Lakini, tusisahau kwamba mashahidi wa upinzani ni mawakala wao.
Je, mawakala wao wametoa feedback ipi?
Msingi wowote wa madai yao waanzia kwa feedback kutoka kwa mawakala.
Mawakala wakitokeze na wazungumze na vyombo vya habari na kiongozi wao aeleze shida ya kila kituo cha kupiga kura.
Kwa sasa wanachofanya akina Tundu Lissu, Zitto Kabwe na Freeman Mbowe hakina maana.
Jambo la msingi ni hilo la mawakala na kisha kwenda mahakamani.
Tundu Lissu ni mwanasheria nguli na mwenye uelewa mkubwa sana, hivyo aandae hoja za kisheria na wapeleke hoja hizo mahakamani.
Kama wameamua kuingia barabarani wafanye hivyo na kitaeleweka hukohuko barabarani.