Hizo changamoto ulizotaja huenda zikawa kwenye injini tofauti tofauti za Toyota. Ninatumia gari yenye injini ya 1ZZ-FE (1794cc), hizo changamoto zote nimekutana nazo.
Ilikuja imetembea roughly 160,000km, hapa nimeitumia miaka 5 kasoro miezi 2, changamoto za kula oil nilikutana nayo, bahati mbaya it was worse, hivyo overhaul ilifanyika. Tukabadili oil seals, piston rings na cones. Imeacha kula oil. Oil ilikuwa inavuja inaingia kwenye throttle body.
Nilibadili idle control valve, engine mounts pia baada ya kuwa na mtikisiko mkubwa wa injini hadi ndani unauhisi.
Hivi karibuni nimebadili fuel pump baada ya gari kuwa inakosa nguvu pale ninapopanda kilima au ninapobeba mzigo na watu.
Kwa mujibu wa mtandao fulani, injini nyingi za Toyota, life span ni 200,000km. Ikigonga hapo, changamoto kama hizo zinakuwa za kawaida. Muhimu kuzifanyia kazi na maisha kuendelea.