Matangazo ya Cocacola kwenye TV

Kuna Link niliweka nadhani ukisoma itakusaidia zaidi.
 
Ndugu, mtu yoyote wa Masoko anaielewa nguvu ya watoto kwenye manunuzi huu ni utafiti kwa America, Japan, Ujerumani na China.


Marketing to Children

Children as Consumers — Global Issues
 
Ndugu, mtu yoyote wa Masoko anaielewa nguvu ya watoto kwenye manunuzi huu ni utafiti kwa America, Japan, Ujerumani na China.


Marketing to Children
Kaka, ndiyo maana nimekwambia unalitazama hilo jambo kwa jicho la kiurahisi sana. Hivi tamaduni za kitanzania katika malezi na makuzi zinafanana na hizo nchi ulizozitaja? Huwezi kufanya generalisation kwa kutumia utafiti kutoka nchi nyingine zenye tamaduni tofauti kabisa. Katika familia za kitanzania, mtoto hawezi kuwa na influence katika maamuzi ya nini kinunuliwe. Naweza kukuelewa kidogo ukisema pengine familia za wale waishio kama wazungu (ingawa sipo confident katika hili). Lakini watanzania waishio kama watanzania, bado sikubaliani nawe.
 
Hahahaha we jamaa sisi hatuna kawaida ya kuweka hadharani tafiti zetu ingawa makampuni yanafanya Na Nakuhakikishia Nguvu ya watoto katika manunuzi hata hapa ni kubwa sana.

Makundi mengine ni Wanawake/Wasichana/ Wavulana/ ( Vijana )

Asilimia kubwa ya Wababa wanafuata mkumbo wa hayo makundi.

Na eneo zuri kutarget Uswazi Dar na Mikoani.
 
Kwanza unapaswa kujua kuwa Cocacola ni bidhaa ya wamarekani, popote duniani inapo zalishwa inapaswa kufuata mbinu za kushinda soko km anavyo elekeza mwenyewe mwenye bidhaa yake ambae ni mmarekani, hiyo ni kusema matangazo yao lazima ya ni ya ubora wa hali ya juu, tena mengi huwa yana andaliwa hukohuko kwao na lazima yarushwe sana katika media ili kushinda soko, hiyo ndio sera ya mwenye bidhaa yake, na ukishindwa kufanya hivyo unanyang'anya ruhusa ya kuzalisha bidhaa yao
 
Asante wajina
 
Pepsi nao ni wamarekani, nadhani kutokea Atlanta. Unajua hilo?
 
Pepsi nao ni wamarekani, nadhani kutokea Atlanta. Unajua hilo?
Nisaidieni zamani tulikuwa tunasema kirefu cha COCA ni come one, come all, sasa COLA yenyewe ni nini? Sikumbuki, mwenye kukumbuka tafadhali msaada!
 
Kwanini uwape watoto Soda hio?? Watoto yao Juice, hayo mavinywaji kunywa wewe mzee. Ndio maana afya zetu zinayumba miaka hii, mtoto ana miaka mitano alishakunywa coca kama lita 20 hivi?? Why??
Tatizo si coke bali jinsi tangazo lilivyo huo mchezo hata wakiufanya wakati wanakunywa maji ni hatari pia, tatizo ni kimiminika mkuu.
 
Cocacola siku zote wanatangaza sana

kabla hata ya bakhresa kuja

na hakuna anaejua nani ana lead kwa mauzo
Vipi kuhusu Vodacom? hawa ndio nawashangaa zaidi, maana wanawekeza kwenye matangazo halafu gharama za vifurushi wanapandisha, watu wanawakimbia kwa sababu ya gharama zao na sio kutokujitangaza, maana sijui kama kuna mtumiaji wa simu asiyejua kuna vodacom hapa tz
 

Voda ni mtandao wa kuaminika kwa mikoani na internet ndo maana
wana jeuri ya kupandisha gharama
 
Kosa - marangazo
Sahihi - matangazo

Kosa - curious
Sahihi - serious
Lugha husika - makini badala ya neno "serious "


Napita tu.......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…