Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 790
- 1,316
Moja ya mistari inayonigusa sana katika biblia, nakunifanya nijitathmini mm mwenyewe ni mtu wa aina gani, ni Mathayo 7:20 "mtawatambua kwa matendo yao"
Wanadamu tuna hulka ya kupenda kuonekana ni watu wema mbele za watu (reputation) wakati kwa kificho tunafanya mambo ambayo tunaona aibu kuhusishwa nayo (character)
Hulka hii haiishii tu kwenye maisha binafsi, ukweli ni kwamba ipo hivyo katika maeneo yote ya maisha yetu ikiwemo siasa na uongozi wa serikali za nchi zetu.
Ni ukweli uliowazi kuwa hakuna kiongozi mwenye tabia ya kuchukua rushwa anayependa ajulikane kwa umma kama mla rushwa. Hata kama umma unaijua tabia yake bado atafanya jitihada za kujisafisha ili aonekane ni mwadilifu.
Changamoto ya hali hii ni kwamba pamoja na jitihada za namna hii kufanyika, anayetuhumiwa, wanaomtetea na wanaoshindwa kumuwajibisha wote hujikuta katika kadhia ya tuhuma hizo hizo hata kama hawakufanya kitendo hisika.
Katika mukadha wa siasa, vitendo visivyofaa, vinapofanywa na viongozi wa chama fulani, na wenye mamlaka wakashindwa kuchukua hatua, matendo ya viongozi hao yatageuka ndio sura inayokitambulisha chama chao kwa wananchi.
Kama chama chochote cha siasa, kinayo nia ya dhati ya kujenga na kudumisha ushawishi wake kwa umma, ni wazi kuwa sera tu hazitoshi! Ni lazima chama kijitenge na matendo ya viongozi wake yasiyokidhi matarajio ya wananchi.
Hatua kama hizo zisipochukuliwa, ni wazi kuwa matendo mabaya ya viongozi wa chama yatachukuliwa kuwa ndio utambulisho rasmi wa hicho chama ambao wanachama wote kwa ujumla wao watajikuta wamevalishwa utambulisho huo.
Ni imani yangu kuwa mkakati mzuri wa uenezi wa itikadi ya chama ni pamoja na kuhakikisha kuwa matendo na maneno ya viongozi, yanaleta matumaini kwa wananchi kuwa jitihada zinafanyika kukidhi matarajio yao.