Matapeli wa kisiasa waliopoteza chanzo cha mapato wanatafuta msaada kwenye tuta

Matapeli wa kisiasa waliopoteza chanzo cha mapato wanatafuta msaada kwenye tuta

Nashauri ARV nazo zisitolewe bure ili tuzinunue ghali kama yalivyo madawa ya Cancer!
Mbinyo uwe mkali mpaka kila mwananchi ausikie umegonga mfupa!Pengine tutakumbuka kutenda haki!
Unatamani upewe ARV, una ngoma nini???
 
Kama EU wanataka hiyo 27m Euro yao ya Corona warudishiwe tu, hela za masimango hazina faida. Waendelee na mishe zao watuache na nchi yetu. Misaada ya EU ni kwenye 100m Euro kwa mwaka ( 600m kwa miaka 6 ), makampuni yao makubwa yapewe nchini hasa hasa kwenye mining wapigwe tu unfair tax invoice pesa hiyo ije kwetu kwa njia nyingine.
Hakuna kurudisha hela hapo! Lazima tuheshimiane tu. Warejee kwenye mkataba nao jamaa vigeugeu. Walisema Tanzania kuna korona, tungekufa kama kuku, ndipo tukajipanga kama mchwa. Halafu hata hiyo hela yao haijatosha.
 
Nashauri ARV nazo zisitolewe bure ili tuzinunue ghali kama yalivyo madawa ya Cancer!
Mbinyo uwe mkali mpaka kila mwananchi ausikie umegonga mfupa!Pengine tutakumbuka kutenda haki!
Hawa dawa yao dude linalokuja huko kutoka ICC na vikwazo kabambe. We waache tu wajitoe ufahamu. Ila wajue tu Safari hii wazungu lazima wawanyooshe kisawasawa
 
Mimi hupenda kutoa mfano wa upinzani kwetu Kilimanjaro:

Karibu asilimia 90 ya wazee Kilimanjaro yaani mama zetu na baba zetu wako CCM na karibu vijana 70% wapo upinzani.

Hawa wazee tunaishi nao, tunapokea maelekezo yao, tunawapatia mahitaji yao, tunahakikisha mwisho wa mwaka tuna watembelea na tunawaachia kitu mkononi na kupata baraka zao. Kama tunaweza kuishi nao wazee wetu tunashindwaje kuishi na wanaCCM wengine. Au kwa kuwa sio wazazi wetu?

Yaliyotokea yametukwaza sana lakini wazee wetu hutufukuza tukifikia umri wa kutafuta mbona tunarudi kuwapelekea chochote na tuna jivunia wazee wetu.

Jee wanachama wa CCM ambao wengine huchanganyika na wazee wetu kwa nini tuwaone ni taabu?.

Tubadilike, Uchaguzi upo na utapita lakini maisha yata endelea.
Uchaguzi kuisha ndio kwamba mateso kwa wapinzani yameisha?Akina Nusrat Henje wako mahabusu bila dhamana zaidi ya miezi minne sasa!Kosa ni kuimba "Mungu ibariki Chadema...",wakati huo huo CCM walioimba Mungu mmbariki Magufuli maisha yanaendelea kama kawaida!
Halafu unakuja kuniambia tuwe wamoja,shwain niwe na umoja na watu ambao wanatesa ndugu na rafiki zangu!
Mimi naunga mkono tuwekewe vikwazo mpaka tuishi kwa taabu sana,ilimradi mateso hayo tutapata wote!
Mgombea anakamatwa na Polisi kwa kuandamana halafu anajitetea "msininyanyase kwani mimi sio mpinzani bali ni mwana CCM",hadi wenyewe mnajua wanaopaswa kunyanyaswa ni upinzani!
Sina huo moyo,majanga yanyoikumba hii serikali basi kwangu mimi ni furaha!Iko hivyo,tutakapopata serikali inayotenda haki kwa wote,nitaiunga mkono!
 
Kwa hiyo tuharibu nchi yetu kwa kuwa tunao waunga mkono wamepigwa chini Ubunge? Udiwani?.

Urais wote tulikuwa tunajua Magufuli atashinda. Ukinyimwa ugali na mama unavunja vyombo vyote nyumbani ?.

HII NCHI NI MAMA YETU.
 
Nashauri ARV nazo zisitolewe bure ili tuzinunue ghali kama yalivyo madawa ya Cancer!
Mbinyo uwe mkali mpaka kila mwananchi ausikie umegonga mfupa!Pengine tutakumbuka kutenda haki!

Hata wabinye na korodani kabisa watz hawatobadilka.Kila mtu yupo na hamsini zake
 
Tunajua fika Chadema na Act wazalendo ni vyama ambavyo kwa ushahidi wa wazi kabisa ambao hauna chembe kuwa ni vyama vya wasaka matonge. Wao kuweka pesa mfukoni ndio lilikuwa jambo la kwanza kuliko maslahi ya Tanzania na raia wake.

Tulishuhudia Zitto Kabwe akizurula Ulaya na Usa na kunadi kuwa hakuna demokrasia nchini,na hata haki ya watoto wa kike kusoma wakiwa na mimba inaminywa,akaandika barua tunyimwe mkopo. Hakuwa na muda wa kutumikia wananchi wa Kigoma, muda wote alikuwa anazurula nje ya nchi kusaka ufadhili wa mabeberu ili ajinufaishe kwa madai ya kutetea demokrasia kama vile Tanzania hakuna Demokrasia.

Chadema wao ndio wananchi walisha wachoka na siasa zao za kishamba za harakati zisizo na mashiko, kudai maandamano, kuvamia magereza, kupinga maendeleo ya wananchi huku nao wanayafaidi, wananchi waliwachoka hata kabla ya kupiga kura. Na kwenye boksi la kura wamepata wanacho stahili.

Act wazalendo na Chadema walizoea kupata ruzuku na michango ya wananchi bure kabisa, sasa kimoja kimekufa mende style hakuna ruzuku ya mil 360, hakuna michango ya wabunge zaidi ya mil 100 kwa mwezi.

Kilichobaki wanasaka msaada kwenye tuta, Eu iinyime misaada Tanzania ili wao wafurahi! Watanufaika nini? Tril 2 ambazo ni msaada wa EU kwa Tanzania mimi naona ni kitu kidogo sana kwa nchi ambayo inakusanya tril 1.5 kwa mwezi, achana na mapato mengine.

Watanzania tunajua siasa ni mtaji wenu, mlikuwa mnakula kwa kupitia vyama vyenu sasa wananchi wamewakataa, kuomba dua mbaya kwa Tanzania ni kupoteza muda.
Angalia wazalendo wa nchi hawa wabunge wa ccm wanalia lia
 
Back
Top Bottom