Matajiri wakubwa Tanzania si wafanyabiashara bali ni wanasiasa, viongozi wa serikali na ndugu zao, kuonyesha kwamba kuna kitu hakipo sawa

Utapambania wapi bro bila fair play .sasa hivi kuna Ka kikundi kanadhani ndo Kako na mandate ya kuongoza.
 
matajiri wa kisiasa uongozi wanalinda sana himaya yao, mara nyingi kwa kutumia vyombo vya dola kama polisi, na sasa hata wanajaribu kutumia jeshi la ulinzi, JW.
Sasa naelewa kwa nini ma askari huitwa MBWA WA CCM.

Shida sio hao wanasiasa shida ni wananchi na majeshi yao kukubali kuwa wajinga.

Waacheni wanasiasa wale mema ya nchi.
 
Wataje hao wanasiasa wenye hela kumzidi Bakhresa, Mount Meru, Mo au Lake group,

Sometimes tusidanganyane sana, wanasiasa wana hela ila usiseme ndio wenye hela nying nchini, matajiri hii nchi ni wahindi na waarabu
Watanzania wengi sana wana tatizo la kutoelewa uhalisi kama wewe.

Kuna vijana nawafamu, wao kushika bilioni na kuimaliza ndani ya wiki si mchezo. Hela yao inakuja kutokana na kigogo wa juu serikalini. Anawapa deal za ku supply. Tena basi, wala sio ndugu wa karibu. Huyu kigogo ni kama yuko katika mission ya kusaidia ndugu zake wote wa karibu na mbali katika hiki kipindi ili wawe matajiri.
 
Bila kuwataja na raslimali wanazomiliki itakuwa blah blah.
 
daaaaah
nipe dili mkuu
 
Mkuu, hizo ties za wafanyabiashara na wanasiasa zipo dunia nzima, ukifuatilia huko juu nimetaja mifano,
Ties za wafanya biashara na wanasiasa zinajulikana, na zinafanya wafanya biashara wawe matajiri kwa biashara halali. Hapa tunaongelea wanasiasa matajiri kupita kiasi sio kwa kuwa wanafanya biashara, kwa kuvuta hela ya serikali inayotkana na kodi za wananchi, ku-inflate manunuzi, au kufanya miradi hewa nk. Huyo aliyenunua hekalu la bilioni 25 Dubai unafikiri yeye kazipata hizo hela kwa biashara?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…