Mateso anayonipa jini mahaba

Babu umeruka kipengele cha maelezo yeye alikua anakuingilia ukiwa umelala na kufanya mapenzi na wewe? Unajua unapolielezea jambo lielezee kwa upana sio unaacha magepu mengi hapo umeeleza in general tu hujaeleza in detail kwamba chanzo ni hiki na hiki na hiki na niligundua hivi nikaeleza hivi nikaambiwa hivi maelezo yako bado yana vificho vificho unaficha nini au umeambiwa usiseme tunakupa huyu ila ni siri yako hata ukimwambia mtu usimwambie kila kitu?
 
Wewe elezea huo ulimwengu wa Siri ni upi na unafanyaje kazi? Kwanini kiumbe kutoka kwenye huo ulimwengu anakuja kuishi na kiumbe wa kwenye ulimwengu huu? Hoja yako nimeielewa kwa mukhtadha huu nitatolea mfano kuna nyumba zina vioo vya alminium ambavyo mtu wa nje hawezi kumuona mtu wa ndani vinaitwa 'one way visibility, see Out but not In' au unaweza kuita 'one way observation mirror'

Mfano wa picha

Sasa hicho kioo ndio km sisi na hao viumbe wao wanatuona ila sisi hatuwaoni, hapo unanielewa vizuri maana kwenye kioo km hicho mtu wa ndani tu ndio anaeweza kumuona mtu nje ila mtu wa nje hawezi kamwe kumuona mtu wa ndani

Nimekufafanulia kuhusu huo ulimwengu wa siri kwa uelewa wangu, sasa nataka unipe sababu kwanini hao viumbe wanatoka huko ndani na kuja kuishi viumbe wa huku nje ambao sio ulimwengu wao, toa sababu
 
Nope wala haiko hivyo - Yeye ni mwanamke sindio maana kuna mahali nimesema akawa ana niambie nimuoe , Akiwa ana kuingilia Wakati wewe ni mwanaume Hilo ni Pepo tena Baya linapaswa kutolewa, Nainatakiwa ujue kuwa kama ni wachain yakutoka ktk family tree yenu kumshinda ni ngumu wengine wako na power kubwa Sana you can't defeat them ever hayo mambo ya kwenda Kwa mashekhe au wachungaji ili umtoe lazima yata kutokea puani it's either amuue huyo shekhe au akuue wewe Au akikuonea huruma bhasi ana kupiga vifungo vikali Sana utaishi ktk umaskini wa kutupwa mpaka kifo chako
 
Duh!
 
Aaahh wewe Jamaa maswali yako bhana na wao ni kama watu Wana hisia pia kuna wakati Wana taka kudhihirisha uwepo wao Kwa kutumia binaadamu,

Waki kupenda basi jua ndio hivyo tena imekula kwako wata kuandama mpaka ujute kuzaliwa mpaka ukubali wanachotaka ufanye ndio inakuwa upo huru otherwise utaiona dunia Chungu
 
Bado hujatoa maelezo ya kutosha wewe hali hio ilianzaje anzaje na ilikuchukua muda gani kujua kinachokusibu? Na pia nimekuuliza sababu ni nini namaanisha chanzo ni nini mpaka atoke kwenye ulimwengu huo aje kuishi na wewe kwenye ulimwengu huu? Nmekutolea mfano hapo juu kwa jinsi ilivyo sasa toa sababu
 
Ni story ndefu inahitaji Uzi Mzee for now ridhika na hayo maelezo niliyokupa ,

Ilinichukua Sana kujua kuwa Nina Hilo Tatizo all most 10yrs but now I'm satisfied nimelitatua
 
Rabbon Yesu Anakuja
 
Unasema mpaka ukubari wanachotaka ufanye, hapo unamaanisha wapo kikundi sio mmoja? Na pia utajua wao wanataka ufanye nini? Wewe ulijuaje wanataka ufanye nini walikwambia au uliambiwa na mtu mwingine? Ninajua unaposema unaongea nao hapo unatupiga kamba maana ni suala ambalo haliwezekani hata kwa maelezo yako unasema mwenyewe kwamba masaibu yalikua yanakupata ila hujui yanatoka wapi maana yake huwezi kuongea nao na hata sasa huongei nao kwa hio ni nani aliekwambia wao wanataka nini na aliongea nao vipi? Fungua ulimwengu huo wa Siri na wengine tuujue
 
Ni story ndefu inahitaji Uzi Mzee for now ridhika na hayo maelezo niliyokupa ,

Ilinichukua Sana kujua kuwa Nina Hilo Tatizo all most 10yrs but now I'm satisfied nimelitatua
Babu bado unaacha magepu mengi unasema umelitatua ila husemi umelitatuaje? Unajua unatupiga kamba
 
Unanibishia mpaka Mimi sasa ninaye ishi na hivyo viumbe 🤣🤣🤣

Ila humu bwana kila mtu ni mjuaji , Mimi nimetoka tu maelezo kidogo ili nimpatie kuanzisha thread mwanga ajue kuwa Hilo suala sio lake peke yake tupo wengi Sana na kuna ambao tuliofanikiwa kushindq Hiyo Hali , Usidhani kuwa nitaweza kueleza kila kitu kinacho nihusu hapa ktk jukwaa , Kama unadhani kuwa nitaweza kufanya hivyo your completely wrong

Kukubali wanachotaka sindio Nimesha kueleza kumuoa kwani hapa tuna ongelea kuhusu nini !? Si- kuhusu Jini mahaba !?
 
Unasema wao ni km watu wana hisia pia, ila hauelezi sababu kwanini wanatoka kwenye ulimwengu wao na kuja kuishi na mtu kwenye ulimwengu huu? Nini sababu hapo mboni unaparuka? Unajua jambo lolote ili litokee kuna sababu hata moto hawezi kua moto bila kua na chanzo cha huo moto hata ajali haiwezi kua ajali bila kua na chanzo cha ajali, sasa toa sababu ni nini?

Unaposema hisia bado maelezo yako yanakua hayajatosha yaan kuna magepu bado unayaacha wazi sasa toa sababu inakuaje wao wanakuvaa tu na kuanza kuishi na wewe ilihali wana ulimwengu wao? Sababu ni nini?

Pia unaposema 'Wana taka kudhihirisha uwepo wao Kwa kutumia binaadamu' bado hujatoa sababu kudhihirisha kivipi tolea maelezo vizuri ueleweke
 
Sasa huelezi na hutoi sababu unategemea nini?

Maana ili watu wakuelewe lazima uelezee sababu ya hicho unachoelezea sio kujielezea wewe nimesema toa sababu ya wao kuamua kuja kuishi na wewe ni ipi?
 
Sasa huelezi na hutoi sababu unategemea nini?

Maana ili watu wakuelewe lazima uelezee sababu ya hicho unachoelezea sio kujielezea wewe nimesema toa sababu ya wao kuamua kuja kuishi na wewe ni ipi?
Sababu si-nimesha kueleza kuwa jini Anakuwa amekupenda Anataka umuoe unataka sababu ipi tena !?

Ukiona mtu ana fuatwa na jini mahaba sababu kuu huwa ni huyo Jini kutaka mahusiano na Mtu huyo Nasio kingine , Ndio maana anaitwa jini mahaba
 
Polee mkuu Mimi nakuelewa sana, nikishapitia hiyo changamoto, nilikuwa hata nifanye wema Gani kwa mtu mwisho wake nachukiwa sana tena na wakati mwingine unatengenezewa scenario ya kuchukiwa na kila unayekutana nae ...Mungu ni mwema Mimi nimepona kupitia maombi.....though inahitaji kukaza sana kwenye maombi kama ukianza maombi, km ukiombewa na wewe ujiombee
 
💯
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…