Mateka wa Kiroho: Kutekwa kwa Nafsi badala ya msukule

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,316
Reaction score
871,876
Zamani tulizoea kusikia habari za misukule kule vijijini ambapo mtu anafanywa msukule wa kimwili, anazikwa kisha anaenda kulimishwa mashamba usiku.

Siku hizi ulimwengu wa giza umeweka kambi mijini na vijijini kwa mfumo wa kisasa zaidi...!
hawapotezi muda kuchukua mwili wako, wanateka nafsi yako ukiwa bado unatembea na suti zako mitaani.

Ugonjwa mkubwa wa mateka hawa wa kiroho upo kwenye mzunguko wao wa uchumi. Hapa tunazungumzia utumwa wa kisasa ambapo unakuwa na akili timamu, una kazi nzuri au dili zinazokupa pesa ndefu, lakini uhalisia wa mfuko wako ni wa kilio na kusaga meno.

Pesa unapata kwa jasho, lakini hazikai kabisa; zinayeyuka kama barafu juani bila kufanya maendeleo yoyote ya maana.

Ukweli ni kwamba, wengi wetu tumenaswa kwenye madhabahu za viapo batili zilizowekwa na mababu, ukoo, au hata sisi wenyewe kupitia mahusiano na marafiki wa ajabu.

Hizi madhabahu huwa hazizuii wewe kupata pesa; zinachofanya ni kusubiri ushike mkondo wa fedha, kisha zinarusha mishale ya dharura zisizoisha.
Utasikia gari limeharibika injini ghafla, magonjwa yasioeleweka ndani ya nyumba, starehe bila mipaka au unafanya maamuzi ya hovyo ya kitapeli ambayo ukiisha kufilisika ndio unazinduka na kujiuliza "nilikuwa nina akili gani?".

Huu ni utumwa wa siri wa ulimwengu wa giza ambapo adui amekugeuza wewe kuwa mhudumu (baba wa kambo) wa fedha zako mwenyewe.

Unafanya kazi usiku na mchana, lakini matunda ya jasho lako yanaenda kulisha falme za giza na dharura za kishetani. Unabaki na jina kubwa la mtu mwenye hela, lakini kiuhalisia unamiliki madeni na msongo wa mawazo kuliko hata asiye na ajira.

Kama unahisi unalima lakini huvuni kitu, na pesa zako zinaishia kwenye mifuko yenye matundu, ujue upo chini ya mateka wa kiroho. Kujikomboa hapa hakuhitaji ushauri wa kifedha , kunahitaji kusimama imara kiroho, kubomoa madhabahu za ukoo, na kuvunja kila viapo batili vinavyofyonza jasho lako.
 
Sawa papa👍
6ce600bc-209b-4001-8a54-ee624ce93121.jpeg
 
Umateka wa kiroho kupitia ngono hutokea pale mtu anaposhiriki tendo la ndoa nje ya utaratibu na kuingia kwenye maagano ya siri yanayoruhusu roho za umaskini, laana, au mikosi kuhamia kwake.

Katika ulimwengu wa roho, tendo hili si la kimwili tu bali ni muungano wa nafsi unaoweza kutumiwa na "wanyonya nyota" kufyonza neema, kibali, na akili za kifedha, na kumuacha mtu akiwa mhanga wa kufilisika ghafla, kukaukiwa mawazo ya maendeleo, na kuandamwa na madeni yasiyoisha .

Ili kujikomboa na kurejesha mapato yaliyopotea, ni muhimu kutubu kwa dhati, kutamka kuvunja maagano yote ya zamani ya nafsi, na kuishi maisha ya usafi yanayolinda milango yako ya kiuchumi isishambuliwe tena .
Voodoo Woman.jpeg
 
Kujikomboa hapa hakuhitaji ushauri wa kifedha , kunahitaji kusimama imara kiroho, kubomoa madhabahu za ukoo, na kuvunja kila viapo batili vinavyofyonza jasho lako.
Ili kusimama imara na kuvunja viapo batili, hatua ya kwanza ni toba ya dhati na ya kina. Lazima ukiri makosa yako ya siri na kutubu kwa niaba ya makosa ya mababu zako ili kufuta uhalali wa kisheria unaotumiwa na nguvu za giza kuzuia baraka zako.Baada ya toba, unapaswa kutamka kwa sauti kuvunja maagano yote.

Tamka wazi kubatilisha viapo vyote vya maneno au vya damu vilivyowekwa kiukoo, na ukate kabisa "vifungo vya nafsi" vilivyotokana na ngono nje ya utaratibu ili kuzuia wanyonya nyota kuendelea kufyonza jasho lako.Mwisho, bomoa madhabahu za ukoo kwa kukataa matambiko na kuanzisha madhabahu mpya maishani mwako kupitia maombi ya usiku na ibada thabiti.

Linda milango yako ya kiuchumi kwa kuishi maisha ya usafi, kutoa sadaka kwa uaminifu, na kufanya siri mipango yako mikubwa ya maendeleo.
 
Zamani tulizoea kusikia habari za misukule kule vijijini ambapo mtu anafanywa msukule wa kimwili, anazikwa kisha anaenda kulimishwa mashamba usiku.

Siku hizi ulimwengu wa giza umeweka kambi mijini na vijijini kwa mfumo wa kisasa zaidi...!
hawapotezi muda kuchukua mwili wako, wanateka nafsi yako ukiwa bado unatembea na suti zako mitaani.

Ugonjwa mkubwa wa mateka hawa wa kiroho upo kwenye mzunguko wao wa uchumi. Hapa tunazungumzia utumwa wa kisasa ambapo unakuwa na akili timamu, una kazi nzuri au dili zinazokupa pesa ndefu, lakini uhalisia wa mfuko wako ni wa kilio na kusaga meno.

Pesa unapata kwa jasho, lakini hazikai kabisa; zinayeyuka kama barafu juani bila kufanya maendeleo yoyote ya maana.

Ukweli ni kwamba, wengi wetu tumenaswa kwenye madhabahu za viapo batili zilizowekwa na mababu, ukoo, au hata sisi wenyewe kupitia mahusiano na marafiki wa ajabu.

Hizi madhabahu huwa hazizuii wewe kupata pesa; zinachofanya ni kusubiri ushike mkondo wa fedha, kisha zinarusha mishale ya dharura zisizoisha.
Utasikia gari limeharibika injini ghafla, magonjwa yasioeleweka ndani ya nyumba, starehe bila mipaka au unafanya maamuzi ya hovyo ya kitapeli ambayo ukiisha kufilisika ndio unazinduka na kujiuliza "nilikuwa nina akili gani?".

Huu ni utumwa wa siri wa ulimwengu wa giza ambapo adui amekugeuza wewe kuwa mhudumu (baba wa kambo) wa fedha zako mwenyewe.

Unafanya kazi usiku na mchana, lakini matunda ya jasho lako yanaenda kulisha falme za giza na dharura za kishetani. Unabaki na jina kubwa la mtu mwenye hela, lakini kiuhalisia unamiliki madeni na msongo wa mawazo kuliko hata asiye na ajira.

Kama unahisi unalima lakini huvuni kitu, na pesa zako zinaishia kwenye mifuko yenye matundu, ujue upo chini ya mateka wa kiroho. Kujikomboa hapa hakuhitaji ushauri wa kifedha , kunahitaji kusimama imara kiroho, kubomoa madhabahu za ukoo, na kuvunja kila viapo batili vinavyofyonza jasho lako.

Mkuu mshana jr asante kwa bandiko lako mujarabu kabisa ila naomba utolee ufafanuzi wa jinsi gani mimi kama mtoto nawezaje kubeba mikosi na laana za mababu ijapokuwa nimezaliwa kiroho kwa maji ya ubatizo
 
Hakuna mtu aliyefanikiwa kwa nguvu ya maombi,hata wewe mshana ni shahidi mmoja wapo?
Hata nikitoa shuhuda zangu hutaziamini lakini napenda kukuambia kitu kimoja maombi sahihi na maombi thabiti yana nguvu sana

Nguvu ya maombi kiroho ni uwezo mkubwa wa kimungu unaomwezesha mwanadamu kuunganishwa na ulimwengu wa roho, kubadilisha mambo katika ulimwengu wa kimwili, na kushinda vita vya kiroho. Maombi si maneno tu ya kawaida; ni silaha kuu inayobeba mamlaka na kuachilia nguvu za Mungu zilizofichwa kufanya kazi kwa niaba yako.
 
Mkuu mshana jr asante kwa bandiko lako mujarabu kabisa ila naomba utolee ufafanuzi wa jinsi gani mimi kama mtoto nawezaje kubeba mikosi na laana za mababu ijapokuwa nimezaliwa kiroho kwa maji ya ubatizo
Ubatizo unavunja dhambi ya asili na kuleta utakaso wa kimungu.. Laana za ukoo ziko kwenye kizalia (DNA)

Laana inavyovuruga watu bila kujua imetoka madhabahu gani! | JamiiForums Tanzania Laana inavyovuruga watu bila kujua imetoka madhabahu gani!
 
Back
Top Bottom