zerominus10
JF-Expert Member
- Aug 25, 2022
- 8,142
- 13,721
Babu umeruka kipengele cha maelezo yeye alikua anakuingilia ukiwa umelala na kufanya mapenzi na wewe? Unajua unapolielezea jambo lielezee kwa upana sio unaacha magepu mengi hapo umeeleza in general tu hujaeleza in detail kwamba chanzo ni hiki na hiki na hiki na niligundua hivi nikaeleza hivi nikaambiwa hivi maelezo yako bado yana vificho vificho unaficha nini au umeambiwa usiseme tunakupa huyu ila ni siri yako hata ukimwambia mtu usimwambie kila kitu?Ni story ndefu ndugu , Mimi natokea katika ukoo wenye chain ya hayo mambo
Ila nilikubaliana na Huyo kiumbe na kuamua kuishi nae Ndio Nikasalimika
But kabla ya kukubaliana nae nilikutanishwa na watu wajuzi wa hayo mambo waka mkagua kwanza ili kupata kujua kama ni mzuri Au ni mbaya , Walipo mjua kuwa ni mzuri nikashauriwa nikubaliane nae kufanya anavyotaka
Waliniambia endapo nikikataa kuna hatari ya huyo kiumbe kuniua
Maana hapo kabla Alikuwa ananitokea na kunipa matukio mazito mazito yakutisha
Anapiga wanawake Ana wasababishia ajali ana nisababishia ajali mpaka Mimi mwenyewe kuna mwanamke niliwahi kulala nae usiku wa manane akapata kichaa ( kisa alikuwa amelewa )
Niliwahi kwenda barbershop kufanyiwa scrub mwanamke aliyekuwa ana nifanyia scrub akadondoka akazimia kuna siku nilikuwa naenda lodge na mwanamke Nika kamatwa na police wakachukua pesa zote and by that time wakati natokewa na hayo madrama nilikuwa sijui sababu ni nini na ni-matukio ambayo yalikuwa Yana mlolongo wa kufuatana yaani nilikuwa kama Nina andamwa na mikosi mikubwa Sana
So nilikuja kujuaje juaje kuwa ni jini mahaba 👉👉👉 Baada ya hayo madrama akaanza kujitokeza na kuniambia kuwa Anataka nimuoe hapo ndipo palipo kuwa na balaa, Akaanza kuniambia pesa zote ulizokuwa unapata haukuwa ujanja wako ni Mimi ndiye niliyekuwa Nina kupa sasa kama hautaki subiri uone nitakavyo kufilisi
Nikapuuza nikaona kama mazingaombwe tu Na ujinga maana hata mimi pia nilikuwa siamini katika hayo mambo kwanza nilikuwaga ninadhani kwamba ni story za vijiweni na magazetini tu
Basi bwana - Baada ya miezi kama miwili nikaanza kuandamwa na mikosi biashara zikaanza kuyumba vibaya Sana nikawa Nina filisika mpaka nikaanza kuuza vitu vyangu vya ndani ( Hiyo nimekupa Tu ni intro ) 😁😁😁😁🤣🤣
Yaani ni full drama tu inatisha ,