matamshi kiinglish tunayakosea kwa kurithishana

matamshi kiinglish tunayakosea kwa kurithishana

Swahilized German..pia matamshi yanakaribiana!!




ha ha..kumbee eeh! mfano skuli ya mjimkongwe!!

teh teh teh,au skuli ya jang'ombe,sa mi huwa najiuliza mno,hawa wenzetu kiswahili cha skuli hawakijui auu
 
Mimi English Jamaica huwa napata shida sana kuelewa kama Alivyokuwa Akiongea Bob Marley ni likuwa nabaki nashangaa anaongea nini! ukija kwa Shaba Ranks akiimba naambulia maneno Machache je wao wamejifunzaje Lugha hiikwani njuavyo kule hawana makabila yaliyoathiri lafudhi zao...

Kitu nipendacho ile lafudhi ya African Amerian yaani Tamu balaa haswa akiongea Smookey au Chris Tucker... Utasikia Hell Nooo Daaaaaaaaamn.... Ger ou hia...(Get out here)
 
neno question - tunatamka kweshen badala ya kwes'chen
'' consumer - '' konshuma
badala ya konsyuma
'' producer - '' prodyuza badala ya prodyusa
'' assume - '' ashum
badala ya asum au asyum
'' every - '' evere " evri

hayo ni maneno machache katika mengi ambayo nimeshuhudia yakiendelea kukosewa siku hadi siku hadi na walimu wa lugha husika.Mimi nilikua mmoja wa waathirika tokana na aina ya shule nilizosoma ,japo namshukuru Mungu baada ya kufika A level nilisoma Kiingereza katika Combination yangu na kusoma topic ya phonology inayohusisha matamshi ya lugha na kanuni zake ndipo nikagundua nilipokua nakosea na wengine wengi wamekua wakikosea.

Mwenye uelewa wa maneno mengine ya english ambayo ameyasikia yakikosewa na wa Tz ni vyema ayaweke ili tuboreshe lugha kidogo kimatamshi angalau.

Mkuu pamoja na elimu uliyotoa ningependa kukueleza tu japo kwa kifupi kuwa Transcription ya maneno na pronounciation yake huweza kutofautiana kutokana na mazingira ya kifonolojia, na ndio maana kuna dictionary transcription na actual prounciation kama ilivyozoeleka na watumiaji wa lugha husika, laiti kama tungekuwa tunatamka kila neno exactly kama ambavyo inapaswa kutamkwa individually basi tambua kuwa zaidi ya 90 percent ya maneno ya kiingereza tunayatamka sivyo, pitia vitu kama Assimilation, Liason na ellision in language uone nini kinasababisha
 
A bus stops and two Italian men get on. They sit down and engage in an animated conversation. The lady sitting behind them ignores them at first, but her attention is galvanized when she hears one of the men say the following:
"Emma come first. Den I come. Den two asses come together. I come once-a-more. Two asses, they come together again. I come again and pee twice. Then I come one lasta time."
"You foul-mouthed sex obsessed swine," retorted the lady indignantly.
"In this country ... we don't speak aloud in public places about our sex lives ...
"Hey, coola down lady," said the man. "Who talkin' abouta sexa? I'm a justa tellin' my frienda how to spella 'Mississippi'."
Siyo sisi tu tunaokosea,na hawa je?
 
Birthday ni neno linalokosewa sana Tanzania. Wabongo hulitamka "bathdei".

Hiyo "a" haipo kwenye matamshi sahihi. Sasa sijui watu huwa wanaitoa wapi tu!

Neno birthday linatamkwa na irabu ambayo ni intermediate kati ya "a" na "e" . Hiyo irabu hatuna katika lugha yetu ya kiswahili. Kumbuka kuwa katika kiswahili tuna Irabu tano tu na katika kiingereza kuna Irabu ishirini ikiwemo hiyo /3/ inayotumika katika neno birthday, kutokana na mazoea yetu ya zile irabu tano tunajikuta tunatamka kwa kutumia aidha "a" au "e"
 
leo hii mbongo ushuke LIVERPOOL toka tanzania,hata uwe prof wa english bongo,hauwezi sikia neno-it will take u a couple of days kuwaelewa hawa jamaa

Ndio maana Rooney alisema huwa anapata sana shida kumuelewa Carragher akiwa anaongea.
 
Skuli watu wengi tunaitumia vibaya badala ya school (mambo ya swanglish hayo).

kiswahili chake ni shule mkuu.

Shule tumetohoa kutoka kijerumani/kidachi kijerumani na skuli tumetohoa kutoka kiingereza kama tulivyo kopa penseli(english)kitabu(arabic) kalamu(arabic).
Kwa hiyo skuli ,shule si makosa kuyatumia.
 
leo hii mbongo ushuke LIVERPOOL toka tanzania,hata uwe prof wa english bongo,hauwezi sikia neno-it will take u a couple of days kuwaelewa hawa jamaa
Na wewe mwite profesa wa kiswahili hapa bongo aje makunduchi asikie kiswahili cha kimakunduchi kama hata toka jasho la masikio!
mfano:muda fulani JK alitembelea pande za makunduchi-zanzibar wananchi wale wakawa wanampokea kwa makofu huku wakisema "kikwete kanavitako!"wanamaanisha kikwete anapita!sipati picha mkuu alijiulizaje kuhusu "vitako vyake"
 
Kwa mashabiki wenzangu wa mpira,,, neno possesion lina tofauti kubwa na position!! Ila ki boli boli mnaweza shikana mashati,Ee bwana eeh!tatizo ni boli position bwana,ukimwambia amekosea 90% wanakushangaa.

Matamshi sahihi ya possession ni pozeshen
 
Graduation wengi husema Gra-de-she-ni badala ya Gra-dyu-e-shen.
 
Pia neno New Castle, watu hutamka 'New kestlo', matamshi sahihi ni 'Nyu kesol'
Acha Noma hiyo ni kwa Uk tu South Africa kwenye super sport tunawasikia wakitamka kwa herufi zote Kestlo Laga sijawahi sikia wakisema Kesol Laga....

Hata EPL TV mimi husikia Nyu kestlo yunaited... Labda huifinya st isisikike
 
Mi sishangai kwa sababu lugha inabadilika kimsamiati na hata kimatamshi pia baadhi ya hayo maneno yanakosewa kutamkwa kwa sababu ya athari za lugha zingine(lugha mama)
 
Acha Noma hiyo ni kwa Uk tu South Africa kwenye super sport tunawasikia wakitamka kwa herufi zote Kestlo Laga sijawahi sikia wakisema Kesol Laga....

Hata EPL TV mimi husikia Nyu kestlo yunaited... Labda huifinya st isisikike
Umewasikia watangazajii si wasanifu wa lugha,kwani hapa akija mgeni aliyejifunza kiswahili haalafu asome magazeti yetu na kusikiliza vipindi vya radio zetu aje ku top up na tv presenters wetu, si atatokwa mkojo kwa huo uovyo wa lugha ya kiswahili!
 
Acha Noma hiyo ni kwa Uk tu South Africa kwenye super sport tunawasikia wakitamka kwa herufi zote Kestlo Laga sijawahi sikia wakisema Kesol Laga....

Hata EPL TV mimi husikia Nyu kestlo yunaited... Labda huifinya st isisikike
naamini haujasikiliza kwa makini
 
Back
Top Bottom