The Tomorrow People , na wadau wote katika uzi huu.
Toyota IST ncp61 (odometer 129,000KM hadi sasa) ina matatizo yafuatayo:
1. Mlio wa kugonga hivi kwenye engene (knocking sound... koh koh koh koh koh). Mlio huu husikika baada ya engene jupata joto. Yaani unapowasha on the start mlio huo haupo, ila baada ya muda fulani at idle au gari ikishatembea engene ikapata joto ndipo huu mlio huanza kusikika. Mlio huu ni kama nilianza kuunotice baada ya kuanza kuweka 'petrol treatment' kwenye fuel (japo sina hakika sana kuhusu hili). Mlio huu una zaidi ya miezi saba sasa tangu uanze. Usikilize hapa...(audio)
View attachment 1874371
2. Hivi karibuni, mwezi mmoja uliopita, nimegundua engene oil imeanza kupungua kwa kiwango kidogo.
3. Coolant huwa inapungua pia kwa kiwango kidogo. Kwa mwaka mzima nimetumia LITA MOJA ya coolant kwaajili ya kuongezea 'full level' from time to time.
N.B: Nazingatia service kwa wakati (kila kilomita 5,000 nabadilisha engene oil). Natumia oil ya TOTAL 5W-30 (Quartz 9000 full synthetic). ATF natumia TYPE T-IV as recommended kwenye dipstick. Gari ina power vizuri kwenye mwendo. Engene haijaguswa, ni kubadili plugs tu from time to time, nawekaga DENSO Iridium (genuine plugs).
Wakuu naombeni msaada wenu wa mawazo na kitaalamu nitatue matatizo hayo matatu tajwa hapo juu.