Baada ya kuibiwa Sana na mafundi, kupoteza fedha nyingi, na kusoma thread nyingi kuhusu Toyota IST, namshukuru Mungu, nimepata fundi wa uhakika anayejua nini ni nini Yani nini kimesababishwa na nini, na nini afanye ili Kuondoa tatizo, Baada ya kumpelekea gari akaiendesha kwanza, alivyoshuka aliniambia matatizo ya ile gari yote kabla hata Mimi sijamuambia. Nikashangaa. Alinijibu kitaalamu tatizo la gari Kukosa nguvu uwashapo A/C, alinijibu kitaalamu tatizo la gari Kukosa nguvu bila hata kuwasha A/C, alinijibu kitaalamu tatizo la gari kuanza kula mafuta, tatizo la gari kutochanganya speed, kanirekebishia gari vyote Sasa gari imerudi mpya, ingawa ni IST hapo mwanzo ilikuwa inakula 1litre kwa kilometer 10, Sasa inaenda 1litre kilometer 17, na ni Cc 1500, wale walikuwa wanasema sababu ni four wheel Drive automatic, ndo Mana gari haichangani speed haina nguvu si kweli, aisee Kuna vitu vingi Sana hatuvijui kuhusu magari, mafundi wengi sababu hawajui kutengeneza watakuambia hiki kimekufa nunua kipya, kumbe kinarekebishika, akishindwa kabisa atakuambia tubadili kitu flani kumbe ni kizima, na nimegundua watu wengi Sana wameuza magari yao angali ni mazima sababu ya hawa mafundi feki wasiojua Nini wanafanya, Mimi niliambiwa nibadili Exhaust imekufa na ni laki 5 na nusu ili kurekebisha mlio mkubwa kwenye sauti kumbe ni nzima, namshukuru Mungu nilishituka mapema sikufanya hivyo, huyu fundi ndo akanifungua akaniuliza mlio mkubwa wa gari unausikia mbele au nyuma, nikamwambia mbele, akaniambia siyo Exhaust utaibiwa, Yani gari imerudi mpya kabisa nilikuwa niiuze Lakini sasa siuzi Tena. Kutokujua magari nako kumegarimu, Tatizo la A/C Kukosa nguvu hasa mchana amelirekebisha, vitu vingi mafundi wa mwanzo waliniambia havifai yeye karekebisha. Ukipata fundi wa uhakika, na spare original huna haja ya kuuza gari Kama hujalichoka. Nimeibiwa sana na kuliwa fedha zangu nyingi mno, namshukuru Mungu. Huyu fundi wa uhakika Hana tamaa. Kuna mafundi wengine ukitengeneza gari Baada ya mwezi lazima lisumbue tena. Nimegundua mafundi wengi wanaenda kwa mazoea tuu hawazijui gari vizuri, kwa iyo huwa hawaondoi tatizo, Kinachouwa IST nyingi nimejifunza plug feki, oil feki ya gia box, na oil feki, Kama si feki basi si recommend kwa ajili ya Toyota IST na Mimi nilikuwa nabadilishia kwenye sheli kubwa, fundi akaniambia hii oil ni oil ila kwa Toyota IST ni kubwa ingekuja kuuwa engine, hii inatakiwa kwenye Toyota Harrier, alfu ndo wengi tunawekewa kwenye masheli haya, nikasema ndo mana engine zinawahi kufa aisee daah hawa mafundi hawa, na Hawa wanaotubadilishia oil wakitushauri sababu ya ugeni au kutokujua wametuulia Sana magari yetu, Kama umesumbuka kama Mimi na una IST au toyota yenye matatizo Kama hayo hapo juu, Natoa namba ya huyu fundi aliyenisaidia mimi na kunifungua macho na kunishauri 0684516017 -fundi Reginald, ili usije ukapata hasara Kama mimi, inawezekana nawe hulijui gari vizuri Kama mimi huyu atakusaidia, usiize gari Kama bado unaipenda uyu jamaa ni kichwa mtaalamu hasa habatishi kazi yake atakusaidia mcheki.