Mateso ya Masheikh wetu

Mateso ya Masheikh wetu

Status
Not open for further replies.
Mkuu mbona mimi sijakusudia shari ?

Mimi nawazungumzia muamsho na huyu mzee wetu.

Tafadhali sana ndugu,hujui lengo langu,bora ukasubiri kwanza
Nisamehe huwa napenda haki sipendi kuona mateso kwa mtu yeyote anapokwa haki yake hata kama siwa itikadi yangu.
 
Magaidi ni hawa walio bomoa nyumba za watu bila fidia na kusababisha vifo na umasikini.
Magaidi ni hawa wanaopora haki ya kuishi ya watanzania ambao wametofautiana nao kimtazamo.
Magaidi ni hawa wanaotishia kuua watu mchana kweupe kwasababu ya madaraka ili waendelee kutafuna pekee yao keki ya taifa.
 
Hayo yalifanyika Somalia wakati wa Siad Barre na Adhabu iliyokuja ndio mpaka leo tunaiyona kaanza kuondoka Raisi na wakafuatia wengine na mpira unaendelea

Ishara za TZ kuja adhabu tunaziona , labda hatujachelewa hizi dhuluma zifutwe na haki itendeke na kuomba msamaha , vyenginevyo tusubiri mateso ya karne nzima
Pole sana. Wewe huelewi kilichofanya rais aliyepita kuwaweka mahabusu. Pia huwezi kuelewa hayo wanayochunguza au waliyochunguza yana madhara gani yakiwekwa hadharani kwa taifa. Mm naamini kiongozi yeyote hana shida na mtu yeyote asiye hatarishi kwa usalama wa nchi. AMANI YA NCHI YETU NI MUHIMU KULIKO MTU WA AINA YEYOTE ANAYETAKA KUIVURUGA.
 
Haki gani walikuwa wanapigania zidi ya waislamu?
Safuher,
Kesi itakaposikilizwa na hukumu kutolewa ndipo ukweli utajulikana.

Lakini inavyoelekea ni kuwa masheikh wetu hawana kesi ya kujibu wako rumande kwa miaka saba.
 
Pole sana. Wewe huelewi kilichofanya rais aliyepita kuwaweka mahabusu. Pia huwezi kuelewa hayo wanayochunguza au waliyochunguza yana madhara gani yakiwekwa hadharani kwa taifa. Mm naamini kiongozi yeyote hana shida na mtu yeyote asiye hatarishi kwa usalama wa nchi. AMANI YA NCHI YETU NI MUHIMU KULIKO MTU WA AINA YEYOTE ANAYETAKA KUIVURUGA.

Ndio wewe unaelewa ?? au unaamini tu ??, Mbona hujatuambia sababu unadhani tu ??? , Jee dhana kwenye dini yako inakubalika ??? Miaka saba umekaa kimya , umeshindwa kuwasaidia polisi kupeleka ushahidi .

Kumbe wewe ni mtu mbaya sana .
 
Hawa mashehe walikamatwa na waislamu rais akiwa JK, Sheni rais Zanzibar, makamu wa kwanza Maalim Seif, makamu wa pili balozi Iddi.
Na ni muislam Sheni ndiye anayeweza kuwatoa maana ndiye aliyewapeleka jela bara.
Wanateswa kwa sababu ya waislam wenzao
 
Waislamu huwa sio watu wa kuamni 100%
Kama mpo seriaz mchagueni lisu wote mpewe haki yenu
 
Mshukuruni JK lasivyo wangeshakua marehemu na kuwasahau.
nasema hivii watatunzwa Hadi pale tutapoona sio kitisho tena

Sheikh Abud rugo wa Mombasa marehem uamsho ndani cost imetulia
Wanaita Islam phobia
 
MATESO YA MASHEIKH WETU

Ananiambia, ‘’Nakwenda sijda natamani nilie kwenye sijda lakini nyoyo hizi ngumu zimekufa ganzi na pengine hata kuta zake zimesinyaa machozi ya wapi ndugu yangu?

Nanyanyuka natazama picha ya Sheikh Ponda katika pingu yuko mahakamani askari magereza anamfungua pingu zake.

Naiambia nafsi yangu pingu hizi kafungwa Sheikh Ponda si kwa kuwa ni jambazi, la hasha, kafungwa pingu hizi kwa kupigania haki za Waislam na wao waheshimike na wapewe kile ambacho wamekuwa wakikipata wengine toka uhuru upatikane mwaka wa 1961,

Naiambia nafsi yangu Sheikh Ponda yamemkuta yale kwa kupigania kile ambacho Waislam walikifikiria watakipata walipokuwa wanapigania uhuru wa Tanganyika.

Taratibu machozi yanatoka nafungua ukurasa mwingine nawaangalia masheikh wetu waliokuwa kifungoni kwa miaka takriban saba hawana kosa lolote na kesi inaahirishwa kwa miaka saba.

Sasa machozi utadhani bomba limefunguka.

Mume wangu anasikia kwikwi yangu ananifuata na kunipa glasi ya maji napokea.

Hasemi lolote kwani kazoea sasa na anajua kinachoniliza.

Nasoma dua na yeye ndiye muitikiaji wangu.

Mwanangu mkubwa siku moja kaniuliza, ‘’Mama unagombana na baba?

Nakusikia usiku unalia.’’

Wakati mwingine nawaona masheikh wengine katika runinga wamevaa kanzu nzuri za kupendeza kwa rangi zake na kofia za kumeremeta na makoti ya thamani juu wametupia kashda wako katika meza kuu na wakubwa wa chama serikali.

Nyuso zao zinang’ara kwa vyakula na vinywaji vizuri.

Inanijia picha ya masheikh wetu wako Segerea wanalalia virago na kupata shida zote za gerezani.

Nawafikira watoto na wake zao huko waliko na shida hizi za maisha.

Najiuliza hawa masheikh wengine vipi wanaweza kuoga na kujipara na kula na kunywa na wale ilhali ndugu zao wako jela wanateseka?

Tuko mezani na mume wangu na watoto wakati wa chakula cha jioni.

Runinga inawaleta masheikh wengine wamekaa na wale wamependeza wanacheka na kufurahi.

Nikiwafikiria masheikh wetu chakula kinanitumbukia nyongo nanyanyuka kimya kimya sitaki wanangu waone nalia nakwenda chumbani kujificha.

Mume wangu ananiambia, ‘’Honey usimsikilize Sheikh Mselem bin Ali akitafsiri Qur’an anakuliza na usidhani kuwa mimi siumii naumia sana lakini mimi mwanamme naweza kujikaza.

Usimsikilize Sheikh Mselem anakuliza Allah anakuelewa.’’
Malaya tu wewe
 
Kusema kweli hatoki mtu

Labda baadae sana
 
Uislamu utatawala dunia haina shaka ni swala la muda tu na mifuko yote ya kidemokrasia itaondoshwa in sha Allah.
 
FISI ni fisi tu mla mizoga kamwe hawezi kuwa binadamu.

Wenzako wanahoji kwanini hao masheikh wasipelekwe mahakamani, ili haki itendeke yaani kujua kama wanayo makosa kinyume chake wewe unaongea utumbo!!!.

Mtu anawekwa rumande kwa miaka 7 bila kufikishwa mahakamani au kuhukumiwa hiyo ni sawa katika nchi inayofuata misingi ya kisheria na haki za binadanu??!!!.
Utapigwa na butwaa zaidi siku ukikutana na misafara ya kuwapeleka mahakamani ili DPP akaiombe mahakama kuahirisha kesi na kisha kuwarejesha mashehe rumande.Mitutu ya mabunduki,ving'ora nk vinatisha kwelikweli.
 
Wa kulaumiwa sana katika hii kadhia ya Masheikh ni Rais wa Zanzibar Dr Shein, kwani yeye anao uwezo wa kusema Masheikh hao warudishwe Zanzibar kuhukumiwa au wapewe dhamana huko Zanzibar au waachiliwe.

Bara tumekuwa kama "dog" tuliyeamrishwa na "master" wetu Zanzibar kuwafunga watuhumiwa kinyume na haki kwa miaka 7.

Shame on Us.
Jurisidiction ya mashtaka wanayoshtakiwa nayo haiko SMZ.Iko kwa Muungano,wa kulaumiwa hapa ni mahakama kuu iliyokubali kuwekwa kwapani muhimili uliojichimbia chini zaidi.Lakini sisi tumefanya nini kuilinda haki ya mashehe na wote wanaoonewa?
 
Hivi kweli watu wanaweza kuonewa hivi bila hatia?,mwenye kuweza kututhibitishia hawa jamaa hawana makosa afanye hivyo pia atukumbushe nini kilitokea hata wakawa huko waliko.
Kesi isikilizwe ili kama wana hatia wapewe adhabu na kama hawana hatia waachiliwe.Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeipa mahakama mamlaka ya kutoa haki .
 
Mwamposa alipo sababisha mauaji kule moshi-Kilimanjaro unadhani alitumia haki yake ya kikatiba vizuri?
Mwamposa yupo gerezani?

Gwajima alipotukana uislamu na waislamu unadhani alitumia haki yake kikatiba vizuri?
Gwajima yupo gerezani?
Huyu Gwajima alishatukana kila mtu na kuchochea ukabila na vurugu.Huyu siyo wa Mungu,ana mtu wake ambaye humtumikia.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom