Matangazo ya Cocacola kwenye TV

Matangazo ya Cocacola kwenye TV

Hii ndio naona imeimbwa kwa lugha nyingi. Mpaka dai, fally ipupa nao wameimba
Campaign zao huwa ni mabara kwa mabara.... Wakichagua Theme Song ya mwaka husika inarudiwa kwa Lugha inayopendelewa katika masoko yote wanayoyalenga.

Dai walimtumia kwa kuwalenga Wanaosikia Kiswahili ( East African Market ) na Fally wanaosikia Lingala/French ( Central African Market )
 
Hivi kwanni bakhresa asianze kutengeneza Supu ya pweza. Maana nahisi angepata faida koz nw days watu wanainywa sana
 
Mimi lile tangazo lao la watoto wananyang'anyana coke halafu yule mwingine anaibetua wakati mwenzake anakunywa silipendi kwelikweli, linaniogopesha sana maana watoto wanaweza kuiga halafu ikawa majanga soda ikipita mahali pasipo husika mwilini..yaani ni vile sina uwezo wa ku li edit tu.
Hilo Tangazo ili ulipende unatakiwa ukielewe kisa mwanzo mwisho, kaka anamjambisha sana mdogo ake wakiwa nyumbani lakini pale mdogo ake anapo onewa huko kitaa kaka anatokea na kumsaidia, huku kama nae anataka kunywa soda yake wakati dogo anakiu balaa..tunashuhudia upendo wa kaka kwa mdogo wake na dogo haamini kama kaka ake angeweza msaidia na kumpatia soda yake kwa kile anachofanyiwa nyumbani
 
Hilo Tangazo ili ulipende unatakiwa ukielewe kisa mwanzo mwisho, kaka anamjambisha sana mdogo ake wakiwa nyumbani lakini pale mdogo ake anapo onewa huko kitaa kaka anatokea na kumsaidia, huku kama nae anataka kunywa soda yake wakati dogo anakiu balaa..tunashuhudia upendo wa kaka kwa mdogo wake na dogo haamini kama kaka ake angeweza msaidia na kumpatia soda yake kwa kile anachofanyiwa nyumbani

kuna mdau mmoja humu aliwahi kueleza matumizi ya rangi
rangi nyekundu ndo inatawala
na wale waliokimbizwa walivaa blue ...kama coca ikiwepo pepsi anakimbia
au hasemi kitu
 
Mi cpendi yule kijana mdogo anavyonyanyaswa na kaka yake!
Anamkomaza, dogo achangamke ndio maana anakuwa anaonewa skuli, but ingawa kaka anamuonea dogo ake tunauona msaada wake pale anapopokwa coca huku dogo anakiu
Kwanini uwape watoto Soda hio?? Watoto yao Juice, hayo mavinywaji kunywa wewe mzee. Ndio maana afya zetu zinayumba miaka hii, mtoto ana miaka mitano alishakunywa coca kama lita 20 hivi?? Why??
 
Hakuna tangazo linanivutia kama hilo la Cocacola.
Limekaa poa sana.
 
Lakini pia wanawalenga watoto kwasababu ya Ushawishi mkubwa waliokuwa nao ndani ya familia.

Kitu kikipendwa na watoto nyumbani wazazi mnajikuta tu na nyinyi humohumo [emoji23] watu wenye akili zao wanajua kuutumia udhaifu huo vizuri.

Hayo ndiyo yalinifanya niandike haya:

Ulivyoelezea ni as if watoto wana-influence maamuzi ya familia! Hili jambo siyo kweli kabisa! Kwani mzazi hawezi kumwambia mtoto kwamba hawezi kukubali kila jambo ambalo mtoto anaomba? Ilmradi mtoto aambiwe kwanini jambo haliwezekani, hakuna shida. Kama unaendesha familia kwa staili ya kukubali kila jambo ambalo mtoto analitaka, ni hatari sana kwa maisha ya baadaye ya mtoto wako.

Sasa sijui nini hapo sijaelewa! Mimi ninapinga hilo la kusema watoto wana ushawishi mkubwa kwenye familia. Ni dhana uliyoiweka katika mtazamo mrahisi sana, bila kuzingatia mambo kama uchumi wa familia, aina ya malezi na makuzi n.k. Otherwise, prove hicho unachokisema kwa kuleta hapa utafiti unaonyesha watoto wana ushawishi mkubwa kwenye manunuzi ya soft drinks kwenye familia.
 
Back
Top Bottom