Matinyi anasema waziri Ndumbaro alitania, wakati mhusika alisema 'Hatutanii'. Inaondoa uaminifu kwa Serikali

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Wakati waziri Ndumbaro anapiga mkwara kuvaa jezi za Ubuntu Botho au Etisalat alianza na neno wao kama Serikali hawatanii na alienda mbali kusema nguvu ya vyombo vya dola itatumika kwa yeyote atakaeenda kinyume.

Hii italeta taswrira mbaya huko mbele, sisi kama wananchi tutakuwa tunajuaje lini Serikali inatania na lini inamaanisha? Mwisho tukidakwa kwenye mambo serious tuseme tulijua mnatania πŸ˜…

Busara ilikuwa kuchutama na kusema alikosea na kusonga mbele.

Your browser is not able to display this video.

Nukuu ya Ndumbaro
"Tunapotaka kusema tunasimamia uzalendo hatutanii na ndio maana tunakaa na viongozi wa Simba na Yanga ili wao nao wawaambie washabiki wao, atakaekwenda kinyume na maelekezo ya Serikali kwenye suala la uzalendo hatuna mswalie mtume nae....

Ukifanya fujo askari watakuchukua wakupeleke unapokaa upumzike mpaka mpira uishe.
 
Kwani lini serikali hii ilikiwa serious, bwana yule yupo hoi kitandani mkubwa wa mawaziri akasema anachapa kazi, kigamboni wakazindua mradi wa maji wakati hata mabomba chini hayajafukiwa. πŸ˜‚, treni mpaka leo kizungumkuti.

Usimuamini mwanasiasa hata kidogo, hata akikwambia nje mvua inanyesha na kaingia ndani kalowa, usimuamini, toka nje ushuhudie, hata kama unaiona kwenue dirisha na kwenye bati inasikika, toka nje usikite amekodi faya wanamwaga maji. 🀣
 
Hatuna serikali bali genge la wahuni na wezi maofisini
 
Huyo Matinyi ndio anatutania na kujaribu kucheza na akili zetu
Ilifaa

Ndumbaro ndio akanushee Ni sawa sawa aumwe mwingine wewe umsaidie kumeza dawa...

Alaf matinyi alitakiwa arushiwe makopo alicho kifanya Ni manipulation ya wazi wazi kwa sisi wa TZ
 
"Tunapotaka kusema tunasimamia uzalendo hatutanii na ndio maana tunakaa na viongozi wa Simba na Yanga ili wao nao wawaambie washabiki wao, atakaekwenda kinyume na maelekezo ya Serikali kwenye suala la uzalendo hatuna mswalie mtume nae....

Huyu alikuwa serious na sababu ya kuongea huu ujinga ni muendelezo wa ujinga wa wanasiasa wa CCM kujiona wao ndio nchi na nchi ndio wao...

Haya majinga yamejawa kiburi mno...

Natamani FIFA iingilie kati na kutoa adhabu stahiki...
 
Ni mwanasheria yule waziri?
Juzi Chadema wameshangilia ACT Wazalendo ilipoibiwa kura na CCM. Je,Chadema wanatakiwa kukamatwa na Polisi?
Waziri amechemsha.
 
Ila shape ya kichwa cha ndumbaro mwaionaje wakuu
 
Nchi imejaa mazuzu kuanzia juu hadi chini.
Tena Cha ajabu, eti huyo Ndumbaro, tunaaminishwa kuwa ana shahada ya PhD ya Sheria!

Hivi inawezekanaje Kwa mtu kama huyo tunayeaminishwa kuwa amebobea kwenye Sheria, atoe matamshi, ambayo anajua fika kuwa ni kinyume Cha Sheria?πŸ™†
 
Hili sakata ndio linatuonesha ni jinsi gani huko serikalini watu walivyo weupe. Yaani aibu sana, tujitahidi kuwapa watu wanaostahili hizo nafasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…