua fulani auze unga wa muhogo peke yake, akina fulani pekee ndio waagize sukari.

Kule unasema fulani pekee ndio anaweza unda meli za kivita, kwakuwa amefirisika na madeni serikali inalipa madeni yake ili kuokoa uwezo wa jeshi la maji kuendelea kupata melivita. Vitu vinavyoeleweka na hakuna anayepinga.
 
Kupiga marufuku wapinzani wako si ndio kesi za BYD vs Tesla,
Apple Vs Huawei, au wew unaona hizo kesi zipoje?

Alichofanya Obasanjo kuzuia cement ya nje ya Nigeria, ni sawa na alichofanya USA kwa huawei, au alichofanya China kwa Google na WhatsApp,

Hizo ni common practice dunia nzima
 
Siasa na ajira za taasis kama TRA zinazalisha milionea wapya kila siku.
 
Wataje hao wanasiasa wenye hela kumzidi Bakhresa, Mount Meru, Mo au Lake group,


Sometimes tusidanganyane sana, wanasiasa wana hela ila usiseme ndio wenye hela nying nchini, matajiri hii nchi ni wahindi na waarabu
Unataka utajiwe majina ya watu hili iweje?.Au ukapigie porojo kwenye vijiwe vya kahawa.
 
Muda utaongea oneday
 
Umeeleza vyema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…