Matatizo ya Engine za Toyota IST na suluhisho lake

Asante sana mkuu kwa taarifa hio. Swala tu, hio timing chain ipi nzuri?
 

Kwa Tanzania Model ya magari yaliyo mengi kwa mujibu wa utafiti mdogo niliofanya ni IST ,yakipita magari 10 basi manne IST.
 
Kuna ist iko bandarini alieiagiza kakwama kodi
Mwenye uhitaji atatakiwa kuikomboa kodi ni kama 6m,na gharama za mwenye gari alieagiza ni 5m
Namba zake ni 0736770052
 
Passo ni pikipiki sio gari
 
Yangu Mimi Ni 1NZ FE 1490cc, 4WD, IST shida nayokutana nayo sasa gariimebadilisha sound engine, ikichanganya inalia Kama Subaru, Yani inabadili mlio kama vile ni manual, si mda wote Kuna wakati inatulia na kutoa mlio vizuri, fundi kwenda kupima hakuona kitu, akapewa namba ya fundi mmoja wa umeme, kwenda kuicheki, yuko muhimbili. Akamuambia hizi nazijua za 4WD, Kuna spacio pia juzi ilikuja hapa 4WD, shida inakuwa ni Exhaust imeziba, akasema Kuna opt mbili, kuizibua ni 1k ila itaongeza ulaji wa mafuta, au kudilisha Exhaust nimeambiwa 5k, nikamwambia nirudishie kwanza gari nijipange, naomba ushauri maana nimekuwa na mashaka na huyu fundi Kama kweli anajua shida ya gari, shida mlio wa gari kubadilika. Shida ya vibration imeshajibiwa hapo au mwenye kujua fundi wa uhakika, wa TOYOTA IST 2004, plz nisaidie.
 
Nina IST engine ya 2NZ, ina shida ya taa ya check engine kuwaka, ila ukiiwasha kwa kuivizia (mfano ukiweka switch on unailia pose kidogo ndio uwashe) check engine haitokei. Funguo yake original ilipotea ivyo natumia ya kuchonga.
 
Kwahio uliogopa hizo bei za Buku(1k) na elfu 5(5k) mkuu?
 
Naikubal Sana
 
Baada ya kuibiwa Sana na mafundi, kupoteza fedha nyingi, na kusoma thread nyingi kuhusu Toyota IST, namshukuru Mungu, nimepata fundi wa uhakika anayejua nini ni nini Yani nini kimesababishwa na nini, na nini afanye ili Kuondoa tatizo, Baada ya kumpelekea gari akaiendesha kwanza, alivyoshuka aliniambia matatizo ya ile gari yote kabla hata Mimi sijamuambia. Nikashangaa. Alinijibu kitaalamu tatizo la gari Kukosa nguvu uwashapo A/C, alinijibu kitaalamu tatizo la gari Kukosa nguvu bila hata kuwasha A/C, alinijibu kitaalamu tatizo la gari kuanza kula mafuta, tatizo la gari kutochanganya speed, kanirekebishia gari vyote Sasa gari imerudi mpya, ingawa ni IST hapo mwanzo ilikuwa inakula 1litre kwa kilometer 10, Sasa inaenda 1litre kilometer 17, na ni Cc 1500, wale walikuwa wanasema sababu ni four wheel Drive automatic, ndo Mana gari haichangani speed haina nguvu si kweli, aisee Kuna vitu vingi Sana hatuvijui kuhusu magari, mafundi wengi sababu hawajui kutengeneza watakuambia hiki kimekufa nunua kipya, kumbe kinarekebishika, akishindwa kabisa atakuambia tubadili kitu flani kumbe ni kizima, na nimegundua watu wengi Sana wameuza magari yao angali ni mazima sababu ya hawa mafundi feki wasiojua Nini wanafanya, Mimi niliambiwa nibadili Exhaust imekufa na ni laki 5 na nusu ili kurekebisha mlio mkubwa kwenye sauti kumbe ni nzima, namshukuru Mungu nilishituka mapema sikufanya hivyo, huyu fundi ndo akanifungua akaniuliza mlio mkubwa wa gari unausikia mbele au nyuma, nikamwambia mbele, akaniambia siyo Exhaust utaibiwa, Yani gari imerudi mpya kabisa nilikuwa niiuze Lakini sasa siuzi Tena. Kutokujua magari nako kumegarimu, Tatizo la A/C Kukosa nguvu hasa mchana amelirekebisha, vitu vingi mafundi wa mwanzo waliniambia havifai yeye karekebisha. Ukipata fundi wa uhakika, na spare original huna haja ya kuuza gari Kama hujalichoka. Nimeibiwa sana na kuliwa fedha zangu nyingi mno, namshukuru Mungu. Huyu fundi wa uhakika Hana tamaa. Kuna mafundi wengine ukitengeneza gari Baada ya mwezi lazima lisumbue tena. Nimegundua mafundi wengi wanaenda kwa mazoea tuu hawazijui gari vizuri, kwa iyo huwa hawaondoi tatizo, Kinachouwa IST nyingi nimejifunza plug feki, oil feki ya gia box, na oil feki, Kama si feki basi si recommend kwa ajili ya Toyota IST na Mimi nilikuwa nabadilishia kwenye sheli kubwa, fundi akaniambia hii oil ni oil ila kwa Toyota IST ni kubwa ingekuja kuuwa engine, hii inatakiwa kwenye Toyota Harrier, alfu ndo wengi tunawekewa kwenye masheli haya, nikasema ndo mana engine zinawahi kufa aisee daah hawa mafundi hawa, na Hawa wanaotubadilishia oil wakitushauri sababu ya ugeni au kutokujua wametuulia Sana magari yetu, Kama umesumbuka kama Mimi na una IST au toyota yenye matatizo Kama hayo hapo juu, Natoa namba ya huyu fundi aliyenisaidia mimi na kunifungua macho na kunishauri 0684516017 -fundi Reginald, ili usije ukapata hasara Kama mimi, inawezekana nawe hulijui gari vizuri Kama mimi huyu atakusaidia, usiize gari Kama bado unaipenda uyu jamaa ni kichwa mtaalamu hasa habatishi kazi yake atakusaidia mcheki.
 
The Tomorrow People , na wadau wote katika uzi huu.

Toyota IST ncp61 (odometer 129,000KM hadi sasa) ina matatizo yafuatayo:

1. Mlio wa kugonga hivi kwenye engene (knocking sound... koh koh koh koh koh). Mlio huu husikika baada ya engene jupata joto. Yaani unapowasha on the start mlio huo haupo, ila baada ya muda fulani at idle au gari ikishatembea engene ikapata joto ndipo huu mlio huanza kusikika. Mlio huu ni kama nilianza kuunotice baada ya kuanza kuweka 'petrol treatment' kwenye fuel (japo sina hakika sana kuhusu hili). Mlio huu una zaidi ya miezi saba sasa tangu uanze. Usikilize hapa...(audio)
Your browser is not able to play this audio.


2. Hivi karibuni, mwezi mmoja uliopita, nimegundua engene oil imeanza kupungua kwa kiwango kidogo.

3. Coolant huwa inapungua pia kwa kiwango kidogo. Kwa mwaka mzima nimetumia LITA MOJA ya coolant kwaajili ya kuongezea 'full level' from time to time.

N.B: Nazingatia service kwa wakati (kila kilomita 5,000 nabadilisha engene oil). Natumia oil ya TOTAL 5W-30 (Quartz 9000 full synthetic). ATF natumia TYPE T-IV as recommended kwenye dipstick. Gari ina power vizuri kwenye mwendo. Engene haijaguswa, ni kubadili plugs tu from time to time, nawekaga DENSO Iridium (genuine plugs).

Wakuu naombeni msaada wenu wa mawazo na kitaalamu nitatue matatizo hayo matatu tajwa hapo juu.
 

Cc: General Mangi
 

Cc: Torque vs HP
 

Cc: pndiba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…