Matajiri wakubwa Tanzania si wafanyabiashara bali ni wanasiasa, viongozi wa serikali na ndugu zao, kuonyesha kwamba kuna kitu hakipo sawa

Matajiri wakubwa Tanzania si wafanyabiashara bali ni wanasiasa, viongozi wa serikali na ndugu zao, kuonyesha kwamba kuna kitu hakipo sawa

Wazi kabisa 🤣 yani hutoboi!

Yani leo hii hata wewe kama una ujamaa na mtu ambaye ni nguli kwenye system au raia namba 1 ukiwa na ujamaa naye unaweza hata kuanza kusafirisha bange toka tarime ukaleta bongo na utaifanya hio biashara as long as yeye anakupa backup hakuna IGP wala ushuzi wowote wa askari atakaegusa body ya gari iliopakia mzigo wa mmea😁! Ndio maana watu wanaunga mkono juhudi za mboga mboga political party na sifa nyingi kwa raia namba one ili mambo yao yaende.

Ila fanya kimya kimya uone hata kama December itafika kabla hujaingia Segerea!
Hahaha
 
Kuna waziri mmoja wa mojawapo za wizara zetu kapiga hela sawasawa. Rais Samia aliposikia alichofanya ni kumuondoa tu wizara hiyo na kumhamishia wizara nyingine. Japo inajulikana amepiga hela ya serikali kubwa, swali ni kwamba kwa nini raisi Samia hajaamuru Takukuru wamchukulie hatua? Na sio huyo. Kuna mawaziri wengine pia walifanya hivi na wakaondolewa bila kuchukuliwa hatua, kama vile wanapewa nafasi wakale walichopiga
🤣Ndio maana unashauriwa uishi vizuri na wakubwa wa nchi. Kuna zile V8 za wana CCM zilizokuwa zimebeba wahamiaji haramu sijui wasomali zikatiwa nyavuni ila kesi ziliishia kwenye matangazo ya habari mule mule.

TRA wanamjua mwenye gari ila kumtaja hawawezi labda mkuu wa kituo amtaje, huku na kule mara mkuu wa kituo anamjua mwenye gari ila hayupo ofisini kwa sasa 😁...

Sasa peleka wewe V8 yako TARAKEA halafu ishikwe ikiwa imebeba wasonjo uone kama jua litazama ukiwa uraiani 😁
 
🤣Ndio maana unashauriwa uishi vizuri na wakubwa wa nchi. Kuna zile V8 za wana CCM zilizokuwa zimebeba wahamiaji haramu sijui wasomali zikatiwa nyavuni ila kesi ziliishia kwenye matangazo ya habari mule mule.

Sasa peleka wewe V8 yako TARAKEA halafu ishikwe ikiwa imebeba wasonjo uone kama jua litazama ukiwa uraiani 😁
Nina wasi wasi wale wahamiaji haramu ndio hupachikwa majina ya wasiojulikana.

Haiingii akilini kuna mtanzania wa kuua mtanzania mwenzake.
 
Mwaka huu kuna ofisi za stationery ziliagiza sukari ya mabilioni nje. Ofisi hata mtaji wa miliono 10 hazina ila ghafla bin vu zimeagiza tani za sukari kwenye meli. Aliyetoa kibali Wizara ya Kilimo, kwanini hawakupewa vibali wazalishaji wa sukari kama ulivyo utarati u kisheria anayejua ni Wizara.
Beberu utasema hizo stationery zina uwezo wa sukari, utajiri wake hauna siasa.
Mkuu huyo achana nae wewe mtu mzima mtu aking'ang'ania sana utaje majina hapo unakua ushaelewa ..
Sasa hvi huo "ushirikiano" ndio hbar ya mjini.
 
Shida sio wananchi, hakuna ambaye haujui mfumo unavyofanya kazi. Shida ni divide and rule system. Unatengeneza makundi kisha unagawa vyeo kwa viongozi wa hayo makundi na kuwapa VIP treatment as long as wanafanya unavyotaka iwe kisheria au kimabavu. This is what MbogaMboga political party does.

Hakuna mtu atataka ku risk maisha yake ikiwa anajua kabisa mfumo hauko in his favour. Kiongozi wenu wa kikundi hayuko pamoja na nyinyi ila kwa interest za aliyempa uongozi huo, sasa mtaanzaje ku strike katika hali kama hio? Ubinafsi ndio unatumaliza wabongo hivyo. Njaa na Patriotisim havikai sehemu moja.
Well said Mkuu

Naanza kuhisi huo mfumo umekuwa so strong kiasi kwamba hata raisi akiwa na nia ya kuuvunja anaweza kupata matatizo yeye - kiasi kwamba anakuwa na option moja tu - to join them. Ni lazima kwamba huo mfumo kwa sasa unafanya kazi kama kaji-association, kaji-mafia ka viongozi wa serikali na wale waliokuwa serikalini huko nyuma, na nimesema katika thread nyingine, inawezekana kabisa ndio walio nyuma ya utekaji na uuaji, wakifanya hivyo sio kama serikali, bali kwa kutumia vyombo vya serikali isivyo rasmi. Nasikia hata wana mtandao wao wa WhatsApp.

Ndio maana tetesi kwamba Magufuli alihujumiwa na kuuawa zinakuwa na mshiko, kwamba alijaribu kuuvunja huo mfumo na akazidiwa. Mtandao kama huo kama ni kweli, sioni mtu kama raisi Samia akiwa na uwezo wa kuuvunja. It is too big for her.
 
Huu ndio ukweli ambao wabongo wengi hatuujui. Kuna siku Fredy Vunja bei aliropoka jambo nikaona kumbe hata yeye anafahamu hilo. Unaweza ukawa meneja mzuri wa biashara yako ndogo na kasi ya ukuaji ikavutia watu wengine kuwekeza pesa zao kwako. Sio lazma uwe na mtaji mkubwa wa kufanya kila kitu mwenyewe.

Hiki ndicho wanasiasa wanafanya sababu anakuwa na pool ya hela ndefu. Akipiga dili lake moja ana stake in billions. Hizo fedha ili asishtukiwe lazima aziingize kwenye biashara ya mtu au afiche nje. Sasa unamuaminije mtu with billions of money?

Ndio maana wanatafutaga wafanya biashara wakubwa na kutaka kuingiza mitaji kwao kisha wanakula migao ya faida. Bahati nzuri watu waaminifu ni wenye asili ya kihindi na kiarabu.
Sasa hapo mkuu mgawanyo wa faida si unakua 50% kwa 50% au

Na pia hivi ni lazima uwe mfanyabiashara mkubwa au kigezo kip muhim wanaangalia ili wawekeze kwako ili mfaidi keki
 
Ni kawaida kwamba katika nchi nyingi matajiri wakubwa utakuta ni wafanya biashara, lakini sio Tanzania. Kwa sasa wanaoongoza kwa kuwa matajiri wakubwa Tanzania ni wanasiasa waliopo madarakani au waliokuwa madarakani huko nyuma. Halafu wanafuatiwa na viongozi wa serikali, pamoja na ndugu zao.

Imefikia kwamba hata ukiwa mfanya biashara, ili utajirike kwa haraka lazima uwe na connection na wanasiasa na viongozi wa serikali, kuanzia connection za ofisi ya raisi, makamu wake au mawaziri. Hata vjana wadogo kabisa wenye hizi connections sasa wanaibukia kuwa na fedha nyingi sana za kufuja na kuishi maisha ya anasa sana.

Inatokea pia kwamba kikundi hiki cha matajiri wa kisiasa uongozi wanalinda sana himaya yao, mara nyingi kwa kutumia vyombo vya dola kama polisi, na sasa hata wanajaribu kutumia jeshi la ulinzi, JW. Hawataki watu wengine wa "kawaida" wawe kama wao. Kwa hiyo wanajaribu kuendeleza umiliki wa himaya zao kwa kuwekeza katika watoto wao ili kuja kuwarithisha kuwa "wenye nchi" pamoja na utajiri wao. Hii ni kutia ndani kuendelea kufanya ufisadi mkubwa ili hata vizazi vyao vya baade viendelee kuwa katika neema ya kuwa tofauti na Watanzania wa kawaida.

Wengi wasichojua ni kwamba tatizo kubwa la serikali kukataa uraia pacha sio suala la "usalama wa nchi", bali ni usalama wa hiki kikundi kuona Watanzania walioko nje wana uhuru wa mawazo na upeo wa kuona wanachokifanya. Ndio maana hawataki watu wa diaspora wapewe nafasi ya kuja kuwa tishio kwa himaya yao. Wanawaogopa sana watu wa diaspora na wanaona kuwapa uraia pacha ni kuleta hatari ya kuondolewa katika "ufalme wao". Hawa "wenye nchi" wanajua watu wa diaspora hawana "political illiteracy" ambayo wameijenga katika Watanzania wanaoishi nchini. Wanadiaspora wana macho na wanaona, na wanaogopwa.

Lakini nataka nitoe tahadhari kwa watu hawa, kwamba katika jamii yoyote ile, hali kama hii iliyopo Tanzania huwa haidumu. Kuna wakati itafikia critical point, na kutakuwa na mlipuko mkubwa ambao ni namna fulani ya mapinduzi, ili kuliondoa tabaka hili la "wenye nchi" katika hii himaya yao ambayo kwa sasa wanaifurahia sana na kujaribu kuilinda kwa kila namna. Hili ndilo lililotokea nchi kama Tunisia na Misri, na si muda mrefu litatokea Tanzania, hali ikiendelea hivi.
Mwanasiasa gani tajiri, ana nini?
Huwezi kuwa tajiri ukawa hujulikani
 
Well said Mkuu

Naanza kuhisi huo mfumo umekuwa so strong kiasi kwamba hata raisi akiwa na nia ya kuuvunja anaweza kupata matatizo yeye - kiasi kwamba anakuwa na option moja tu - to join them. Ni lazima kwamba huo mfumo kwa sasa unafanya kazi kama kaji-association, kaji-mafia ka viongozi wa serikali na wale waliokuwa serikalini huko nyuma, na nimesema katika thread nyingine, inawezekana kabisa ndio walio nyuma ya utekaji na uuaji, wakifanya hivyo sio kama serikali, bali kwa kutumia vyombo vya serikali isivyo rasmi. Naikia hata wana mtandao wao wa WhatsApp.

Ndio maana tetesi kwamba Magufuli alihujumiwa na kuuawa zinakuwa na mshiko, kwamba alijaribu kuuvunja huo mfumo na akazidiwa. Mtandao kama huo kama ni kweli, sioni mtu kama raisi Samia akiwa na uwezo wa kuuvunja. It is too big for her.
Duuh
 
Tuliamua kama taifa siasa ndio iwe kazi ya mapesa mengi kuliko nyingine yeyote ile!

ELewa hivyo!Kila jambo linapangwa!

Dola ndio inaamua nani awe tajiri na nani awe maskini bila kujali viwango vya hustling!

Kuna mstari umechorwa ukiuvuka tu unashughulikiwa!!

RIP Rama wa kariakoo!
 
Nchi nyingi za Kiafrika siasa na biashara ni mifumo tangamani.
Wanasiasa hujificha kwenye biashara na wafanyabiashara hujificha kwenye siasa.
 
Huu ndio ukweli ambao wabongo wengi hatuujui. Kuna siku Fredy Vunja bei aliropoka jambo nikaona kumbe hata yeye anafahamu hilo. Unaweza ukawa meneja mzuri wa biashara yako ndogo na kasi ya ukuaji ikavutia watu wengine kuwekeza pesa zao kwako. Sio lazma uwe na mtaji mkubwa wa kufanya kila kitu mwenyewe.

Hiki ndicho wanasiasa wanafanya sababu anakuwa na pool ya hela ndefu. Akipiga dili lake moja ana stake in billions. Hizo fedha ili asishtukiwe lazima aziingize kwenye biashara ya mtu au afiche nje. Sasa unamuaminije mtu with billions of money?

Ndio maana wanatafutaga wafanya biashara wakubwa na kutaka kuingiza mitaji kwao kisha wanakula migao ya faida. Bahati nzuri watu waaminifu ni wenye asili ya kihindi na kiarabu.
Kama wasomali pale kenya!!!

Utajiri umechorwa Kwa ramani ya chuma na damu!tuliamua hao waasia ndio wawe wamatumbi wabaki kama walivyo!
 
Mwanasiasa gani tajiri, ana nini?
Huwezi kuwa tajiri ukawa hujulikani
Unamtabuaje mtu kuwa ni tajiri? Kwamba ana jenga nyumba kubwa, ana magari ishirini ya kifahari nk? Sasa Tanzania kuna matajiri sana assets zao zikiwa Dubai na kwingineko. Watu wana ma-block ya estates huko nje. Na pia unaambiwa umekuwa mtindo kwa viongozi wa serikali sasa kuwa na chumba cha hela kwenye nyumba zao, stacks and stacks of Tshs and US dollars, kwa sababu hawawezi kuziweka benki
 
Huu ndio ukweli ambao wabongo wengi hatuujui. Kuna siku Fredy Vunja bei aliropoka jambo nikaona kumbe hata yeye anafahamu hilo. Unaweza ukawa meneja mzuri wa biashara yako ndogo na kasi ya ukuaji ikavutia watu wengine kuwekeza pesa zao kwako. Sio lazma uwe na mtaji mkubwa wa kufanya kila kitu mwenyewe.

Hiki ndicho wanasiasa wanafanya sababu anakuwa na pool ya hela ndefu. Akipiga dili lake moja ana stake in billions. Hizo fedha ili asishtukiwe lazima aziingize kwenye biashara ya mtu au afiche nje. Sasa unamuaminije mtu with billions of money?

Ndio maana wanatafutaga wafanya biashara wakubwa na kutaka kuingiza mitaji kwao kisha wanakula migao ya faida. Bahati nzuri watu waaminifu ni wenye asili ya kihindi na kiarabu.
Na huo ndio utakatishaji pesa wenyewe.

Sio ule wa kufikirika wa kina Kabendera.
 
Back
Top Bottom