Matajiri wakubwa Tanzania si wafanyabiashara bali ni wanasiasa, viongozi wa serikali na ndugu zao, kuonyesha kwamba kuna kitu hakipo sawa

Hahaha
 
🤣Ndio maana unashauriwa uishi vizuri na wakubwa wa nchi. Kuna zile V8 za wana CCM zilizokuwa zimebeba wahamiaji haramu sijui wasomali zikatiwa nyavuni ila kesi ziliishia kwenye matangazo ya habari mule mule.

TRA wanamjua mwenye gari ila kumtaja hawawezi labda mkuu wa kituo amtaje, huku na kule mara mkuu wa kituo anamjua mwenye gari ila hayupo ofisini kwa sasa 😁...

Sasa peleka wewe V8 yako TARAKEA halafu ishikwe ikiwa imebeba wasonjo uone kama jua litazama ukiwa uraiani 😁
 
Nina wasi wasi wale wahamiaji haramu ndio hupachikwa majina ya wasiojulikana.

Haiingii akilini kuna mtanzania wa kuua mtanzania mwenzake.
 
Mkuu huyo achana nae wewe mtu mzima mtu aking'ang'ania sana utaje majina hapo unakua ushaelewa ..
Sasa hvi huo "ushirikiano" ndio hbar ya mjini.
 
Well said Mkuu

Naanza kuhisi huo mfumo umekuwa so strong kiasi kwamba hata raisi akiwa na nia ya kuuvunja anaweza kupata matatizo yeye - kiasi kwamba anakuwa na option moja tu - to join them. Ni lazima kwamba huo mfumo kwa sasa unafanya kazi kama kaji-association, kaji-mafia ka viongozi wa serikali na wale waliokuwa serikalini huko nyuma, na nimesema katika thread nyingine, inawezekana kabisa ndio walio nyuma ya utekaji na uuaji, wakifanya hivyo sio kama serikali, bali kwa kutumia vyombo vya serikali isivyo rasmi. Nasikia hata wana mtandao wao wa WhatsApp.

Ndio maana tetesi kwamba Magufuli alihujumiwa na kuuawa zinakuwa na mshiko, kwamba alijaribu kuuvunja huo mfumo na akazidiwa. Mtandao kama huo kama ni kweli, sioni mtu kama raisi Samia akiwa na uwezo wa kuuvunja. It is too big for her.
 
Sasa hapo mkuu mgawanyo wa faida si unakua 50% kwa 50% au

Na pia hivi ni lazima uwe mfanyabiashara mkubwa au kigezo kip muhim wanaangalia ili wawekeze kwako ili mfaidi keki
 
Mwanasiasa gani tajiri, ana nini?
Huwezi kuwa tajiri ukawa hujulikani
 
Duuh
 
Tuliamua kama taifa siasa ndio iwe kazi ya mapesa mengi kuliko nyingine yeyote ile!

ELewa hivyo!Kila jambo linapangwa!

Dola ndio inaamua nani awe tajiri na nani awe maskini bila kujali viwango vya hustling!

Kuna mstari umechorwa ukiuvuka tu unashughulikiwa!!

RIP Rama wa kariakoo!
 
Nchi nyingi za Kiafrika siasa na biashara ni mifumo tangamani.
Wanasiasa hujificha kwenye biashara na wafanyabiashara hujificha kwenye siasa.
 
Kama wasomali pale kenya!!!

Utajiri umechorwa Kwa ramani ya chuma na damu!tuliamua hao waasia ndio wawe wamatumbi wabaki kama walivyo!
 
Mwanasiasa gani tajiri, ana nini?
Huwezi kuwa tajiri ukawa hujulikani
Unamtabuaje mtu kuwa ni tajiri? Kwamba ana jenga nyumba kubwa, ana magari ishirini ya kifahari nk? Sasa Tanzania kuna matajiri sana assets zao zikiwa Dubai na kwingineko. Watu wana ma-block ya estates huko nje. Na pia unaambiwa umekuwa mtindo kwa viongozi wa serikali sasa kuwa na chumba cha hela kwenye nyumba zao, stacks and stacks of Tshs and US dollars, kwa sababu hawawezi kuziweka benki
 
Na huo ndio utakatishaji pesa wenyewe.

Sio ule wa kufikirika wa kina Kabendera.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…