Matatizo ya Tanzania na mapendekezo ya wana JamiiForums

si kidogo... Katiba inasema sisi ni Wajamaa.. lakini kivitendo tumeachana na Ujamaa toka Zanzibar. je kwa viongozi wetu kutokujenga nchi kwa misingi ya kijamaa, hawavunji Katiba?
 
Mwl alisema kuwa.. kuzungumzia na kutetea ujamaa inabidi uwe mwendawazimu!
Walipotoka Zanzibar, Rais Mstaafu Nd. A. H. mwinyi alitoa hotuba hii hapa kwenye attachment!
 

Attachments

Ndiyo nimeipitia hiyo Brutus, hata ukiangalia maelezo hayo ya Zanzibar, utaona kuwa bado tumeyavunja hata hayo! Je ni viongozi wangapi wenye kumiliki majengo kwa ajili ya faida na siyo nyumba za ziada? Ni wangapi ambao wanapokea mshahara zaidi ya mmoja? Tunaposema Itikadi ya kijamaa, tunamaanisha nini? Huku nyuma angalau tulikuwa na mawazo kama ya Azimio la Arusha na wale tuliosoma Political Economy utaona ni jinsi gani tulikuwa tunafundishwa ujenzi wa Taifa la Kijamaa.

Kama ni kweli bado tunataka kujenga ujamaa, wasomi wetu wako wapi kutufafanulia ujamaa wetu ukoje? Kama hatujengi ujamaa na sasa tunashughulika na Umtaji (Capitalism) kwanini bado Katiba ya Nchi na ile ya CCM bado vinatuzuga kuwa tunataka kujenga Ujamaa? Kama tumeamua kujenga ubepari ambapo kila mtu kivyake vyake ila Mungu wetu sote, basi tuambiane ili tujue ya kuwa kujaribu kufanya mambo ya kijamaa haiwezekani. Au wajamaa ni sisi wachini (SACCOS, NGOs n.k) lakini wakubwa ndio mabepari!?

Na hili suala la kunyonyana, hivi tumesharuhusiwa kuanza kunyonyana maana nakumbuka miaka ile tuliimba:

"Mabepari walia, mabepari walia, mabepari walia kukatiwa mirija!
Walipotangaziwa, Walipotangaziwa Azimio la Arusha!"

Hivi leo mabepari wana sababu ya kulia wanaposikia Azimio la Arusha????

Nakumbuka kikatuni kimoja kiliwa kuwepo (Mfanyakazi????) ambapo mijamaa minene imekaa huku mirija ikiwa midomoni mwao wakimfyonza mfanyakazi ambaye alikuwa amekondeana na kunyong'onyea!
 
Nd. Mwanakijiji!
Hebu tuanze kwanza kuangalia Definition ya CHAMA CHA MAPINDUZI!
Ni Mapinduzi gani yanayozungumziwa??

Itakuwa inaingia akilini kama yangekuwa ni Mapinduzi-Endelevu!
Kama Walipokutana Zanzibar walikubaliana ku-tafsiri Azimio la Arusha ili liende na wakati.. (Mapinduzi-Endelevu).. mkutano ambao Muasisi wa Azimio la Arusha aliuchunia... na baadaye kuwaponda; basi hatuna budi kukaa chini tena na kufanya tafakuri juu ya Ujamaa wetu na Azimio la Arusha.

Hata ufafanuzi alioutoa Mwenyekiti mstaafu (Rais Mwinyi) kwa kweli ni joke!
Imekuwa kama kumfungulia mbwa aliyekuwa amefungwa kwenye banda miaka mingi... ametoka nje anakimbia kimbia hovyo, yuko excited!!

Katiba ya nchi na ile ya CCM bado vinatetea sera ya Ujamaa!
kwa hiyo kwenda kinyume na ujamaa ni kosa la jinai!
Usaliti!
Linalotakiwa ni kukaa chini na kufanya tafakuri juu ya ujamaa wetu... maana watu walichanganyikiwa na style yetu!.. ulikuwa ni Ukomunisti, ujamaa wa Nordic au wachina?
Bado tuna opportunity ya kulifanya taifa letu kuwa la mfano barani Afrika na Duniani kwa sababu tuna opportunities ambazo nchi nyingine duniani hawana.
Tuna Ardhi ya kutosha, maziwa, mbuga, madini, pwani kubwa yewe uwezo wa kubeba bandari za kisasa, na zaidi ya yote watu wanaishi kwa kuelewana.

Mshairi mmoja amesema:-

"Kutaraji uongofu bila kupitia njia zake ni kama kulitaka
jahazi kutembea nchi kavu"
.... Rais Mstaafu Nd. A. H. Mwinyi
 
hii hotuba imenikumbusha enzi za mzee mwinyi, unajua ccm ni watu wa ajabu sana, ukisoma hotuba zao ni nzuri kweli na za kuleta matumaini, lakini wanakuja kufanya mambo kinyume kabisa na yale wanayo aihidi,
hii hotuba mzee mwinyi amejitahidi kuonyesha kuwa ccm ni chama progressive lakini walicho kuja kukifanya baada ya azimio la zanzibar ni disastrous!!
 
watu wa London, wangemuuliza Muungwana.... "Mhe. Rais, Katiba ya Tanzania na ya CCM vinasema wazi kuwa Tanzania ni nchi ya kijamaa inayojenga ujamaa kwa misingi ya kujitegemea. Hata hivyo halisi ni kuwa Tanzania inatilia mkazo mtaji na ujasiriamali (capital and enterpreneurship), je unaweza kuwaambia watanzania kuwa Tanzania bado inafuata misingi ya Kijamaa ilivyofafanuliwa na Azimio la Arusha na baadaye Azimio la Zanzibar? Ni ujamaa wa aina gani Tanzania inajaribu kujenga??
 
Hilo swali linahitaji Political Scientist!
Hata hivyo tunaweza kutumia Entrepreneurship na tabia nyinginezo za capitalism kujenga taifa la kijamaa!
Ni suala la uamuzi tu!
 
Nd Mwanakijiji,
naomba nisikurupuke kujibu hili swali!
Acha nikusanye maelezo ya kutosha!

Maana ukiangalia kwa undani, hata USA, Canada na Britain ambao tunasema ni pure-capilalists bado wana vitu kama free care kwa wasiojiweza , posta na mashirika sensitive kama haya bado yanamilikiwa na Federal Govt ingawa yanajiendesha kibiashara! Gharama za masomo kwenye Public Schools ni rahisi na opportunities za kuendelea kwa watoto waliofaulu hata kama ni maskini zipo!
Hizi ni tabia za kijamaa ndani ya mfumo wa ubepari!

Sisi wenye neno ujamaa kwenye Constitution hatuna hizi habari!

let me do some homework then i will be back with something ... maana swali lako linaweza kuwa dissertation ya PhD candidate!
 
Brutus, while youa re at it.. jaribu kuninyambulia kama tungetaka kujenga "Ujamaa wa Kiafrika" ungekuwaje?
 
Mzee Mwanakijiji,

Kwanza nimshukuru Brutus kwa kipande cha hotuba ya Mwinyi... Duuuh jamani hata Mwinyi kumbe alikuwa kabuntas?

Toka lini DIRA YA NCHI ikawa na mabadiliko ambayo yanatokana na mikakati mfumo wa kibiashara ama kisiasa?... Tena anatumia mifano ambayo haihusiani kabsia na swala la wakati kwa sababu UJAMAA na KUJITEGEMEA hakuna wakati isipokuwa njia za kufika huko ndizo zinaweza kubadilika lakini tafsiri itabakia palepale.

Ujamma, and self reliance
The objective of Ujamaa (socialism) in the United Republic of Tanzania is to build a society in which all members have equal rights and equal opportunities; in which all can live in peace with their neighbours without suffering or imposing injustice, being exploited, or exploiting; and in which all have a gradually increasing basic level of material welfare before any individual lives. (Nyerere 1968: 340)

Sasa jamani kweli leo hii na Utandawazi bado hatuwezi kufanya UJAMAA huo?
 
Wanaforum,

wakati tunajiuliza kama tunafuata ujamaa au ubepari, naona itakuwa vyema tujiulize kwanza kuwa China ni nchi ya kijamaa au kibepari?
 
mTz

Duh. Wachina mimi sifahamu sera zao lakini nafikiria wamepunguza kidogo zile itikadi zao za zamani. Wamefanya mabadiliko kidogo ndio maana wanawekeza sana sasa huku Afrika ili wajizatiti.
 
Ole!

Jana kulikuwa na progran kwenye Skynews about China and their economic growth, swali hilo lilikuwa pasua kichwa. Lakini kama member mmoja alivyosema hata kwenye nchi za kibepari, elements za ujamaa zipo tu. Watu UK wanapata tiba bure thru NHS, vilevile wazee wanasafiri bure ndani ya mabasi. I think the crucial thing is how to strike that delicate balance between ubepari and ujamaa in order to attain prosperity ya citizens
 
mTz na Ole,
Mimi siku zote sikubaliani na tafsiri za watu kwa sababu moja kubwa sana. Ujamaa ni dira na haiwezi kuwa inabadilika kwa sababu ya mfumo wa kisiasa ila kuna uwezekano wa mambo fulani kuwa na kipaumbele kabla ya mengine kulingana na siasa za chama kinachotawala...hapo ndipo mifumo na sera zinapoingia kati lakini lengo bado linaweza kuwa lile lile. - UJAMAA na KUJITEGEMEA. Ukiwambia Norway kuwa wao Mabepari mjomba watakuua!
Kuna msemo fulani wa kisiasa ambao wengi huutumia wakisema hivi:-
Kipi kinaleta maendeleo haraka, Kuwa na tajiri mmoja ambaye atawapa ajira ya uhakika familia nzima (ubepari) au kuwa na familia ambayo wote ni waajiriwa!(ujamaa)

Kwa bahati mbaya Tanzania leo hii familia yote ni waajiriwa (Ujamaa) ktk mfumo ambao kuna matajiri wachache nje ya familia (wageni). Kwa hiyo sisi sio Wajamaa wala Mabepari.
Na kinachochekesha zaidi ni kwamba wanapo pima maendeleo ya nchi siku zote huangalia maendeleo ya wananchi wake kwa UJUMLA (ujamaa) na uwezo wa nchi kujitosheleza kiuchumi (Kujitegemea) pasipo madeni.

Kazi kwenu!
 
Brutus, while youa re at it.. jaribu kuninyambulia kama tungetaka kujenga "Ujamaa wa Kiafrika" ungekuwaje?

Nd. Mwanakijiji!
Hili suala sio dogo na wala tusili-underestimate!
kabla hatujatazama "Ujamaa wa Kiafrika hebu kwanza tutupie macho "Ujamaa wa kizungu au ki-asia!

Marx na Angels walieleza kwamba mfumo wa maendeleo ya maisha ya binadamu una hatua kadhaa:
1. Primitive Communalism ( Ujima)
hapa watu waliishi maisha duni yasiyo na teknologia. Waliishi pamoja kupitia jamii zao za kijima (Communal societies)!
mfano mzuri wa hili kaangalie movie.. " The gods must be crazy"

2. Utumwa ( Slavery)
Hapa watu waliuzwa toka kwenye "Communal Societies" kwenda kwenye tabaka jingine la watu walioendelea kidogo baada ya kuhodhi ardhi kubwa "Feudal Lords" ambako walitumika kama vitendea kazi!
Mchanganyiko huu wa watumwa na mabwana zao wenye kuhodhi mashamba makubwa uliunda mfumo mpya..,..

3 Ukabaila..(Feudalism)
Na huu mfumo mpya ulipoendelea na kuanza kuchipuka kwa viwanda... na kukomeshwa kwa biashara ya utumwa kukazaa mfumo mpya...

4. Capitalism ( Ubepari)..
Hapa sasa... wale watumwa walioachiwa huru toka kwenye mfumo wa Ukabaila wakageuka kuwa Wafanyakazi (workers)!

Lakini kukawa na tatizo... hawa wafanyakazi wakawa wananyonywa sana... wakafanyishwa kazi ngumu kwa masaa mengi lakini kwa ujira mdogo. Hali hii ni unyonyaji wa jasho la wafanyakazi... ndipo kukatokea fukuto la mapinduzi .. kwamba kuwe na mgawanyo sawa wa mapato. Fukuto hili likazaa mfumo mwingine wa kinadharia zaidi kuliko vitendo ..

5. Socialism!
Hapa ndipo tunawasikia Bolsheviks na ndugu zao... (Mapinduzi ya Urusi)

Lakini sasa... sio watu wote waliokubaliana na mgawanyo sawa wa mali. Hii ikasababisha mgawanyiko wa itikadi.
Waliofuata Warusi wakaunda kundi lao.. na waliokataa wakaunda makundi yao.. ( Eastern and Western Blocs)!

Ingawa hawa watu wa magharibi hawakukubaliana na Bolsheviks, lakini walikuja na ideas zao.. na mojawapo kuu likawa ni kupunguza makali ya Ubepari ,.. "social injustices) ili mfumo huu uwe na faida kwa wote... wenye mali na wafanyakazi. Vikaundwa vyama vilivyokuwa na lengo la kuimarisha sheria za kazi (labour laws) ili wafanyakazi wapate haki zao za kimsingi.. wasinyonywe na mabepari; vyama hivi pia vikajitahidi kuhakikisha middle class inaneemeka na mfumo mzima wa kibepari kwa kutumia mifumo ya ustawi wa jamii.. (Welfare)!
Hapa ndipo tunapokutana na Democrats wa marekani, Labour wa UK, Social Democrats wa Ujerumani na kadhalika.
Ni vyama vinavyotetea tabia za kijamaa bila kuwa na nembo ya Ujamaa!

Sasa tukirudi Afrika....

Sisi hatukupitia hizi pilika pilika kama walizopitia wenzetu!
Wana wa Afrika akina Lumumba, Nyerere, Mondlane, Nkrumah, Neto na wengineo wakaja na ideologies zao!

Mwl. Nyerere akaonyesha mfano kwa ku-implement Ujamaa na Azimio la Arusha. Na wazo lake kuu ni kama alivyosema;
nanukuu...

The objective of Ujamaa (socialism) in the United Republic of Tanzania is to build a society in which all members have equal rights and equal opportunities; in which all can live in peace with their neighbours without suffering or imposing injustice, being exploited, or exploiting; and in which all have a gradually increasing basic level of material welfare before any individual lives. (Nyerere 1968: 340)


Akaja na idea za Vijiji vya ujamaa,.. hapa watekelezaji wakaanza kuvurunda.. wakawa kama Bolsheviks... mambo ya kuchapana bakora na kuhamishana kinguvu!

Vikaanzishwa viwanda na mabenki... lakini watendaji wakavurunda pia...
Badala ya Kuendesha miundombinu hii kwa kutumia kanuni na sheria za kibepari kwa faida ya umma, wakayaendesha kwa staili ya ( Cha-wote.. who cares!)
Kwa hiyo tulikuwa na mwelekeo sahihi ( vector) lakini tukashindwa kuendesha mambo kisayansi!

Mwalimu alipokata tamaa, waliorithi ndio kama hao.. umesoma mwenyewe hotuba kwenye attachment!

Ikawa ni style ya "fungulia mbwa"!

Awamu ya tatu ikaja.. ikakuta hali imekuwa mbaya... tumeshanasa kwenye nyavu. katika kukuru-kakara za kujinasua.. tumejikuta tunajisonga zaidi kwenye nyavu zao... jamaa wanatubeba kilaiiiniiii wanatimua zao na kapu kwapani!

Tuko kwenye awamu ya nne!
Can we jump out of the basket and be free?
Au ndio tutaangukia mchangani na kukaushwa na jua?
What are we supposed to do?

The middle class is suffering!
The question is...
How can we reform the current situation for our own good?

Grandma aliyeko kijijini atapataje huduma za afya za kisasa kwa gharama nafuu?
Je, Huyu Grandma anaishi vipi wakati anaendelea kulima kwa kutumia jembe la mkono na maksai kama walivyotumia nabii Musa na mitume wenzake karne mia kadhaa zilizopita?

Tunasemaje kwamba Kilimo ndio UTI WA MGONGO wakati babu kizee wa nebraska analima shamba lake kwa kutumia John Deer na kumwagilia na anauza mahindi yake mpaka kwenye makampuni ya kutengeneza Ethanol.. na babu yetu wa Tosamaganga mpaka avute bangi kwanza.. alime weee halafu mvua inampiga bao.. na hakuna alternatives?

Tanzania ilipaswa isambaze chakula mpaka Sudan, Somalia, Eritrea na Ethiopia!
badala yake tunapokea msaada wa vyakula!
 
Brutus, hapa umenikuna umenikumbusha mambo ya "Primitive Accumulation of Capital"...! nitakujibu baadaye ngoja niliwazia.. maana silali....
 
Ndio mzee!
Pengine utanikuta maana Mimi niko tu natafakari hizi stori za mtu wa kwanza kuishi Olduvai Gorge..(pengine alikuwa masai)!.. najiuliza alitorokaje akaenda kuishi middle east halafu Cain (mfugaji.... mmasai) akampiga ndugu yake na rungu..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…