Matatizo ya Tanzania na mapendekezo ya wana JamiiForums

Mzalendo,

Usitiwe moyo sana na CPI ya Transparency International. Hata mimi mwanzo niliwaamini sana nilipowafagilia kwenye thread hii hapa. Lakini baada ya kuelewa jinsi gani wanavyofikia index hiyo nikagundua kuwa siyo reliable sana ingawa inatoa mwelekeo wa impact ya rushwa kwa wananchi. Kuna nchi kama Haiti wamepewa score ya chini sana lakini ukiangalia aina ya rushwa inayoongelewa Haiti ni ile tuliyokuwa tunaita "chauchau" miaka ya zamani au "chai kidogo:" ni rushwa ile ndogo ndogo ya kumhonga trafiki polisi Shs 2,000 kusidi asikushike au kumhonga karani wa ofisi Shs 1,000 kusudi akukamilishie faili lako. Rushwa hii huwa ni kero sana kwa wananchi wa kawaida na ndiyo inayoripotiwa na TI; nadhani ndiyo maana inaitwa perception index. Rushwa kubwa zinazohusu mikataba ya serikali lakini ambazo mwananchi wa kawaida hawoni kero yake mara moja hazichangii sana kwenye hii CPI. Nadhani umenielewa.

Halafu ukisoma jinsi wanavyoifikia namba hiyo pia kuna utata kidogo kwa vile wanatumia "businesspeople and country analysts." Kama wafanyabiashara wanafaidi katika rushwa iliyopo, perception yao inakuwa nzuri na wasiopfaidi then preception yao inakuwa mbaya. Unaweza kuangalia wafanyabisahara wa Tanzania ni nani na ni nani anayefaidi zaidi system hii ya ruhswa. Iwapo tasisi kama polisi na TRA wakianza kuwazongazonga wafanyabiashara hawa bila sababu ya msingi utaona CPI inapungua hata kama Serikali kuu ikiwa perfectly clean katika mikataba yake yote.
 
kwa kifupi ni kuwa hali ilivyo tanzania ni time bomb.


Na bahati mbaya zaidi ni kuwa yule aliyetegemewa kuwa tegemeo la mwisho kwa ukombozi bado ana strategies wakati manyang'au wanajifaragua katika fungate lisilokwisha....

Tanzanianjema
 
Hata hivyo, kumbukeni kuwa na kiasi. Tanzania ni nchi nzuri sana. Ruksa kuchukia CCM (ambayo ndiyo imelea maovu haya), lakini mwiko kuchukia Tanzania.

Kuinusuru Tanzania ni lazima CCM ikae benchi kidogo. Haiwezekani kuendesha gari vingine kama dereva atabaki yule yule. CCM ipelekwe kambi ya upinzani kama ilivyofanyika kwa KANU.

Augustine Moshi
 
Ruksa kuchukia CCM (ambayo ndiyo imelea maovu haya

CCM haipaswi kuchukiwa bali inahitaji upendo zaidi na sio ushabiki wa kipambe kama ulikuwapo sasa. Maovu yanalelewa na watanzania wote ambao tunapenda njia za mkato katika kila kitu...


Tanzanianjema
 
Du,
Sasa sisi ni lipi la kufurahia? Amani na utulivu? Au may be uvumilivu tuliokuwa nao miaka yote?
 

Sio inaongoza kwa RUSHWA bali kwa WIZI wa mali ya umma.
 
duhhhhhhhhhhhhhhh ! hii iwekwe kwenye nyepesi nyepesi aiseeeee, maana ! ok, ndio tz hiyo babu. acha waliopo bongo wajichane, kwani hata JK mwenyewe alisema watz wapo nje wanasubiri nchi watengenezewe, na nani ? kama wanataka changes waende bongo wafanya changes, sasa nimemuelewa !
 
Pressure on Kikwete to act on graft

When the gathering political storm in Tanzania reaches a crisis, President Jakaya Kikwete might be forced to do the unthinkable - sacrifice bosom friend, Prime Minister Edward Lowasa.

The public views the premier as the embodiment of graft in the Government, which the president cannot tame.

Jakaya has come under pressure in the past two months to purge "rotten eggs" from his stable.

Among the donor community, he is anything but not in charge..

The Government was last week thrown into panic after Western development partners demanded action on runaway corruption, failing which they threatened to withhold financial support pending the arrest and prosecution of the culprits.

Donors have warned that Tanzania, which has a hole in its $5.8 billion budget, risks aid cuts for failing to rein in graft.

The prospect of aid cutback elicited angry response from Foreign Minister, Mr. Bernard Membe, who demanded that the envoys stop meddling in Tanzanias affairs.

Matters were worsened whenhe threated to expel foreign envoys who recently threatened to halt development funding pending investigation of fraud allegations.

The standoff between Tanzania and donors had a ring of the controversy between Kenya and its development partners, during which aid was withheld for more than 14 years from 1992.

Sourcestold the Sunday Standard that a Cabinet reshuffle looms in which key Kikwete allies, including Lowasa, are likely to be relieved of their duties.
He added that the public is concerned that the Government has failed to quell ethnic cleansing in the West where scores of people have been killed. (????)

The media have been directed not to report the blood bath in Kagera "to maintain a good image of the country abroad." (?????)

The opposition has taken the cue from the public and given the Government one-month ultimatum to institute investigation into fraud allegations and quell ethnic cleansing or risk countrywide civil disobidience.

Opposition parties - Chadema, Tanzania Labour Party (TLP), NCCR-Mageuzi and Civic United Front (CUF) - announced on Monday plans to organize demonstrations to force the Government to come clean on graft allegations.

President's son in financial rip offs???

Word on the streets in Dar has it that the reshuffle could be on the cards soon after the national elections of the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) next month.

To cushion himself againstpotential retribution, opposition leaders said, Lowasa involved the president's son in one of massive financial ripoffs in which the taxpayer lost huge sums of money through faulty tendering of Tanzania Electric Supply Company (Tanesco for the procurement of emergency power generators last year.

The expensive equipment turned out to be second-hand. They stalled just months after they were commissioned,(???)plunging the country into darkness and limited production hours.

The public is also concerned over dumping of the junk presidential jet for which the Exchequer paid $44 million - more than twice the actual cost of a new aircraft.(?????)The jet is not in use, barely six years since it was bought.

There is also the matter of the Bank of Tanzania (BOT) that is set to cost the taxpayer $340 million; which experts saying the figure is 10 times above the actual cost. The president is accused of being aware of the scams but failing to act as his henchmen have huge stakes in them.

This is a new experience for Dar es Salaam, which is beginning to feel the heat after donors demanded transparency in public expenditure.

The demand was prompted by the compilation and circulation of a 'List of shame'by the Opposition, which indicts Lowasa, Kikwete's son and wife (????), businessman and MP Rostam Aziz - who bankrolled Kikwete's election in 2005).

But the Director of Communications Salva Rweyemamu dismissed the 'List of shame' as 'A List of Lies'. Rweyemamu, a journalist, who used his position as a managing editor at Habari Corporation to Campaign for Kikwete, admitted on Tuesday that BOT was indeed under investigation.

Civil disobidience is an alien concept in Dar and would never have been contemplated as a means of protesting at State culpability. Political unrest is also rare, save for occassional flare-ups at election time.

But this time round, senior Cabinet members are under scrutiny as an increasingly restless public question the Kikwete administration's inability to fight poverty and corruption.

As a sign of the gathering storm, Cabinet ministers going round the country to 'explain' the budget to the electorate were heckled as wananchi complained of rising cost of food, fuel and unemployment.

The level of public discontet is unpresidented and the opposion has rolled out civil education to sensitise the public.

Source: Sunday Standard (Kenya) of October 14, 2007.
Repoter: Ernest Mpinganjira

Tukiacha ushabiki alionao mwandishi huyu - kwani tunajua kuwa akisikia Tanzania imezama Bahari ya Hindi atafungua mvinyo wa kusherehekea, kutokana na maandishi yake ya siku nyingi kuhusu Tanzania, mambo mengi aliyoyagusia yanaeleweka na mengine hayaeleweki na hayajawahi kusikika hata hapa JF, pamoja na majigambo ya wengine wetu hapa kwamba mambo mengi yanaanza kujulikana kupitia JF.

Kwa mfano: Je, kuna ukweli wowote kuhusu ethnic cleansing huko Kagera ambayo hata vyombo vya habari vimezibwa midomo?

Jambo la ndege ya rais nalo ni la kusikitisha na wengi hatulifahamu vizuri. Je, ni kweli hiyo ndege ni mkweche, na ilinunuliwa kwa bei mbaya hiyo inayosemwa humo? Kama hivyo ndivyo, mbona hata hatulipigii kelele zinazostahili na hao waliotuingiza katika hasara hiyo wawajibishwe iasavyo?


Nayo hiyo 'List of shame' iliyo na watoto na wake wa mkuu mliwahi kuiona popote? Hilo 'deal' la Tanesco na Kikwete mdogo yawezekana likawepo.

Inazidi kudhihirika sasa kuwa Kikwete mwenyewe ni sehemu ya tatizo la rushwa katika serikali yake. Anayafahamu yote yanayoendelea. Hii ni dalili mbaya ya uongozi kwa upande wake. Hana tofauti yoyote na Kibaki, na yeye sasa tuanze kufikiria kumpa miaka yake iliyobaki, baada ya hapo akapumzike. Inaonekana hastahiri kupewa miaka mingine mitano huyu.
 
The author has point, however me and you we don't have enough facts to prove some of his points. I can't declare all of his points are false, but i can't accept some of them because i don't have enough evidence to accept them.

All in all, i like his article.
 
Atajibiwa humuhumu JF na hata kwenye makaratasi cha muhimu tusubiri ni majibu gani hususani hli la Bukoba huko
 
Huyu mwandishi anatumia ukweli kidogo kufanya madai ambayo
hana data za kuyathibitisha.

Article kama hii angeandika huku kwao wangemaliza mara moja.

Kwasababu anajua hatuna watu wa kukabiliana naye kwa hoja basi anaandika uchafu wowote aliowahi kuusikia karibuni bila kufanya uchunguzi wa kina.
 
Pamoja na kukosa baadhi ya facts ama kuwa nazo ambazo hazijafanyiwa kazi, lakini mwandishi anatupa picha moja mbaya sana kwamba kuna PENGO KUBWA KATIKA MEDIA ZA TANZANIA.
1. Media za Tanzania haziwezi moja kwa moja kumuandika Lowasa na Rostam Aziz, jambo ambalo mwandishi hapa kawaandika. Thisday wamejaribu naona wanabanwa sasa na mumeona Nguba katoa statement.
2. Media ya Tanzania imekua na woga na upenzi ambao hausaidii Taifa.
3. Media ya Tanzania haina umoja kwa mambo yanayogusa maslahi ya Taifa, habari ikiandikwa na gazeti moja mengine hayafuatilii kama ilivyo Kenya na Uganda.
 
Brown envelopes zinafanya kazi.
 

Halisi:
Sote tunaelewa udhaifu wa vyombo vya habari hapa nchini kwetu. Hivyo vinavyomilikiwa na serikali, wao hawana lolote na pengine hatuwezi kuwalaumu kwa kuogopa kuukata mkono wa asali. Vile vinavyomilikiwa na wafanya biashara, mambo ni yale yale, wako katika biashara. Lengo sio kupasha habari kama zinavyotokea.

Lakini....., bado siamini kabisa kwamba 'ethnic cleansing' huko Kagera itokee na pasiwe hata na chombo kimoja tu cha kutoa habari hiyo, eti kwa kuogopa kulipaka tope taifa. Huo ni uzushi wa huyo mwandishi wa habari wa Sunday Standard; na sitaamini mpaka niambiwe kuwa ni kweli hayo yapo, na yanaendelea kutokea na vyanzo vinavyoaminika.
Mbona hapa JF kuna watu toka sehemu mbalimbali nchini; nao kweli wanaogopa kutoa habari kama hizo? Sababu ikiwa ni nini!
 
Jamani watanzania wenzangu..tumekua tukipiga makelele kila siku..usiku na mchana..lakini makelele haya yanaoneka kuwa sio sauti ya wengi..bali ni sauti ya watu wacheche tu wenye upeo na elimu na uelewa tosha wa namna nchi inavyokwenda.. Scandals nyingi zinaibuka..zina heat na zinafifia..nikianza kuzitaja hapa sitamaliza.. nanitazidi kujiongezea machungu tu..Watanzania tunakerwa na jinsi mambo yanvyoendeshwa katika nchi yetu hii tajiri lakini sisi wenyewe kwa vinywa vyetu kutokana na kujazwa ujinga na viongozi hawa wasio na sifa tunaaita eti nchi maskini.''si kweli''...wenye upeo wanapinga..wanakerwa..na bado wanaendeleza mapambano wakiamini kuwa ipo siku watakuja kushinda na nchi itaendeshwa kama inavyotakiwa na kila mtanzania atanufaika na kujivunia na nchi yake...mapambano ni makali..lakini chakusikitisha wanaopambana ni wachache mno..kwa kukadiria haiwezi kufika asilimia 10 ya total population ya Tanzania...ili mapambano yaende katika muelekeo wa kushinda nadahani kuna challenge kubwa ya kuongeza iyo silimia niliyoitaja hapo juu..nafikiri mtakubnaliana na mimi kuwa watanzania wengi sana..hawajui na hata hawana hulka ya kufuatilia jinsi mambo yanavyo kwenda kwenye nchi yao..wengi ni mashabiki tu hasa ifikapo kipindi cha uchaguzi..magezeti hawasomi..kama watasoma basi ni ya udaku..TV habari hawaangalii kama kuangalia ni miziki..Internet ndio kabisa..laiti wangekua wanafuatilia mambo basi leo hii tusingepata viongozi ama tulio nao kwa sasa...kuna mwanafalsafa mmoja alisema ''Democracy is the Tool for the Fools'' Yani akimaanisha kwamba Wengi wape'' na hao wengi wengi wao ni mashabiki tu na hawaelewi kitu wanachokifanya kina madhara gani kwao na kizazi chao kijacho...Hapa basi ndipo napopata tasirwa..je katika nchi hii watu kama mzee mwanakijiji, kichuguu,fidel mashall, Rev, Kishoka, na wadau wengi wa humu JForum wangekua wapetapakaa nchi nzima walau kwa asilimia 40 tu.. nadhani vita hivi vingekua rahisi mno kuliko tunavyofikiria...na sasa tungekua tunaongele masuala ya maendeleo ya nchi yetu tu..sio kupoteza muda kunyooshea vidole mafisadi.

Sasa hapa ndipo ninapojiuliza je ..umefika wakati sasa wa somo la uraia kwa watanzania wote liwe ni la lazima??????

Nawasilisha hoja ndugu wadau..


''Huu ni mtazamo tu wananchi msijenge chuki''
 
Umalaya Tanzania tunaambiwa ni raha ya kuwa na cheo cha juu serikalini.
Kwa ujinga wetu hatuelewi kwamba Fedha za kuhonga Malaya waMafisadi zinachotwa katika Bajeti ya Serikali.

Fisadi na Malaya wengi maana yake Matumizi makubwa,matumizi makubwa yanachochea wizi mkubwa.

Umalaya ni Sumu kwa famila na kwa jamii nzima.

Watanzania ni vema tuamke toka kwenye usingizi wetu na kuhoji iweje viongozi wetu wamegeuza nchi yetu kichwa cha mwendawazimu?

Tanzania iliyovamiwa na mafisadi wa KiSISIEMU itakombolewa na Watanzania wenyewe bila nguvu ya ya mtu mwingine yeyote kutoka nchinyingine. Pia Tanzania itajengwa na Watanzania wenyewe siyo mashirika ya kigeni yanayozidi kujikita Tanzania.

Viongozi wengi wa SISIEMU ni lazima waachie ngazi kupisha Watanzania waliotayri kuijenga nchi yao. Yote haya yatafinyika ndani ya uhai wetu.
 
Tanzania,tuko wapi? na tunaelekea wapi? kila nikiwaza sipati majibu kichwa kinaniuma nabaki kutapatapa,hebu sisi kumbe hatujui tuko katika mfumo gani, hatujui kama tumo ndani ya ubepari, au ule ubeberu,ama ni zile sela za ulaya za karne ya 15? yaani PAC(Primitive accumulation of capital), sina jibu.
Ndugu zangu watanzania mbona tunamalizana wenyewe? mbona twalizana wenyewe? hebu tutafika? wachache muwe nacho sisi hoi!kamwe hatutafika,iko siku litapasuka,litalipuka tu, hatuombi iwe hivyo na Mungu atunusuru.
Mwalimu alituachia nchi njema ikiwa na madini,ardhi ya kutosha ila sasa tumeanza kutosana,hebu tanzania tunaelekea wapi? sioni mwelekeo naona giza, na mawingu mazito, wenye tochi,miamvuli na majaketi hao wachache ndiyo wanahimili safari hii, sasa na sisi watoto wa walala hoi tutafikaje huko?
Serikali tuambieni tuko katika mfumo gani? ni ule wa kugawana tulichokuwa nacho(sisi wanyonge) na kukifanya chenu tu(viongozi) ama ni chetu sote? siku itafika tutakuwa wote miguu sawa.
Wale wakulima kule kijiji mmewasahau,wafugaji mmewatupa,mnasema tutafika tuu,mmesahau navyi mlikuwa watoto wa wakulima na wafugaji na tena mkasoma bure, mijengo yenu sasa iko fukweni,na sehemu zenye unadhifu, hakika mmejisahau,yale ya Kenya kutaka haki sawa siku moja yatafika na hapa kwetu

Sina hasira ila nawajibika.
 
Ndugu wanaJF na watanzania kwa ujumla popote mlipo,
Mijadala mingi sana hususan katika ukumbi huu wa jukwaa la siasa pamoja na habari zinazopostiwa hapa,zinaendelea kuthibitisha jinsi taifa letu lilivyo katika matatizo makubwa sana. Mbaya zaidi ni dhahiri kwamba uongozi tulionao sasa hauleti matumaini kwamba siku moja taifa litaondokana na matatizo hayo. Matharani kwa sasa unatajwa sana ufisadi, tena mafisadi wenyewe ni viongozi hao hao ambao wangeudhibiti huo ufisadi.

Sasa ndugu zangu, tutadumu katika kuwajadili watu hawa hata lini? tutaendelea kusimulia matatizo tuliyonayo mpaka mwaka gani?

Wakati umefika tuanze kuhabarishana na kujadiliana ni nini tufanye na bila kusahau nani afanye. Yawezekana tukaendelea kulia,na machozi yetu yasitofautiane na ya samaki ziwani, nchi yetu itaangamia hivi hivi tunaona.
Jamani mgonjwa atibiwe sasa vinginevyo atatufia mkononi na msiba utakuwa ni wetu sote. Ni nini dawa,iko wapi, nani tabibu???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…