Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Wakati waziri Ndumbaro anapiga mkwara kuvaa jezi za Ubuntu Botho au Etisalat alianza na neno wao kama Serikali hawatanii na alienda mbali kusema nguvu ya vyombo vya dola itatumika kwa yeyote atakaeenda kinyume.
Hii italeta taswrira mbaya huko mbele, sisi kama wananchi tutakuwa tunajuaje lini Serikali inatania na lini inamaanisha? Mwisho tukidakwa kwenye mambo serious tuseme tulijua mnatania 😅
Busara ilikuwa kuchutama na kusema alikosea na kusonga mbele.
Nukuu ya Ndumbaro
"Tunapotaka kusema tunasimamia uzalendo hatutanii na ndio maana tunakaa na viongozi wa Simba na Yanga ili wao nao wawaambie washabiki wao, atakaekwenda kinyume na maelekezo ya Serikali kwenye suala la uzalendo hatuna mswalie mtume nae....
Ukifanya fujo askari watakuchukua wakupeleke unapokaa upumzike mpaka mpira uishe.