Material hizi zimepitwa na wakati

Material hizi zimepitwa na wakati

Dirisha la mbao, kwa ma maana ya frame ya mbao na shutters kioo zimepitwa na wakati kwa sababu ya gharama na kufuata ukisasa tu ila it's the best. Jaribu kuuliza bei ya dirisha la mbao then linganisha na aluminium glass windows utajua nini nasema.
 
Ceiling Board ni ngumu sana kuliko gypsum, bado nina imani na ceiling Board
Moto ndio advantage kubwa kwenye Gypsum boards, moto ukishika kwenye mbao kama umefunga ceiling boards nakupa 5mins mzigo umeshashuka ndani ya nyumba na mnaungua wote, unlike Gypsum board. Ndio advantage kubwa hiyo.
 
Old is gold .. Tutakuja kurudi huko
Sahihi kabisa
  • Hiyo wall puty inachakaa ndani ya muda mfupi inabanduka
  • Madirisha ya mbao yanatunza joto katika maeneo ya baridi kali ila ya vyuma yanabenjuliwa sana na wezi
  • Seng'enge ni nzuri sana ikiambatana na bouganvillea inaruhusu air flow ndani
Kwa ufupi kila kimoja hapo kina faida zake
 
Ukitaja kitu kilichopitwa na wakati ni vyema ukaweka mbadala wake
 
Ni hulka ya binadamu kujaribu kufanya vitu vizuri, watanzia tulio wengi tunajipima na tunapimwa mafanikio kimaisha kupitia ujenzi, ukionekana pesa inapita mikoni mwako lakini huna nyumba inayoonekana ni nzuri utakosolewa sana na kupuuzwa kwa kiwango fulani, katika kuzunguka kwangu tanzania, nimejifunza baadhi ya material za ujenzi zinazopatikana kwa wingi mikoani zimepitwa na wakati.

Ukizitumia unaonekana wewe bado sana na hili limefanya ujenzi uwe very very complicated na unapoteza fedha nyingi kiasi kwamba hizo fedha ungezitumia kwingine huenda ungekuwa umetoboa, endelea kuorodhesha vifaa vilivyo pitwa n wakati ili hata sisi wa mikoani tusiendelee kuvitumia mimi nilivyoona vimepitwa ni hivyo,

1. Bati jeupe (huku niliko linaitwa bati la mama mjane)
2. Cement laini inayopigwa sakafuni
3. Chokaa inayopigwa ukutani
4. Maramaru zenye maua
5. Ceiling board
6. Mlango wa chuma
7. Wire za fensi ( wanaita senyenge na waya nyingine
8. Dirisha la mbao
Kuanzia namba sita kitu bado kinatumika
 
Hivi nawezaje kuzuia fungus wa kwenye ukuta? Nmepiga rangi ya mafuta inabanduka tu, km ukuta unaoza
Fungus wanasababishwa na unyevunyevu katika ukuta. Ukipaka rangi ya mafuta au kuweka tiles ni kwamba unyevunyevu utaendelea kuwepo na ukizidi utazibandua hizo rangi au tiles. Kwa sababu hiyo, hatua ya kwanza ni ya kuondoa fungus waliopo. Goldstar ( algaekill) na Robbialac ( antifungal wash) wanaziuza hizo dawa. Ukienda kwa dealer wa rangi watakueleza namna ya kuzitumia. Unaweza pia kuwapigia simu na kuwauliza. Kama hizo fungus ziko kwa nje, paka rangi ya weather guard baada ya kuondoa fungus. Kama ziko ndani basi paka rangi ya wash and wear. Bafuni tunashauriwa kufanya waterproofing kabla ya kufunika kwa tile ili maji yanayotokana na kuoga yasiingie kwenye ukuta. Maji yanapenya kwenye tiles kupitia pale zinapoungana. Ila ushauri mzuri zaidi unaweza kupata kutoka kwa wanaotengeneza rangi. Namba zao ziko kwenye mtandao.
Aidha, rangi za mafuta ni hatari panapotokea moto. Nakushuri uachane nazo kabisa.

Amandla...
 
Ni hulka ya binadamu kujaribu kufanya vitu vizuri, watanzia tulio wengi tunajipima na tunapimwa mafanikio kimaisha kupitia ujenzi, ukionekana pesa inapita mikoni mwako lakini huna nyumba inayoonekana ni nzuri utakosolewa sana na kupuuzwa kwa kiwango fulani, katika kuzunguka kwangu tanzania, nimejifunza baadhi ya material za ujenzi zinazopatikana kwa wingi mikoani zimepitwa na wakati.

Ukizitumia unaonekana wewe bado sana na hili limefanya ujenzi uwe very very complicated na unapoteza fedha nyingi kiasi kwamba hizo fedha ungezitumia kwingine huenda ungekuwa umetoboa, endelea kuorodhesha vifaa vilivyo pitwa n wakati ili hata sisi wa mikoani tusiendelee kuvitumia mimi nilivyoona vimepitwa ni hivyo,

1. Bati jeupe (huku niliko linaitwa bati la mama mjane)
2. Cement laini inayopigwa sakafuni
3. Chokaa inayopigwa ukutani
4. Maramaru zenye maua
5. Ceiling board
6. Mlango wa chuma
7. Wire za fensi ( wanaita senyenge na waya nyingine
8. Dirisha la mbao
Ukijenga nyumba kuendana na fasheni utajutia hapo hiyo fasheni itakapopitwa nayo na wakati. Kuna wakati kulikuwa na mtindo wa kupata nyumba ulioitwa Msumbiji. Hizo nyumba zilijaa Sinza. Sasa hivi sidhani kama kuna mtu ana hamu nazo.
Chagua vifaa kutokana na ubora wake, matumizi yake na bajeti yako. Usimjengee jirani yako. Nyumba sio nguo kuwa utabidili kila msimu.

Amandla...
 
Chokaa imepitwa na wakati kutokana na washindane wake waliokuja ambao ni white cement na baadaye wall puty.

White cement na wall puty wamemzidi chokaa uwezo wa kutengeneza smoothness ukifanya skimming kwa ajili ya maandalizi ya upakaji rangi.Nawasilisha hoja
Kat ya white cement na wall puty kipi Bora zaid
 
Hivyo vyote umetaja havijapitea na wakayi isipokuwa preferences za ujenzi zimebadilishwa na fursa ya kibiashara...

Matumizi ya mbao kwenye ujenzi, mathalani katika kutengeneza madirisha na frame zake itabaki kuwa ni kitu cha muda wote, huwezi iepuka mbao kabisa...
 
Terrazzo floor imeondolewa na wood, granite, porcelain, ceramic marble and glass tiles
Terrazzo inabakia kuwa ndio material Bora kabisa kutumika sehemu zenye maji maji kama Chooni,jikoni na pia kwenye kumbi za watu wengi kama makanisani au Hostel za umma..

Binafsi bado naipenda sitaki hivyo vya kung'aa Sana vya Viwandani.
 
Binafsi bado naipenda sitaki hivyo vya kung'aa Sana vya Viwandani
 
Attachments

  • Screenshot_20221019-083713.png
    Screenshot_20221019-083713.png
    256.6 KB · Views: 22
True ,mtoa mada amesahau kwamba hata tradition house zimepitwa na wakati saizi ni mwendo wa contemporary [emoji116]
Hahahaaaa na hata wewe umesahau kuwa siku hizi watu wanatumia waffle slabs style, unapata eneo juu la kupumzikia au kujenga gorofa Kwa garama nafuu ukicompare na garama za bati mbao na hata kupata eneo
 
Terrazzo inabakia kuwa ndio material Bora kabisa kutumika sehemu zenye maji maji kama Chooni,jikoni na pia kwenye kumbi za watu wengi kama makanisani au Hostel za umma..

Binafsi bado naipenda sitaki hivyo vya kung'aa Sana vya Viwandani.
Uko sahihi kabisa. Na terrazzo haitunzi uchafu kama tiles kwa sababu haina joints nyingi. Grout ya kwenye joint ya tiles mara nyingi sio waterproof na zinapitisha unyevunyevu.

Amandla...
 
Hahahaaaa na hata wewe umesahau kuwa siku hizi watu wanatumia waffle slabs style, unapata eneo juu la kupumzikia au kujenga gorofa Kwa garama nafuu ukicompare na garama za bati mbao na hata kupata eneo
Waffle slab ni style au structural system? Na inahusika vipi na bati?

Amandla...
 
Back
Top Bottom