Matofali yanayofyatuliwa huku mitaani yana ubora mdogo sana

Matofali yanayofyatuliwa huku mitaani yana ubora mdogo sana

Mchanga unanunuliwa kutoka mto msimbazi , mchanga wenye kila aina ya kemikali na alkalini.

Alafu mjenzi anayanunua anaenda kujengea mabondeni😂 .
Hii nchi watu wamevurugwa na CCM, wanafanya mambo hovyo hovyo TU .

Sehemu kubwa sana ya jiji la Dar es salaam ni mapitio ya maji. Either ni mito swamps na mikondo ya bahari.

Mfano mbezi yote ni mkondo wa bahari.

Kijitinyama yote ni njia Kwa ajili ya mito kumwaga maji baharini.

Shughuli zulipaswa kuhamia mkoa wa pwani
Ni changamoto sana ambazo ni kama tumeridhia ziendelee
 
Katika mambo ambayo yanashangaza sana ni uwepo wa matofali yenye ubora mdogo sana huku mtaani ni aibu kubwa sana kwa nchi mamlaka ziko wapi

Mimi nilisoma umbwe miaka flani hivi ile shule imeanza mwaka 1948 ila huwezi amini wakati nasoma ule ukuta wake huwezi gongelea msumari kirahis ilikuwa kwa mbinde sana sijajua sahivi

Mfano leo hii ukiona nyumba inauzwa chanika au chamazi million 15 au 20 fahamu kabisa matofali yaliyotumika kutengenezea hiyo nyumba ni yale yakiguswa tu kidogo na pembe ya kitanda yanaanza kumomonyoka

Na hawa wanaotengeneza wanayatengeneza bila kificho chochote huko mitaani sio sawa kama nchi lazima tuwe na standard bahati mbaya sana hakuna anayejali

Nikiwa rais wa Tanzania

Matofali yanayotengenezwa yatakuwa na standard kubwa na
atakayebainika ametengeneza matofali yenye kiwango kidogo basi atachukuliwa hatua za nidhamu

Na pia kutakuwa na maeneo maalumu ya kutengeneza matofali sio watu wanajichagulia eneo na kuanza kufyatua matofali lazima kutakuwa na utaratibu

Serikali za awali kabla ya uhuru na ile ya awamu ya Kwanza baada ya uhuru zilikua na mipwngo ya miaka 200 mbele.
Hiyo shule ya Umbwe ni shule za zamani hata marumaru na tailis za choo zinauwezo wa kudumu kwa karne Mbili .

Ujenzi wote wa kuanzia miaka ya 90 ni ujenzi wa kihuni .
 
Back
Top Bottom