Mateka aisifu Hamas

Mateka aisifu Hamas

Mwanamke mzee Muisrael aliyeachiliwa huru na wapiganaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema alikirimiwa na kutendewa wema katika muda wa wiki mbili alipokuwa ameshikiliwa mateka na kundi hilo la wanamapambano wa Palestina.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Yocheved Lifshitz, ajuza wa miaka 85, amesema Hamas ilimpatia daktari wa kushughulikia afya yake na kufanya kila njia kuhakikisha anapata dawa zake.

Ameongeza kuwa wapiganaji wa Hamas walishughulikia pia mahitaji yake. Bi Lifshitz amesema: "tulikula mkate, jibini nyeupe na matango, kama wao."

Bi Kizee huyo Muisrael ameendelea kusimulia alivyokirimiwa na wanamuqawama wa Palestina akisema: "walituambia wanaiamini Qur'ani na kwa hivyo hawatatudhuru".
Alipoulizwa kwa nini alipeana mkono na mmoja wa wanachama wa Hamas wakati wa kuachiliwa kwake, Bi Lifshitz alisema kwa sababu "walliamiliana nasi kwa wema na walishughulikia mahitaji yetu yote."

Jumatatu usiku, tawi la kijeshi la Hamas la Brigedi za Al Qassam lilitangaza kuwa limewaachilia huru mateka wawili wa Israel - Yocheved Lifshitz na Nurit Cooper mwenye umri wa 79 - kwa "sababu za ubinadamu."
Uislam mwema sana.
 
Toa ushaidi mateka alibakwa au kuuliwa na Hamas. Mmetumia nguvu nyingi sana kukaririsha watu kuwa Hamas ni watu wa ovyo kwa stori nyingi zisizokuwa na ushaidi. Sasa angalia m/mungu jinsi anavyotisha. Mnawasafisha Hamasi wenyewe bila shuruti
Raia zaidi ya 1500 walijiua wenyewe sio?!
 
Watoto wa kiislamu tuache kusifia ugaidi
Gaidi ni gaidi tu hata kama akijificha kwa kusoma Quran tukufu
Watu wangapi wameuawa na hao hamas mpk Sasa em acheni ujinga .
 
Inaruhusiwa kuteka kwa nia na madhumuni mazuri
Wacha we, kumbe kukamata mateka inaruhusiwa. Nikajua ni kitendo cha kigaidi wakati ni utaratibu wa watu fulani.
Vipi suala la kuvamia music festival nalo limeruhusiwa, na la kufyatua maroketi
 
Kumteka kikongwe kama huyo tu ni ugaidi na ndio tushuhudie wale wanaosema vikundi kama Hamas ni vikundi vya kigaidi sio waongo.

Na huyo kikongwe kwenye mahojiano alisema wakati wa kutekwa alipewa kipigo pamoja na kuporwa mkufu wake na watekaji taarifa ambayo mleta mada kwa sababu za kiimani hajaongelea kabisa.

Kama wewe kweli ni muungwana na mwenye kumuogopa Mungu kiukweli bila unafiki huwezi kabisa kufanya vitendo vya kigaidi kama kuteka watu sanasana unatakiwa kutafuta ufumbuzi wa changamoto zako kwa maombi zaidi.
Israeli yeye hawachi wazee, watoto, hata wale watoto wenye downsyndrome anawafunga na anawatesa.

Hamasi safi sana ushahidi unatoka kwa watu wao wenyewe, wacha America na Europe wawaite freedom fighter ni Ma terrorism kwani maneno ya wajinga yanauzwa 😂
 
Mwanamke mzee Muisrael aliyeachiliwa huru na wapiganaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema alikirimiwa na kutendewa wema katika muda wa wiki mbili alipokuwa ameshikiliwa mateka na kundi hilo la wanamapambano wa Palestina.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Yocheved Lifshitz, ajuza wa miaka 85, amesema Hamas ilimpatia daktari wa kushughulikia afya yake na kufanya kila njia kuhakikisha anapata dawa zake.

Ameongeza kuwa wapiganaji wa Hamas walishughulikia pia mahitaji yake. Bi Lifshitz amesema: "tulikula mkate, jibini nyeupe na matango, kama wao."

Bi Kizee huyo Muisrael ameendelea kusimulia alivyokirimiwa na wanamuqawama wa Palestina akisema: "walituambia wanaiamini Qur'ani na kwa hivyo hawatatudhuru".
Alipoulizwa kwa nini alipeana mkono na mmoja wa wanachama wa Hamas wakati wa kuachiliwa kwake, Bi Lifshitz alisema kwa sababu "walliamiliana nasi kwa wema na walishughulikia mahitaji yetu yote."

Jumatatu usiku, tawi la kijeshi la Hamas la Brigedi za Al Qassam lilitangaza kuwa limewaachilia huru mateka wawili wa Israel - Yocheved Lifshitz na Nurit Cooper mwenye umri wa 79 - kwa "sababu za ubinadamu."
Kuna Waisrael wa Kimara, Yombo, Makete, hawataki kabisa hizi habari.
 
Attachments

  • 692ebbf9-95ba-4604-ae3c-fb161faa7f20.mp4
    8.5 MB
Aisee Wayahudi wamemmaindi kichizi huyo mama.

Nimetembelea Website ya Waisrael wanalaumu kuwa kwa nini Serikali haikumanage situation kabla huyo mama hajaongea na vyombo vya habari.
mtando huu hapa: Why did Israel allow a public diplomacy disaster?

Hata Sky news wamenukuu maneno ya huyo mama , wamendika hivi

View attachment 2791685
Katika vita unaweza kutumia huduma kwa mateka kama silaha ya ama kutafuta uungwaji mkono,kuonekana wewe una utu na unajali binadamu ,au kinga dhidi yamashambulizi ya adui. Usidhani hao Hamasi ni wajinga, wanajua wanachokifanya, na ndiyo maana hata humu mmeanza kuwaona kama wana utuw, ni wauji tu. Hata hao mateka wakifa ,watu wa Israel wakawa salama miaka 400 ijayo ni sawa tu ,.wameachiwa.je hawatakufa, jibu ni watakufa.
Maswala ya vita yana mbinu nyingi
 
Na
Wacha we, kumbe kukamata mateka inaruhusiwa. Nikajua ni kitendo cha kigaidi wakati ni utaratibu wa watu fulani.
Vipi suala la kuvamia music festival nalo limeruhusiwa, na la kufyatua maroketi
Nani kakuambia kukamate mateka vitani ni ugaidi? Mateka wanakamata kwa madhumuni mengi sana. Na la kupiga mabomu kwenye makazi ya watu kwa madhumini ya kuuwa watoto, wanawake na vikongwe mbuna haulizungumzii?
 
Huu wa kuteka, kuua na kubaka wanawake kwa kisingizio cha kupigania ardhi huku wakitaja jina la allah
Hizo porojo na chuki zako tu.

Huelewi kuwa sheria zote za kimataifa za mateka wa kivita kupewa haki zao, sheria za kutokuuwa wanawake, watoto na wazeee vitani zilianzishwa na Uislam. Soma Uislam upate faida.

Kuna mwanamke mwandishi wa habari maarufu sana Uingereza anaitwa Yvonne Ridley, alienda kuandika vita vya Afghanistan kwa bahati nzuri akatekwa na Taliban, alivyoachiwa akasilimu. Unaelewa kwanini? Msikilize mwenyewe:

View: https://youtu.be/nFqtZd0y_0g?si=uykOWd8egquo2Oum

Uislam ni mwema sana.

Huyu alikuja mpaka Tanzania akaongea kisa chake hicho Starlight na MUM.

Wewe unangoja nini?
 
RDT_20231024_170657593304608923665346.jpg
 
Kama Hamas ni watu wema, mbona wameua maelfu ya watu baada ya kuivamia na kuishambulia Israel kwa mabomu pamoja na risasi...!!
Waisrael wengi waliuawa na jeshi lao wenyewe walipoanza kurushiana risasi na HAMAS. HAMAS ilienda kuchukua watu wa kuwasaidia kwenye intelijensia yao na ambao watasaidia kushinikiza Israel nayo iachie raia wengi wa Palestina iliyowateka huko nyuma wakiwemo watoto, lakini kwa bahati mbaya IDF ilipofika haikujali maisha ya raia wao. Ikaanza kurusha risasi zilizoua waisrael wenzao wengi.
 
Aisee Wayahudi wamemmaindi kichizi huyo mama.

Nimetembelea Website ya Waisrael wanalaumu kuwa kwa nini Serikali haikumanage situation kabla huyo mama hajaongea na vyombo vya habari.
mtando huu hapa: Why did Israel allow a public diplomacy disaster?

Hata Sky news wamenukuu maneno ya huyo mama , wamendika hivi

View attachment 2791685
Sawa amesema ukweli na kwa sababu wazungu hawapindishi maneno wameripoti hivyo hivyo; ila ukweli unababaki pale pale kuwa HAMAS wanatimiza Agenda ya Uislam ambayo Iko kwenye charter yao ya 1988 inayonukuliwa Toka Sahih Muslim Hadith 2922 kuwa ule mwisho haitokei mpaka Waislam wameua kila Myahudi. Na pia charter hiyo hiyo inasema Uislam utatawala Dunia.
 
Back
Top Bottom