Mateso anayonipa jini mahaba

Mateso anayonipa jini mahaba

Ni story ndefu ndugu , Mimi natokea katika ukoo wenye chain ya hayo mambo

Ila nilikubaliana na Huyo kiumbe na kuamua kuishi nae Ndio Nikasalimika

But kabla ya kukubaliana nae nilikutanishwa na watu wajuzi wa hayo mambo waka mkagua kwanza ili kupata kujua kama ni mzuri Au ni mbaya , Walipo mjua kuwa ni mzuri nikashauriwa nikubaliane nae kufanya anavyotaka

Waliniambia endapo nikikataa kuna hatari ya huyo kiumbe kuniua

Maana hapo kabla Alikuwa ananitokea na kunipa matukio mazito mazito yakutisha

Anapiga wanawake Ana wasababishia ajali ana nisababishia ajali mpaka Mimi mwenyewe kuna mwanamke niliwahi kulala nae usiku wa manane akapata kichaa ( kisa alikuwa amelewa )

Niliwahi kwenda barbershop kufanyiwa scrub mwanamke aliyekuwa ana nifanyia scrub akadondoka akazimia kuna siku nilikuwa naenda lodge na mwanamke Nika kamatwa na police wakachukua pesa zote and by that time wakati natokewa na hayo madrama nilikuwa sijui sababu ni nini na ni-matukio ambayo yalikuwa Yana mlolongo wa kufuatana yaani nilikuwa kama Nina andamwa na mikosi mikubwa Sana

So nilikuja kujuaje juaje kuwa ni jini mahaba 👉👉👉 Baada ya hayo madrama akaanza kujitokeza na kuniambia kuwa Anataka nimuoe hapo ndipo palipo kuwa na balaa, Akaanza kuniambia pesa zote ulizokuwa unapata haukuwa ujanja wako ni Mimi ndiye niliyekuwa Nina kupa sasa kama hautaki subiri uone nitakavyo kufilisi

Nikapuuza nikaona kama mazingaombwe tu Na ujinga maana hata mimi pia nilikuwa siamini katika hayo mambo kwanza nilikuwaga ninadhani kwamba ni story za vijiweni na magazetini tu

Basi bwana - Baada ya miezi kama miwili nikaanza kuandamwa na mikosi biashara zikaanza kuyumba vibaya Sana nikawa Nina filisika mpaka nikaanza kuuza vitu vyangu vya ndani ( Hiyo nimekupa Tu ni intro ) 😁😁😁😁🤣🤣

Yaani ni full drama tu inatisha ,
Babu umeruka kipengele cha maelezo yeye alikua anakuingilia ukiwa umelala na kufanya mapenzi na wewe? Unajua unapolielezea jambo lielezee kwa upana sio unaacha magepu mengi hapo umeeleza in general tu hujaeleza in detail kwamba chanzo ni hiki na hiki na hiki na niligundua hivi nikaeleza hivi nikaambiwa hivi maelezo yako bado yana vificho vificho unaficha nini au umeambiwa usiseme tunakupa huyu ila ni siri yako hata ukimwambia mtu usimwambie kila kitu?
 
Mwenzenu ana matatizo baadhi yenu badala ya kutafuta namna ya kumsaidia mna mkashifu

Hayo mambo yapo na yanawatesa Sana watu tena Sana na sababu kubwa ya kuwafanya watu wateseke na waangamie ni kwasababu jamii imelifumbia macho suala Hilo Kwa kuamini kuwa hayo mambo hakuna Matokeo Yake baadhi ya watu wenye hayo matatizo wanaishi Kwa kuteseka mpaka mauti yanapo wafika bila ya kupata ufumbuzi

Duniani viumbe wenye nguvu na mamlaka makubwa / viumbe intelligence hatuko binaadamu peke yetu , Hii dunia inatisha Sana tena Sana inaogopesha kuna ulimwengu wa Siri Wa Siri unaotawaliwa na hayo madubwasha (Majini/ Mizimu) huo ulimwengu unatesa Sana watu usiombe itokee uwe umezaliwa katika ukoo ambao Una connection na hayo mambo ,Inatisha

Ni Bora kama mtu hujui kitu kukaa kimya na kuto toa comment yoyote ya kum-bully mtu kaa kimya na uwape nafasi watu wenye uzoefu na mambo hayo watoe testimony zao , Nimesoma baadhi ya comment za watu ambazo zina michango negative nimeshangaa Sana ,
Wewe elezea huo ulimwengu wa Siri ni upi na unafanyaje kazi? Kwanini kiumbe kutoka kwenye huo ulimwengu anakuja kuishi na kiumbe wa kwenye ulimwengu huu? Hoja yako nimeielewa kwa mukhtadha huu nitatolea mfano kuna nyumba zina vioo vya alminium ambavyo mtu wa nje hawezi kumuona mtu wa ndani vinaitwa 'one way visibility, see Out but not In' au unaweza kuita 'one way observation mirror'

Mfano wa picha
5mm-6mm-8mm-10mm-12mm-Customized-Interrogation-Room-One-Way-Mirror-Two-Way-Mirror-Glass-for-Ob...jpg

Sasa hicho kioo ndio km sisi na hao viumbe wao wanatuona ila sisi hatuwaoni, hapo unanielewa vizuri maana kwenye kioo km hicho mtu wa ndani tu ndio anaeweza kumuona mtu nje ila mtu wa nje hawezi kamwe kumuona mtu wa ndani

Nimekufafanulia kuhusu huo ulimwengu wa siri kwa uelewa wangu, sasa nataka unipe sababu kwanini hao viumbe wanatoka huko ndani na kuja kuishi viumbe wa huku nje ambao sio ulimwengu wao, toa sababu
 
Babu umeruka kipengele cha maelezo yeye alikua anakuingilia ukiwa umelala na kufanya mapenzi na wewe? Unajua unapolielezea jambo lielezee kwa upana sio unaacha magepu mengi hapo umeeleza in general tu hujaeleza in detail kwamba chanzo ni hiki na hiki na hiki na niligundua hivi nikaeleza hivi nikaambiwa hivi maelezo yako bado yana vificho vificho unaficha nini au umeambiwa usiseme tunakupa huyu ila ni siri yako hata ukimwambia mtu usimwambie kila kitu?
Nope wala haiko hivyo - Yeye ni mwanamke sindio maana kuna mahali nimesema akawa ana niambie nimuoe , Akiwa ana kuingilia Wakati wewe ni mwanaume Hilo ni Pepo tena Baya linapaswa kutolewa, Nainatakiwa ujue kuwa kama ni wachain yakutoka ktk family tree yenu kumshinda ni ngumu wengine wako na power kubwa Sana you can't defeat them ever hayo mambo ya kwenda Kwa mashekhe au wachungaji ili umtoe lazima yata kutokea puani it's either amuue huyo shekhe au akuue wewe Au akikuonea huruma bhasi ana kupiga vifungo vikali Sana utaishi ktk umaskini wa kutupwa mpaka kifo chako
 
Duh!
 
Wewe elezea huo ulimwengu wa Siri ni upi na unafanyaje kazi? Kwanini kiumbe kutoka kwenye huo ulimwengu anakuja kuishi na kiumbe wa kwenye ulimwengu huu? Hoja yako nimeielewa kwa mukhtadha huu nitatolea mfano kuna nyumba zina vioo vya alminium ambavyo mtu wa nje hawezi kumuona mtu wa ndani vinaitwa 'one way visibility, see Out but not In' au unaweza kuita 'one way observation mirror'

Mfano wa pichaView attachment 3126335

Sasa hicho kioo ndio km sisi na hao viumbe wao wanatuona ila sisi hatuwaoni, hapo unanielewa vizuri maana kwenye kioo km hicho mtu wa ndani tu ndio anaeweza kumuona mtu nje ila mtu wa nje hawezi kamwe kumuona mtu wa ndani

Nimekufafanulia kuhusu huo ulimwengu wa siri kwa uelewa wangu, sasa nataka unipe sababu kwanini hao viumbe wanatoka huko ndani na kuja kuishi viumbe wa huku nje ambao sio ulimwengu wao, toa sababu
Aaahh wewe Jamaa maswali yako bhana na wao ni kama watu Wana hisia pia kuna wakati Wana taka kudhihirisha uwepo wao Kwa kutumia binaadamu,

Waki kupenda basi jua ndio hivyo tena imekula kwako wata kuandama mpaka ujute kuzaliwa mpaka ukubali wanachotaka ufanye ndio inakuwa upo huru otherwise utaiona dunia Chungu
 
Nope wala haiko hivyo - Yeye ni mwanamke sindio maana kuna mahali nimesema akawa ana niambie nimuoe , Akiwa ana kuingilia Wakati wewe ni mwanaume Hilo ni Pepo tena Baya linapaswa kutolewa, Nainatakiwa ujue kuwa kama ni wachain yakutoka ktk family tree yenu kumshinda ni ngumu wengine wako na power kubwa Sana you can't defeat them ever hayo mambo ya kwenda Kwa mashekhe au wachungaji ili umtoe lazima yata kutokea puani it's either amuue huyo shekhe au akuue wewe Au akikuonea huruma bhasi ana kupiga vifungo vikali Sana utaishi ktk umaskini wa kutupwa mpaka kifo chako
Bado hujatoa maelezo ya kutosha wewe hali hio ilianzaje anzaje na ilikuchukua muda gani kujua kinachokusibu? Na pia nimekuuliza sababu ni nini namaanisha chanzo ni nini mpaka atoke kwenye ulimwengu huo aje kuishi na wewe kwenye ulimwengu huu? Nmekutolea mfano hapo juu kwa jinsi ilivyo sasa toa sababu
 
Ni story ndefu inahitaji Uzi Mzee for now ridhika na hayo maelezo niliyokupa ,

Ilinichukua Sana kujua kuwa Nina Hilo Tatizo all most 10yrs but now I'm satisfied nimelitatua
 
Kwema.

Naomba niende kwenye mada binafsi nasumbuliwa na jini mahaba kiukweli kama hujawahi kupitia adhabu ya haya madude unaweza kuonana kama vitu vya kufikirika

Mimi binafsi nina umri wa miaka 36 lakini kiuchumi niko kama dogo wa 20+ Yani Kila nachfanya narudishwa nyuma Hatua mia ukianzisha mahusino inatokea tu dharula unachukiwa mazima pia hata kudharauliwa Yani kama Kuna mada inazungumzwa na washikaji nikichangia mada nitatumia nguvu nyingi sana kusikilizia

Mambo ni mengi nimejarbu kuwapigia baadhi ya watumishi wananiombea lakini Hali inabaki pale pale kiukweli nimechoka na hii Hali sifanyi starehe lakini unakuta kwangu ni rahisi kukopesheka kuliko kuingiza naombeni msaada wadau nijinasue vipi kwenye huu mtego nimechoka.

Pia soma
- Rafiki yangu anasumbuliwa na jini mahaba. Je ni namna gani ya kumtoa?
Rabbon Yesu Anakuja
 
Aaahh wewe Jamaa maswali yako bhana na wao ni kama watu Wana hisia pia kuna wakati Wana taka kudhihirisha uwepo wao Kwa kutumia binaadamu,

Waki kupenda basi jua ndio hivyo tena imekula kwako wata kuandama mpaka ujute kuzaliwa mpaka ukubali wanachotaka ufanye ndio inakuwa upo huru otherwise utaiona dunia Chungu
Unasema mpaka ukubari wanachotaka ufanye, hapo unamaanisha wapo kikundi sio mmoja? Na pia utajua wao wanataka ufanye nini? Wewe ulijuaje wanataka ufanye nini walikwambia au uliambiwa na mtu mwingine? Ninajua unaposema unaongea nao hapo unatupiga kamba maana ni suala ambalo haliwezekani hata kwa maelezo yako unasema mwenyewe kwamba masaibu yalikua yanakupata ila hujui yanatoka wapi maana yake huwezi kuongea nao na hata sasa huongei nao kwa hio ni nani aliekwambia wao wanataka nini na aliongea nao vipi? Fungua ulimwengu huo wa Siri na wengine tuujue
 
Ni story ndefu inahitaji Uzi Mzee for now ridhika na hayo maelezo niliyokupa ,

Ilinichukua Sana kujua kuwa Nina Hilo Tatizo all most 10yrs but now I'm satisfied nimelitatua
Babu bado unaacha magepu mengi unasema umelitatua ila husemi umelitatuaje? Unajua unatupiga kamba
 
Unasema mpaka ukubari wanachotaka ufanye, hapo unamaanisha wapo kikundi sio mmoja? Na pia utajua wao wanataka ufanye nini? Wewe ulijuaje wanataka ufanye nini walikwambia au uliambiwa na mtu mwingine? Ninajua unaposema unaongea nao hapo unatupiga kamba maana ni suala ambalo haliwezekani hata kwa maelezo yako unasema mwenyewe kwamba masaibu yalikua yanakupata ila hujui yanatoka wapi maana yake huwezi kuongea nao na hata sasa huongei nao kwa hio ni nani aliekwambia wao wanataka nini na aliongea nao vipi? Fungua ulimwengu huo wa Siri na wengine tuujue
Unanibishia mpaka Mimi sasa ninaye ishi na hivyo viumbe 🤣🤣🤣

Ila humu bwana kila mtu ni mjuaji , Mimi nimetoka tu maelezo kidogo ili nimpatie kuanzisha thread mwanga ajue kuwa Hilo suala sio lake peke yake tupo wengi Sana na kuna ambao tuliofanikiwa kushindq Hiyo Hali , Usidhani kuwa nitaweza kueleza kila kitu kinacho nihusu hapa ktk jukwaa , Kama unadhani kuwa nitaweza kufanya hivyo your completely wrong

Kukubali wanachotaka sindio Nimesha kueleza kumuoa kwani hapa tuna ongelea kuhusu nini !? Si- kuhusu Jini mahaba !?
 
Aaahh wewe Jamaa maswali yako bhana na wao ni kama watu Wana hisia pia kuna wakati Wana taka kudhihirisha uwepo wao Kwa kutumia binaadamu,

Waki kupenda basi jua ndio hivyo tena imekula kwako wata kuandama mpaka ujute kuzaliwa mpaka ukubali wanachotaka ufanye ndio inakuwa upo huru otherwise utaiona dunia Chungu
Unasema wao ni km watu wana hisia pia, ila hauelezi sababu kwanini wanatoka kwenye ulimwengu wao na kuja kuishi na mtu kwenye ulimwengu huu? Nini sababu hapo mboni unaparuka? Unajua jambo lolote ili litokee kuna sababu hata moto hawezi kua moto bila kua na chanzo cha huo moto hata ajali haiwezi kua ajali bila kua na chanzo cha ajali, sasa toa sababu ni nini?

Unaposema hisia bado maelezo yako yanakua hayajatosha yaan kuna magepu bado unayaacha wazi sasa toa sababu inakuaje wao wanakuvaa tu na kuanza kuishi na wewe ilihali wana ulimwengu wao? Sababu ni nini?

Pia unaposema 'Wana taka kudhihirisha uwepo wao Kwa kutumia binaadamu' bado hujatoa sababu kudhihirisha kivipi tolea maelezo vizuri ueleweke
 
Unanibishia mpaka Mimi sasa ninaye ishi na hivyo viumbe 🤣🤣🤣

Ila humu bwana kila mtu ni mjuaji , Mimi nimetoka Tu maelezo kidogo ili nimpatie kuanzisha thread mwanga ajue kuwa Hilo suala sio lake peke yake tupo wengi Sana na kuna ambao tuliofanikiwa kushindq Hiyo Hali , Usidhani kuwa nitaweza kueleza kila kitu kinacho nihusu hapa ktk jukwaa , Kama unadhani kuwa nitaweza kufanya hivyo your completely wrong
Sasa huelezi na hutoi sababu unategemea nini?

Maana ili watu wakuelewe lazima uelezee sababu ya hicho unachoelezea sio kujielezea wewe nimesema toa sababu ya wao kuamua kuja kuishi na wewe ni ipi?
 
Sababu si-nimesha kueleza kuwa jini Anakuwa amekupenda Anataka umuoe unataka sababu ipi tena !?

Ukiona mtu ana fuatwa na jini mahaba sababu kuu huwa ni huyo Jini kutaka mahusiano na Mtu huyo Nasio kingine , Ndio maana anaitwa jini mahaba
 
Polee mkuu Mimi nakuelewa sana, nikishapitia hiyo changamoto, nilikuwa hata nifanye wema Gani kwa mtu mwisho wake nachukiwa sana tena na wakati mwingine unatengenezewa scenario ya kuchukiwa na kila unayekutana nae ...Mungu ni mwema Mimi nimepona kupitia maombi.....though inahitaji kukaza sana kwenye maombi kama ukianza maombi, km ukiombewa na wewe ujiombee
 
💯
 
Back
Top Bottom