Haika Kimaro
Member
- Dec 25, 2025
- 12
- 42
Jeshi la Polisi mkoa wa Mtwara limesema kuwa, jana Desemba 30,2025 lilimfikisha Mahakamani Mathias Fabian John (25) kwa tuhuma za mauaji ya Samli Napone (42) aliyekuwa fundi ujenzi.
Imetolewa na:
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Mtwara.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linapenda kuujulisha umma kuwa tarehe 30.12.2025 lilimfikisha mahakamani mtuhumiwa Mathias Fabiani John mwenye umri wa miaka 25, mkazi wa Kata ya Shangani kwa tuhuma za mauaji ya Juma Samli Napone (42) fundi ujenzi na mkazi wa mtaa wa Indiani kota Kata ya Shangani Wilaya ya Mtwara.
Tarehe 14.12.2025 mtuhumiwa alimkamata marehemu na kwenda naye katika pori la mikoko ambalo lipo katika fukwe za kata ya shangani na ilipofika tarehe 17.12.2025 majira ya saa sita usiku mwili wa marehemu ulipatikana ukiwa umeanza kuharibika. Awali mtuhumiwa alimtuhumu marehemu kwa kosa la kumuibia pikipiki yake, hata hivyo tukio la kuibiwa kwa pikipiki hiyo halikuripotiwa katika kituo chochote cha Polisi.
Jeshi la Polisi mkoa wa Mtwara linatoa rai kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi badala yake kutumia njia sahihi katika kutatua changamoto zao, ikiwa ni pamoja na kushirikisha taasisi au mamlaka zinazotambulika kisheria ili kumaliza tofauti zao. Jeshi halitakuwa na muhali kwa yeyote atakaye bainika kujichukulia sheria mkononi.