Wape na hii wasome.. Halafu usiwaamini maana wengine hawajitambui kama ni matekaNimekosa cha kuchangia
Ngoja wadau waje nisome
Dad umejipangaje na wale wanaosema hizo issue ni fix?
Sawa papa๐Wape na hii wasome.. Halafu usiwaamini maana wengine hawajitambui kama ni mateka
Mateka na watumwa kwenye ulimwengu wa roho | JamiiForums Tanzania Mateka na watumwa kwenye ulimwengu wa roho
Asante sana kwa mada.Unafanya kazi usiku na mchana, lakini matunda ya jasho lako yanaenda kulisha falme za giza na dharura za kishetani. Unabaki na jina kubwa la mtu mwenye hela, lakini kiuhalisia unamiliki madeni na msongo wa mawazo kuliko hata asiye na ajira.
Ili kusimama imara na kuvunja viapo batili, hatua ya kwanza ni toba ya dhati na ya kina. Lazima ukiri makosa yako ya siri na kutubu kwa niaba ya makosa ya mababu zako ili kufuta uhalali wa kisheria unaotumiwa na nguvu za giza kuzuia baraka zako.Baada ya toba, unapaswa kutamka kwa sauti kuvunja maagano yote.Kujikomboa hapa hakuhitaji ushauri wa kifedha , kunahitaji kusimama imara kiroho, kubomoa madhabahu za ukoo, na kuvunja kila viapo batili vinavyofyonza jasho lako.
Zamani tulizoea kusikia habari za misukule kule vijijini ambapo mtu anafanywa msukule wa kimwili, anazikwa kisha anaenda kulimishwa mashamba usiku.
Siku hizi ulimwengu wa giza umeweka kambi mijini na vijijini kwa mfumo wa kisasa zaidi...!
hawapotezi muda kuchukua mwili wako, wanateka nafsi yako ukiwa bado unatembea na suti zako mitaani.
Ugonjwa mkubwa wa mateka hawa wa kiroho upo kwenye mzunguko wao wa uchumi. Hapa tunazungumzia utumwa wa kisasa ambapo unakuwa na akili timamu, una kazi nzuri au dili zinazokupa pesa ndefu, lakini uhalisia wa mfuko wako ni wa kilio na kusaga meno.
Pesa unapata kwa jasho, lakini hazikai kabisa; zinayeyuka kama barafu juani bila kufanya maendeleo yoyote ya maana.
Ukweli ni kwamba, wengi wetu tumenaswa kwenye madhabahu za viapo batili zilizowekwa na mababu, ukoo, au hata sisi wenyewe kupitia mahusiano na marafiki wa ajabu.
Hizi madhabahu huwa hazizuii wewe kupata pesa; zinachofanya ni kusubiri ushike mkondo wa fedha, kisha zinarusha mishale ya dharura zisizoisha.
Utasikia gari limeharibika injini ghafla, magonjwa yasioeleweka ndani ya nyumba, starehe bila mipaka au unafanya maamuzi ya hovyo ya kitapeli ambayo ukiisha kufilisika ndio unazinduka na kujiuliza "nilikuwa nina akili gani?".
Huu ni utumwa wa siri wa ulimwengu wa giza ambapo adui amekugeuza wewe kuwa mhudumu (baba wa kambo) wa fedha zako mwenyewe.
Unafanya kazi usiku na mchana, lakini matunda ya jasho lako yanaenda kulisha falme za giza na dharura za kishetani. Unabaki na jina kubwa la mtu mwenye hela, lakini kiuhalisia unamiliki madeni na msongo wa mawazo kuliko hata asiye na ajira.
Kama unahisi unalima lakini huvuni kitu, na pesa zako zinaishia kwenye mifuko yenye matundu, ujue upo chini ya mateka wa kiroho. Kujikomboa hapa hakuhitaji ushauri wa kifedha , kunahitaji kusimama imara kiroho, kubomoa madhabahu za ukoo, na kuvunja kila viapo batili vinavyofyonza jasho lako.
Hata nikitoa shuhuda zangu hutaziamini lakini napenda kukuambia kitu kimoja maombi sahihi na maombi thabiti yana nguvu sanaHakuna mtu aliyefanikiwa kwa nguvu ya maombi,hata wewe mshana ni shahidi mmoja wapo?
Ubatizo unavunja dhambi ya asili na kuleta utakaso wa kimungu.. Laana za ukoo ziko kwenye kizalia (DNA)Mkuu mshana jr asante kwa bandiko lako mujarabu kabisa ila naomba utolee ufafanuzi wa jinsi gani mimi kama mtoto nawezaje kubeba mikosi na laana za mababu ijapokuwa nimezaliwa kiroho kwa maji ya ubatizo
Ukipata muda nikusanyie maandiko yako yote uniwekee yatengeneze kama documentary nitashukuru sanaUbatizo unavunja dhambi ya asili na kuleta utakaso wa kimungu.. Laana za ukoo ziko kwenye kizalia (DNA)
Laana inavyovuruga watu bila kujua imetoka madhabahu gani! | JamiiForums Tanzania Laana inavyovuruga watu bila kujua imetoka madhabahu gani!